Leo ni siku ya ukimwi duniani, siku ambayo tunakumbushwa kuhusu gonjwa hili,pamoja na mambo mengine pia tunaaswa kutowatenga na kuwanyanyapaa waathirika
na siku hii ya leo napenda kushea nanyi kisa hiki kwa ushauri wenu.
Januari mwaka huu nilienda moro kwenye harusi ya mshkaji wangu na katika pilika za harusi ikatokea tumepewa jukumu la kusimamia vinyaji na binti mmoja makini sana, nakatika mazungumzo yetu tukajuana kumbe na yeye anakaa Dar, basi tukapeana contact
baada kama wiki mbili akanipigia nihudhurie kikao cha harusi ya ndugu yake sinza, hapo ndipo nilipomuona vizuri na kutambua uzuri wake.
Nikavuta subira vikao vikaenda hadi harusi, hiyo ilikua april.
Siku ya kuvunja kamati nikamtolea uvivu nikampa yamoyoni.aliniomba nimpe mda, baada ya wiki akanijibu the same, mtu mzima nikajua nimetolewa nje kiani. Nikaacha kumtafuta, akaanza yeye kuja moto, baada ya muda mambo yakawa shwari majina ikawa ni dear, darling, honey, swetee nk.
Tatizo likawa moja mzigo sipewi, nimesha lala nae mara 3 ananiambia nisiwe na haraka.
Maranyingi tukiwanae anauliza sana mara umepima? Ukijua mpenzi wako vvu utafanyaje? Namengi yanayofanana na hayo, mimi nilikunamjibu juu juu tu naona ananiyeyusha,
nilipombana zaidi akataka tukapime kwanza wote, kwakua nilikua nimemind nikakubali.
Sikuamini nilichosikia na kuona kuwa huyu binti ameathirika mimi nipo ok. Baada ya hapo nikaanza kama kumuogopa hivi.
Ndipo aliponieleza ukweli kuwa alikua anajua kama ana vvu toka mwaka jana na anatumia vidonge, alishindwa kuniambia akaamua kutumia njia hiyo na aliomba ushauri kwa dokta ambaye alitupima, dokta akamwambia aniambie mimi nikapime nae kwa huyo dokta ili atushauri. kisha dokta akatushauri namna salama ya jinsi ya kufanya bila kuniambukiza, hivyo hatuna haja ya kuachana, tena tukitaka tunaweza hata kuzaa watoto salama.
Baada ya hapo kusema kweli mzuka wote umeniisha nikabaki na act upendo kama mwanzo,hata denda nikawa najishtukia, na mbaya kuliko zote nipale tulipopanga tuivunje ile amri ya sita, kilichotokea siku hiyo jogoo likagoma kabisa kuwika.
Masikini binti wawatu muelewa kweli akanambia najua ni hofu usijali tutajaribu asubuhi, nilipo amka nikajifanya naharaka nikaondoka.
Tukapanga tena the same thing happen, basi binti analia tu eti namuona kama mnyama mara namnyanyapaa, akinipigia tuonane labda itokee nikashindwa kwenda basi inakua balaa namtenga, namkimbia nk.
Tuna wiki ya 3 sasa ameniambia maneno makali sana nahataki kuniona tena wala hapokei simu yangu, facebook kanitoa.
Rafiki yake ameniletea mashtaka eti anadai nimemnyanyapaa na kumzalilisha sana.
Naombeni mawazo yenu kama nimemkosea au vipi