Hivi huu ubovu ni wa EWURA, au wamiliki wa Vituo Vya Mafuta?

kovidii

Senior Member
May 4, 2020
167
250
Straight to the point, imekua kawaida kwa muda mrefu, mabadiliko ya bei ya mafuta ni kila jumatano ya mwezi husika... either kupanda au kushuka,au kubak palepale, mwezi ulopita tulinufaika na corona huko dunian petrol tukauziwa buku jero.

Ila mwez huu ikapanda kidgo hd 1600, ila mwezi huu July kumekua na kupanda kiholela bila taarifa maalum. Yaani unalala unaamka unakuta imepanda sh mia, Mara sh70 yaani vagalant.

Bila taarifa, bila mazoea ya once per month. Sasa hivi iko 1800+ kwa Dar! Hebu nyie EWURA mlioko humu tufafanulieni huu upandishaji holela mnapandisha nyie au ukaid wa wamilik wa shell?

Shubaaaamit!
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,307
2,000
Siko EWURA, kwa hiyo nakomenti tu kama mpitanjia. Vituo vya Mafuta mengine ikikaribia Jumatano ya kwanza ya mwezi ujao, na wakijua mwezi ujao bei itapanda sana, basi wao hufunga Vituo vyao vya mafuta mpaka ifike siku ya bei mpya. Hii ni ili waweze kuuza mafuta yaliyoko kwa bei mpya.

Nakumbuka Mheshimiwa Mkapa (Apumzike Kwa Amani) alipokuwa madarakani, aliondoa mambo ya bei ya serikali kwenye bei za mafuta. Aliliachia soko liamue. Ndio maana utakuta palikuwa kila kituo cha mafuta na bei yake. Halafu pili aliruhusu kila kampuni kuagiza mafuta yenyewe. Soko huria.
 
kovidii

Senior Member
May 4, 2020
167
250
Siko EWURA, kwa hiyo nakomenti tu kama mpitanjia. Vituo vya Mafuta mengine ikikaribia Jumatano ya kwanza ya mwezi ujao, na wakijua mwezi ujao bei itapanda sana, basi wao hufunga Vituo vyao vya mafuta mpaka ifike siku ya bei mpya. Hii ni ili waweze kuuza mafuta yaliyoko kwa bei mpya...
Sasa tangu juzi vituo vyote vya mafuta Dar Bei wamepaisha... serikali iko wapi!? Au wote wako busy na msiba?
 
chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
7,150
2,000
Zitaifishwe tu hivyo vituo vya mafuta zinazobana mafuta na kupandisha bei kiholela.... mafuta kwenye soko la dunia yalifikwa kugaiwa bure :D bana huku tunauziana buku jero kwenda mbele, hawana hata aibu.
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,307
2,000
Zitaifishwe tu hivyo vituo vya mafuta zinazobana mafuta na kupandisha bei kiholela.... mafuta kwenye soko la dunia yalifikwa kugaiwa bure :D bana huku tunauziana buku jero kwenda mbele, hawana hata aibu.
Tukirudi je kwenye soko huria? Waonaje?
 
Mwetavekha

New Member
Jul 28, 2020
4
45
Straight to the point...imekua kawaida kwa muda mref, mabadiliko ya Bei ya mafuta ni kila jumatano ya mwezi husika..!
Makonda hayupo kila kitu katika jiji la Dsm naona kinarejea katika hali ya mwanzo, tazama uchafu umerudi kama kawaida.
Hawa jamaa wa shell ni hatari sana ila walifyata mkia, na huu muda wa kampeni tutaona mengi..
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
763
1,000
Tukirudi je kwenye soko huria? Waonaje?
Hapa wauzaji si ndio watakua wanapanga na kukubaliana tu na kuuza bei watakavyo kwa umoja kama wanavyofanya makampuni ya simu au ya simenti. Mfano Unakuta Buku unapata mb500 na dakika 10 na SMS 100 (tigo, voda,airtel nk kote wanafanana). Simenti kampuni zote bei inalingana nk
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,252
2,000
Straight to the point...imekua kawaida kwa muda mref, mabadiliko ya Bei ya mafuta ni kila jumatano ya mwezi husika... either kupanda au kushuka,au kubak palepale...mwez ulopita tulinufaika na corona huko dunian petrol tukauziwa buku jero...ila mwez huu ikapanda kdgo hd 1600.ila mwezi huu July kumekua na kupanda kiholela bila taarifa maalum....yaan unalala unaamka unakuta imepanda sh mia...Mara sh70... yaani vagalant!!!...bila taarifa...bila mazoea ya once per month...ss hv iko 1800+ kwa dar!!!heb nyie ewura mlioko humu tufafanulieni...huu upandishaji holela mnapandisha nyie,au ukaid wa wamilik wa shell!!?shubaaaamit!!!
Kituo gani umeweka mafuta 1,800/- hapa Dar? Jana nimeweka Puma kwa bei elekezi.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,252
2,000
Hapa wauzaji si ndio watakua wanapanga na kukubaliana tu na kuuza bei watakavyo kwa umoja kama wanavyofanya makampuni ya simu au ya simenti. Mfano Unakuta Buku unapata mb500 na dakika 10 na SMS 100 (tigo, voda,airtel nk kote wanafanana). Simenti kampuni zote bei inalingana nk
Cartel.
 
sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
763
1,000
Siko EWURA, kwa hiyo nakomenti tu kama mpitanjia. Masheli mengine ikikaribia Jumatano ya kwanza ya mwezi ujao, na wakijua mwezi ujao bei itapanda sana, basi wao hufunga sheli zao mpaka ifike siku ya bei mpya. Hii ni ili waweze kuuza mafuta yaliyoko kwa bei mpya...
Sikuwa nafahamu hii tekniki ya kusubiri jumatano, ahsante kwa kunijuza.

Hili la soko huria, sidhani kama ni suluhu. Kwa maana ya bei kuwa chini ni kama haitawezekana, maana tungeweza kuliona hadi sasa. Bei ikiwa elekezi, sifikiri kama ni kosa kuuza chini ya bei hiyo, isipkuwa ni kosa kuuza juu ya bei iliyopangwa. Labda kama bei huwa zinapanda sababu ya uagizaji mafuta wa pamoja.

Ama nielekeze mkuu jinsi soko huria linavyoweza saidia.
 
Kayoka

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
1,873
2,000
Sio kila kituo cha kujaza mafuta ni mali ya kampuni ya "SHELL" vingine ni vya Puma, Total, Lake, Oilcom, etc
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
51,179
2,000
Siko EWURA, kwa hiyo nakomenti tu kama mpitanjia. Vituo vya Mafuta mengine ikikaribia Jumatano ya kwanza ya mwezi ujao, na wakijua mwezi ujao bei itapanda sana, basi wao hufunga Vituo vyao vya mafuta mpaka ifike siku ya bei mpya. Hii ni ili waweze kuuza mafuta yaliyoko kwa bei mpya...
Nakumbuka enzi hizo nilikuwa na Toyota Mark II, Double Twincam Super Charger, nikazama kituo Cha Big Bon, nikaweka full tank ili nisafiri.

Waliniwekea Mafuta machafu Kama tope, badala ya kusafiri kazi ikawa Ni kutafuta pump mpya, kumwaga Mafuta, kusafisha tank na kuwalipa mafundi.

Mfumo huu wa Sasa ni mzuri Sana, ila Cha kusikitisha Ni kwamba EWURA imewekwa mfukoni mwa wajanja wachache
 
dyuteromaikota

JF-Expert Member
Apr 30, 2013
4,554
2,000
Siko EWURA, kwa hiyo nakomenti tu kama mpitanjia. Vituo vya Mafuta mengine ikikaribia Jumatano ya kwanza ya mwezi ujao, na wakijua mwezi ujao bei itapanda sana, basi wao hufunga Vituo vyao vya mafuta mpaka ifike siku ya bei mpya. Hii ni ili waweze kuuza mafuta yaliyoko kwa bei mpya.

Nakumbuka Mheshimiwa Mkapa (Apumzike Kwa Amani) alipokuwa madarakani, aliondoa mambo ya bei ya serikali kwenye bei za mafuta. Aliliachia soko liamue. Ndio maana utakuta palikuwa kila kituo cha mafuta na bei yake. Halafu pili aliruhusu kila kampuni kuagiza mafuta yenyewe. Soko huria.
Hii ni kweli jana nimezunguka petrol stations 4 wanasema hawana petrol wanauza diesel tu. Nkaja kupata kwenye ya petrol station ya 5 na wanauza 1800 na ushee
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom