Hivi huu udwanzi wa 'Cover' kauleta nani?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,791
15,688
Naona vijana wanaibuka kwa kasi kutengeneza kava badala ya kuutumia mda huo kutengeneza hits zao, huu ni uduanzi, kama kweli nyie ni wasanii si mtengeneze hits zenu? Yaani unakaa unaskilizia staa fulani atoe wimbo ili 'usafirie nyota' yake upitie mgongo wake, dah vijana wa sikuhizi wanapenda dezodezo, hii spidi ya kava naiona kabisa itafikia wakati redioni kava zinakuwa nyingi kuliko nyimbo original.

Mi nnavyoelewa kava zilikuwepo tangu enzi hizo, ila zilikuwa zina maana kubwa, hasa ilikuwa ni kwa ajili ya kuwaenzi ma'legend', mfano Brandy na Ray J walivyofanya another day in paradise ya Phil Collins, Jide alivyofanya Muhogo wa Jang'ombe ya Bi Kidude, Mr. Paul alivyofanya Zuwena ya Marijani, n.k, na nnavyoelewa hizi kava zilikuwa zinafanyika baada ya wimbo original kuwa umeshatoka miaka mingi, hiyo ina make sense, but hii ya kutoka baada ya mwezi mmoja hata hainiingii akilini.

Halafu cha ajabu media zinasapoti huu ujinga, hapo ndo naamini kwamba media zinachangia kuua mziki. Nyie wasanii na Media acheni huu uduanzi aisee!
 
wakitoa zao watu hawan mda wakuwasikiliza ndio mana wanafanya cover za wasafi ili wapate nafas yakukik
 
ulimbukeni tu..
siku hizi wamefanya kama fashion
 
Kufanya cover jambo la kawaida...
Kaangalie ngoma ya another round ya fat joe ina cover ngapi na zimefanyika ndani ya muda gani toka itoke
 
Huku kukaa muda mrefu Nanjilinji kunanifanya nipitwe na mengi, hapa naona nyotanyota tu
 
Cover kama nchi za wenzetu kuna watu zinawapa pesa na umaarufu japo si sana laikn ni mtindo wa kawaida tuu

Kuna cover zna kuwaga kali kulko wimbo yenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom