Hivi huu mzaha mzaha wake dhidi ya Mke wa aliyemtangulia hawezi Siku moja akaamua Kufanya kweli na akapita nae mazima?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nina Mjumbe wangu wa Nyumba Kumi huwa anapenda mno Kufanya Mizaha inayokaribia na Ukweli na Mke wa aliyekuwa Mjumbe wetu wa Nyumba Kumi na hupenda Kufanya Mizaha yake hiyo pale tu akiwa anazungumza na Halaiki ya Watu ( ambao ni Sisi Wananchi wake ) kiasi kwamba tunahisi labda amekuwa akimtamani huyo Mke wa Mtangulizi wake tokea muda mwingi tu na labda anataka sasa Kumtafunia kwakuwa ana Mamlaka yote ya Ujumbe.

Ila Mke wa Mjumbe Mstaafu ni mzuri sana Jamani halafu tokea Mjumbe Mstaafu muda wake umalizike Mkewe ndiyo amezidi sasa kuwa Mzuri na yawezekana ndiyo maana labda Mjumbe wa sasa wa Nyumba Kumi nae hafichi Hisia zake Kwake na mara kwa mara amekuwa akituonyesha Hadharani Sisi wapiga Kura wake wa Mtaani na huenda muda si mrefu akaamua Kumnyang'anya Mjumbe mwenzie Mkewe.

Je nyie mnadhani huyu Mjumbe wangu ( wetu ) wa Nyumba Kumi hawezi Siku moja Kufanya Kweli na Mstaafu akaishia Kulia tu?
 
jiwe ana kazi sana wmaka huu...kwakweli kila anachokifanya kinatizamwa kwa jicho la pili...!
 
Vp kwani unamtamania shemeji wa aliyemtangulia uwe ww? I hope we ni mwanamke
 
Je nyie mnadhani huyu Mjumbe wangu ( wetu ) wa Nyumba Kumi hawezi Siku moja Kufanya Kweli na Mstaafu akaishia Kulia tu?[/FONT]
kwani kuna tatizo akiliwa?.. si atakuwa mwanamke kapenda!... kama mpaka wamestaafu ila tamaa ya mihogo ipo sisi tufanyaje?.. Mpe pole huyo 'mstaafu' kupenda dogodogo kama mkewew ni dogodogo!..

ila wanaume hatuna umbea kufatiriana mashimo yapi tunayatamani!
 
Nina Mjumbe wangu wa Nyumba Kumi huwa anapenda mno Kufanya Mizaha inayokaribia na Ukweli na Mke wa aliyekuwa Mjumbe wetu wa Nyumba Kumi na hupenda Kufanya Mizaha yake hiyo pale tu akiwa anazungumza na Halaiki ya Watu ( ambao ni Sisi Wananchi wake ) kiasi kwamba tunahisi labda amekuwa akimtamani huyo Mke wa Mtangulizi wake tokea muda mwingi tu na labda anataka sasa Kumtafunia kwakuwa ana Mamlaka yote ya Ujumbe.

Ila Mke wa Mjumbe Mstaafu ni mzuri sana Jamani halafu tokea Mjumbe Mstaafu muda wake umalizike Mkewe ndiyo amezidi sasa kuwa Mzuri na yawezekana ndiyo maana labda Mjumbe wa sasa wa Nyumba Kumi nae hafichi Hisia zake Kwake na mara kwa mara amekuwa akituonyesha Hadharani Sisi wapiga Kura wake wa Mtaani na huenda muda si mrefu akaamua Kumnyang'anya Mjumbe mwenzie Mkewe.

Je nyie mnadhani huyu Mjumbe wangu ( wetu ) wa Nyumba Kumi hawezi Siku moja Kufanya Kweli na Mstaafu akaishia Kulia tu?
Unakoelekea sasa unavuka mpaka.
 
Unakoelekea sasa unavuka mpaka.

Kwani anaelekea wapi??🤣

Kwani hata yule dada aliyetumwa na mjumbe wa nyumba kumi wa mtaa jirani kutuletea mali yetu iliyotaka kutoroshwa naye alisifiwa hivyo hivyo,wakati alipopigiwa simu na mjumbe wetu lakini huyo mjumbe wa mtaa jirani akaamua kumpotezea kwa kumwambia; "achana naye huyo" 🤣🤣.

Hainaga ushemeji hiyo ,😝
 
Kwa tabia hii Jiwe anajipambanua kuwa yeye ni kiranga miongoni mwa viranga. Kama huwa anafanya mzaha basi aachane na hiyo mizaha kutokana na hadhi yake.🤔🤔
 
Back
Top Bottom