Hivi huu ni mpango wa kumaliza twanga pepeta au ni ushindani wa biashara.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huu ni mpango wa kumaliza twanga pepeta au ni ushindani wa biashara....

Discussion in 'Entertainment' started by only83, Mar 9, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hallo wanaJF,

  Hakuna atakayepinga kuwa kwa miaka ya karibuni bendi ya Twanga Pepeta chini ya ASET imekuwa ikifanya vyema kiasi cha kuzifunika bendi zilizojaza wakongo kama FM Academia na nyinginezo..Hakika uwezi taja mafanikio ya Twanga Pepeta bila kumtaja Mama Asha Baraka aka Iron Lady,huyu mama amekuwa mstari wa mbele kulisukuma gurudumu la ASET..Lakini upepo umeanza kuvuma vibaya kwasasa,wanamuziki wengi wanaikimbia hii bendi na katika siku za karibuni zaidi ya wanamuziki 10 wameikimbia mfano Fargeson,Chalz Baba,Liliani Internet,nyamwela,ally akida na wengine wengi..na hawa wengi wanaenda kwenye bendi pinzani za Twanga Pepeta kama Extra Bongo,Akudo nk...Je,huu si mpango madhubuti wa kumuangusha huyu mama jasiri? Au ni ushindani katika biashara.
   
 2. 1

  19don JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  nikukumbushe kdg fargeson aliletwa na ali choki kutoka znz hakuna aliyekuwa anamjua, asha baraka akaamua kuiua bendi ya extra bongo kwa kuchukua wanamuziki wote, nakumbuka siku ya mwisho extra bongo walipiga leaders waimbaji wakiwa wawili tu ali na chokoraa ikapigwa regina tulimbeba chokoraa kwani alihidi haondoki kwenda popote, fitina ya asha baraka kesho yake jumapili kapandishwa jukwaani twanga pepeta ndio ikawa kifo rasmi cha bandi yetu ali akajiunga mchinga, NGOJA NA YEYE AONE MACHUNGU YA ALIYO YAFANYA KWA EXTRA BONGO MIAKA ILE NA BADO
   
 3. Muuza Sura

  Muuza Sura JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,990
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  what goes around comes around!!!!huu ushindani wa biashara naona umeingia mpaka katika uwanja wa nyumbani twanga pepeta pale mango garden kwani opposite kuna uhuru peak wanakula nyomi mpaka wanasahau kwenda kuiangalia twanga
   
 4. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Hii ni muziki iliyojaa rafu za hali ya juu na kila namna... KWanzia fitna, ushirikina, majungu nk nk nk

  Naye huyo Mama amewapiga sana fitna FM Academia, pia kuna mda aliishika sana Media utafikiri Twanga ndio ilikuwa bendi pekee....

  Hivyoo aamke apambane na aendelee na sio kulia-lia....

  Hizo ni kanuni za mchezo huo hata Koffi O'lomide zimemkuta sana kabla Afrika haijamkubali kuwa ye ni gwiji.
   
 5. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mpenzi sana wa muziki wa dansi, bendi hii ya Twanga pepeta ambayo imeanzishwa mwaka 1997 imepitia kwenye misukosuko mingi. Lakini sifa kubwa ya bendi hii ni kutotetereka katika kipindi kigumu. Halafu kinachoisaidia Twanga ni sapoti kubwa ya mashabiki wake. Mashabiki wa Twanga ni sawa na mashabiki wa mpira wa miguu ambao timu wanaoishangilia hata ifungwe goli mia hawaatacha kuipa sapoti timu yao. Pamoja na sifa nilizozitaja bendi ina udhaifu mkubwa wa kuwapa maslahi duni wasanii wake hali inayopolekea ikimbiwe na wanamuziki wake kila kukicha. Udhaifu mwingine wa bendi hii ni wa kiuongonzi, hawataki kuwapa mikataba wasanii wake hali inayotia shaka hatma ya wasanii wenyewe na kuamua kwenda kwenye bendi itakayowapatia mikataba. Kuna methali ya kiswahili inayosema "anaejiona amesimama aangalie asije akaanguka" Twanga pepeta inabidi watafakari kwa kina kuhusu hili tatizo la kukimbiwa na wanamuziki wake kwani sasa hali ni mbaya zaidi. Nitatoa mfano, katika albam ya kumi ya bendi hii kuna waimbaji kama Katapila,Chaz baba, kalala Juniour na chokoraa ambao washatimka.vile kuna repa Ferguson huyo ndie mtunzi wa rap ya kisigino nae ametimka. Kuna densa mahili kama Nyamwela,Danger boy,Otilia Boniface, Aisha Madinda,Queen Suzy na Lilian Internet nao wametimka. Pia kuna mpiga besi mahili anaeitwa Hosea Mgosachi a.k.a Hosea bass nae amechapa lapa.Kwa wale waliokuwa wanakwenda kwenye Live on stage za Twanga watakuwa wanamfahamu mpiga bass kwa mbwembwe zake hasa ikizingatiwa gitaa anayotumia ni wireless. Kumbuka wanamuziki hawa wameondoka katika kipindi cha mwaka mmoja tu. Unategemea nini hapo? Mpaka leo Mashabiki wa Twanga bado wanapenda nyimbo za albam ya kumi iitwayo Mwana Dar es salaam lakini zikipigwa nyimbo hizo zinaboa kwa kuwa sauti za waimbaji wa nyimbo hizo hazipo. Kuna siku Kalala Juniour alikuja kuisalimia Twanga pale Leaders club akapanda jukwaani na kuimba wimbo wa mwisho wa ubaya ni aibu nilishuhudia baadhi ya mashabiki wakimzonga Asha Baraka wakitaka awarudishe kina Kalala Juniour. UKURASA UMEISHA MNSAMEHE
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  ni kawaida sana chakufanya kwa twanga nikupigana. bendi kama twanga ni yamuda mrefu haiwezi kufa kirahisi kwani walisha dominate market,cha kufanya ni kufight na ku win trust again kwa sababu biashara inakuwa nzuri inapokuwa na ushindani na kwa ushindani huu wa bendi za muziki nmeupenda na katika upinzani pesa utumika kwenye mapambano!
   
 7. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #7
  Mar 12, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,879
  Trophy Points: 280
  Vipi yule Victor Nkambi profeshenali keyboard, aka mwana Sumbawanga, yeye bado yupo nao twanga?
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Wanamziki wanahama kwa kuangalia maslahi bwana,we fikiria dau alilopewa chaz baba(15m upfront,laki nane kwa mwezi kama mshaara na contract juu) sio masikhara sheikh.
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Lakini wamepata mwanamuziki mpya. Chuma cha moto. Lazima washike nambari wani kwenye kibao chao kipya.

  Hapo Nape akipiga gitaa na bendi ya Twanga Pepeta.

  [​IMG]

  Nape akisakata kinanda

  [​IMG]

  Nape alilikoroga gitaa la Bass

  [​IMG]

  Nape akipiga drums

  [​IMG]

  Asha Baraka akifurahia mwanamuziki wake mpya.

  [​IMG]
   
 10. jchofachogenda

  jchofachogenda JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Huyu mpiga kinanda bado yupo Twanga Pepeta.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Mar 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tehe tehe kumbe Nape nae ni mdau wa dansi.
   
Loading...