Hivi huu nao ni unyanyapaa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi huu nao ni unyanyapaa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Paul S.S, Dec 1, 2010.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Leo ni siku ya ukimwi duniani, siku ambayo tunakumbushwa kuhusu gonjwa hili,pamoja na mambo mengine pia tunaaswa kutowatenga na kuwanyanyapaa waathirika

  na siku hii ya leo napenda kushea nanyi kisa hiki kwa ushauri wenu.
  Januari mwaka huu nilienda moro kwenye harusi ya mshkaji wangu na katika pilika za harusi ikatokea tumepewa jukumu la kusimamia vinyaji na binti mmoja makini sana, nakatika mazungumzo yetu tukajuana kumbe na yeye anakaa Dar, basi tukapeana contact
  baada kama wiki mbili akanipigia nihudhurie kikao cha harusi ya ndugu yake sinza, hapo ndipo nilipomuona vizuri na kutambua uzuri wake.
  Nikavuta subira vikao vikaenda hadi harusi, hiyo ilikua april.
  Siku ya kuvunja kamati nikamtolea uvivu nikampa yamoyoni.aliniomba nimpe mda, baada ya wiki akanijibu the same, mtu mzima nikajua nimetolewa nje kiani. Nikaacha kumtafuta, akaanza yeye kuja moto, baada ya muda mambo yakawa shwari majina ikawa ni dear, darling, honey, swetee nk.
  Tatizo likawa moja mzigo sipewi, nimesha lala nae mara 3 ananiambia nisiwe na haraka.
  Maranyingi tukiwanae anauliza sana mara umepima? Ukijua mpenzi wako vvu utafanyaje? Namengi yanayofanana na hayo, mimi nilikunamjibu juu juu tu naona ananiyeyusha,
  nilipombana zaidi akataka tukapime kwanza wote, kwakua nilikua nimemind nikakubali.
  Sikuamini nilichosikia na kuona kuwa huyu binti ameathirika mimi nipo ok. Baada ya hapo nikaanza kama kumuogopa hivi.
  Ndipo aliponieleza ukweli kuwa alikua anajua kama ana vvu toka mwaka jana na anatumia vidonge, alishindwa kuniambia akaamua kutumia njia hiyo na aliomba ushauri kwa dokta ambaye alitupima, dokta akamwambia aniambie mimi nikapime nae kwa huyo dokta ili atushauri. kisha dokta akatushauri namna salama ya jinsi ya kufanya bila kuniambukiza, hivyo hatuna haja ya kuachana, tena tukitaka tunaweza hata kuzaa watoto salama.
  Baada ya hapo kusema kweli mzuka wote umeniisha nikabaki na act upendo kama mwanzo,hata denda nikawa najishtukia, na mbaya kuliko zote nipale tulipopanga tuivunje ile amri ya sita, kilichotokea siku hiyo jogoo likagoma kabisa kuwika.
  Masikini binti wawatu muelewa kweli akanambia najua ni hofu usijali tutajaribu asubuhi, nilipo amka nikajifanya naharaka nikaondoka.
  Tukapanga tena the same thing happen, basi binti analia tu eti namuona kama mnyama mara namnyanyapaa, akinipigia tuonane labda itokee nikashindwa kwenda basi inakua balaa namtenga, namkimbia nk.
  Tuna wiki ya 3 sasa ameniambia maneno makali sana nahataki kuniona tena wala hapokei simu yangu, facebook kanitoa.
  Rafiki yake ameniletea mashtaka eti anadai nimemnyanyapaa na kumzalilisha sana.

  Naombeni mawazo yenu kama nimemkosea au vipi
   
 2. Mahanjam

  Mahanjam JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 325
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Kaka kwa kweli innabidi umpe heshima zote huyo mdada, coz angetaka kukuharibia angefanya hivyo but she behaved responsibly! I know u need time to digest the info. But don't sideline her , just talk each other through the whole thing whatever decision u make. She cares about u and that's y she thought u should know her status.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Katika watu wanaoukupenda huyo mrembo nambari one.
  Mpe tu hali halisi kwamba unaogopa hasa baada ya kujua status yake mweleze kwa upole kabisa ni muelewa na ataendelea kukuelewa sana
  Ingekuwa mwingine angekuruhusu long ago mle tunda na tena angesisitiza kuwa Condoms hasikii lolote na anakupenda kama roho yake .akikukosa wewe atakata roho kabla ya siku zake
  Na mbaya zaidi angekuconvice mpaka mkala tunda kavu kavu ... what iz next ?
  ooh my god nampa hongera huyo dada mungu amzidishie imani kama hiyo ni wachache wenye mapenzi mema na wenzao
   
 4. s

  seniorita JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  "Love is patient; love is kind; love is not envious or boastful or arrogant or rude. It does not insist on its own way; it is not irritable or resentful; it does not rejoice in wrongdoing, but rejoices in the truth. It bears all things, believes all things, hopes all things, endures all things.
  Love never ends"

  Mpendwa let your decisions be guided by love....and even if you decide not to go far with her; you can still love her....huyo no msichana mwenye busara na anayekupenda ndio maana hajakudhuru...sio wengi wa aina hiyo
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huyo dada ni wa kupigiwa mfano.

  Alishindwa kukutamkia wazi lakini amefanya la maana kukupeleka mkapime wote hivyo kujua status yake. Angetaka angekuambukiza kama wanavyoambukiza wengine.

  Inwezekana kuwa alikuwa hataki aingiwe na mapenzi kwa mwanamme na ndio maana akakataa mwanzo, lakini sasa amekupenda na alijipa tamaa ya kuwa ana chance ya kupendwa na anajuta kwa kuingia kwenye tamaa hiyo.

  Bila ya shaka anajisikia vibaya kuwa hakuna mtu anaeweza kumpenda kwa sababu ana virusi hivyo.

  Ongea nae mkuu taratibu na kwa upole umueleze kuwa una hofu, na kama haikuwezekana kuwa na wewe atatokea mwengine atakaeridhika kuishi nae akiwa na hali hiyo.
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Muheshimu sana huyo dada aisee anakupenda kuliko watu wote angetaka kukumaliza si angefanya hivyo lakini kakuheshimu saa mpaka hapo. Muheshimu mrudi tena kwenye ushauri jinsi ya kujamiiana na mtu + na - inawezekana. Ilaa dah dada mzuri sana
   
 7. M

  Mayu JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu mtafute huyo mdada uongee nae.
  Lakini naomba kuuliza wakati mlipotaka ku do jogoo akagoma kuwika ulimficha au alijua kuwa kunahali kama hiyo? Maana kama hajui atadhani umemvua halafu ukakataa tu na si kama hali halisi
   
 8. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mpe respect huyo dada kwa ujasiri wake na alivyokupenda kwa dhati, but when it comes to sex be frankly that you can't take risk. Hilo ni somo kwako,next time try to make sure mwenzio yuko salama kabla ya kuomba tunda.

  Such human being are very rare to find, just make her feel loved and appreciated!
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu kama ulikuwepo, hiyo ni moja ya sababu iliomfanya akasirike sana
   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  It seems that she is not angry with you but angry with herself.

  Mungu amsaidie kwa kumpa patience
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  mkuu ilibidi nimawambie
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Unajua alipokasirika nakuondoka akisema basi nadhanilikosea sana kuto onyesha juhudi za kumtafuta ilituyaongee badala yake nikaona kama ni njia muafaka ya kumtema.
  Wakuu kwa post zenu nahisi kama nahitaji kufanya kitu, siku wahi kuwaza kama amenifanyia uungwana wahali ya juu, nimelala nae mara tatu tena ktk mazingira ambapo hatukuwa na maandalizi hata ya condom, inamaana angekubali tu, dah.
  Na kwa kuanza blv me or not nimemtumia sms ya upole kuomba tuonane akitoka kazini leo, kanijibu in short sina muda, nika insist akanijibu nimtafute jmosi

  wasi wasi wangu nikuwa itakuwaje ile hali maana mwisho wasiku tuta do, pia nadhani kuna haja ya kurudi kwa yule dokta kwa ushauri zaidi
   
 13. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Paulss

  Usijilazimishe kuwa na mtu kwa sababu unamuonea huruma. Kama moyo wako hauko tayari kuwa pamoja na mtu mwenye VVU basi acha muda upite huku ukiwaza zaidi.

  Kuonana nae na kuzungumza nae ni jambo la kiungwana kabisa, lakini usijekutaka kumuonyesha kuwa 'unampenda' kwa kumwambia mwende mkafanye.

  Onana nae umuombe msamaha umuambie kuwa bado uko kwenye shock na hujui unafanya nini lakini ungependa kuwa kwenye contact nae bado mpaka ujue mawazo yako yakoje.

  Kama amaweza kuishi na VVU kwa muda wote huo nafikiri tayari ana nguvu za kuweza kustahamili mambo mengi tu. Nataraji atakuelewa.
   
 14. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #14
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  mmmmnh yaani huyo dada mbona she's one of her kind....angetake kukupa live live inaonekana ungekula tu lakini she chose to tell u the truth, u need to thank her for saving your life, and just let her know that u are also in shock and need time to digest the news .....do not block her out. be her genuine friend!
   
 15. P

  Paul S.S Verified User

  #15
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Thanx mkuu,
  ur advice are highly appreceated
   
 16. B'REAL

  B'REAL JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 3,107
  Likes Received: 173
  Trophy Points: 160
  ni binadamu wa kuingwaa katika hii dunia,watu wate wangekuwaa kamaa yeyee nazani ngomaa ingepungua.
   
Loading...