Hivi hoja ni uchaguzi umekwisha au uchaguzi umekwishaje?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Hii tabia mbovu ya kusema uchaguzi umekwisha na sasa maisha yaendelee huku kukiwa na sauti za wanaopinga namna uchaguzi ulivyoendeshwa,ni kujidanganya mchana kweupe na zaidi ni kuahirisha matizo na kuondoa kabisa moyo wa kuvumiliana kwa siku za usoni.

Mimi nawashauri wenye mamlaka kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu pamoja na kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kabla ya 2020 vinginevyo tunakaribisha matatizo makubwa zaidi siku zijazo.

Tuache kabisa kujidanganya na hoja za kusema eti uchaguzi umekwisha na sasa tusonge mbele ili hali tunajenga mazingira ya kurudi nyuma kama Taifa kwa siku za usoni.

Tuachene na hii tabia ya kufunika kombe mwanaharamu apite kwani kuna siku anaweza kugoma kupita alafu sijui ndio itakuwaje!
 
1. Ni kweli, uchaguzi umekwisha na kuaja majeruhi wengi sana, hasa wale waliowekeza pesa nyingi wakitegemea zitarudi (na faida) pale mtuwao atakaposhinda.
2. Suala la tume huru tulilipigia kelele sana kipindi cha katiba mpya...lakini kwa tamaa za wanasiasa, waliwekeza nguvuzao zote kwenye muundo wa serikali...matokeoyake mmekuja kuyaona tar 29 October 2015.
 
Hii tabia mbovu ya kusema uchaguzi umekwisha na sasa maisha yaendelee huku kukiwa na sauti za wanaopinga namna uchaguzi ulivyoendeshwa,ni kujidanganya mchana kweupe na zaidi ni kuahirisha matizo na kuondoa kabisa moyo wa kuvumiliana kwa siku za usoni.

Mimi nawashauri wenye mamlaka kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka huu pamoja na kuhakikisha Tume Huru ya Uchaguzi inapatikana kabla ya 2020 vinginevyo tunakaribisha matatizo makubwa zaidi siku zijazo.

Tuache kabisa kujidanganya na hoja za kusema eti uchaguzi umekwisha na sasa tusonge mbele ili hali tunajenga mazingira ya kurudi nyuma kama Taifa kwa siku za usoni.

Tuachene na hii tabia ya kufunika kombe mwanaharamu apite kwani kuna siku anaweza kugoma kupita alafu sijui ndio itakuwaje!
HKigwangalla ,baada ya kusoma post yako ya leo,naomba usome hii mada maana nimegundua kumbe nawe ndio wale wale.

Nyinyi mkishinda sawa,wengine nongwa!

Hii nchi si mali yenu kwani nanyi mmeikuta kama sisi tulivyoikuta na wote tutaicha.
 
Last edited by a moderator:
Wale wasiokubali kushindwa waliwekeza hela nyingi na chafu kwenye uchaguzi na ndiyo hao hao wasioitakia mema nchi hii, wanakaa wanawazia vurugu mara oh nchi itawaliki
 
Hivi ni kina nani wanaotajwa kukopa hela kwenye Chama cha Walimu kwa ajili ya kampeni?Na je watazirudishaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom