Hivi huu ulikuwa ushirikina au mazingaombwe?

Tukio hili lilitokea Mombasa Kenya miaka 7 iliyopita...
Asubuhi moja mama mmoja muuza supu mtaani akiwa kainjika sufuria lake la supu ya nyama upenuni ikiendelea kuchemka, mara ghafla lilitokea kundi la nyuki na kuzingira sufuria la supu na kuanza kufyonza supu ya moto
Hili halikuwa tukio la kawaida kwakuwa kwanza nyuki hawapatani na moshi na moto..lakini vilevile vile vyuki hawapatani na chumvi..ni nyuki wa kishirikina pekee ndio wanaweza kutumia hivyo vitu

Kijana mmoja barobaro maarufu sana pale kitaa akajitoa woga na kutafuta ndimu...ili atest uhalisia wa wale nyuki...kama wangeikimbia ndimu basi hakuna shida lakini kama wangekula ndimu basi hapo kulikuwa na shida kwakuwa nyuki na ugwadu ni vitu viwili tofauti kabisa

Kwa mshangao wa wengi nyuki waliokuwa wamezingira sufuria la supu inayochemka na kufyonza kwa raha zao ...ghafla walihamia kwenye vipande vya ndimu iliyoletwa na bwana Erik yule kijana barobaro... Mama muuza supu alikasirika sana japo alikana kuwajua nyuki hao na asili yake

Taharuki ilianza pale baada ya masaa machache bwana Erik kuanza kuugua ugonjwa wa ajabu huku kende na uume vikiwa vimevimba hasa...
Majirani walijaribu tiba ya kila aina ikiwemo maombi nk lakini Erik alifariki kabla ya kutimiza masaa 24

Aisee. Africa hatunaga mzaha eneo ilo.
 
Unazidi sasa, kwani wapi magonjwa yasiyojulikana hakuna?

Hayajulikani sababu hatuna teknolojia nzuri

Corona haijajulikana na wazungu pamoja na sayansi yao
Haaaaa jamani yapo !
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom