Hivi hizi zote ni bendera za Tanzania au macho yangu ndio hayaoni vizuri?

Hero

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
3,932
2,832
Nimekuwa nikijaribu kutafakari sana lakini imefikia niyaweke haya wazi! Kitu kama bendera ni tunu muhimu sana kwa nchi! Lakini nikipita mtaani naona mauzauza sana hasa ktk aina za rangi na nakshi ktk bendera yetu murua hii ya Tanzania.

Naomba mnisaidie kama haya ni shida ya macho yangu tu au nanyi mnaona mauzauza!
Tz.jpg
tz1.png
Tz2.png
Tz3.png
 
Hii nchi ni vurugu tu hata CCM wenyewe hawaeleweki kama ni wanafuata siasa za ujamaa au kibepari. Siku wakijua wanafuata siasa gani watapata muda wa kushughulikia rangi ya bendera....BTW hiyo bendera rangi zake ni blue, nyeusi, njano na kijani au ni blue, nyeusi, dhahabu (gold) na kijani?
 
ukiona kijani kimekolea ujue ni msimu wa vuli/masika...vinginevyo ni kiangazi

njano iliyokoleaaa ni msimu madini yamepatikana kwa wingi na hata TRA wakatangaza ongezeko la patoo

Bluee...ikikolea jua bahari maji yake ni safi na angavu ..vinginevyooo maji ya mito yameingia kwa wingi yakaleta tope baharini

Nyeusi ...naona haijabadilika sanaaa...

mwisho "uchanganyaji wa rangi ni taaluma hivyo watakiwa kuheshimiwa"
 
Kumbuka kung'aa kwa bendera kunatokana na upya na kufifia kunatokana na ukongwe, then material ya rangi iliyotengenezewa, pia kiwanda kilichotengeneza.
Mwisho je huko mtaani wote waliopachika hizo bendera waligaiwa siku moja?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ₜₕₑ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Zote sawa tu ukiwa na njaa huwezi kuwaza tofauti ya rangi. Tutajadili haya mambo utawala huu ukiondoka panapo majaliwa ya Mungu
 
Nimekuwa nikijaribu kutafakari sana lakini imefikia niyaweke haya wazi! Kitu kama bendera ni tunu muhimu sana kwa nchi! Lakini nikipita mtaani naona mauzauza sana hasa ktk aina za rangi na nakshi ktk bendera yetu murua hii ya tanzania.

Naomba mnisaidie kama haya ni shida ya macho yangu tu au nanyi mnaona mauzauza!View attachment 1323844View attachment 1323845View attachment 1323846View attachment 1323847
Bendera za kwanza na ya mwisho kidogo zilitaka kufanana na bendera ya Taifa. Kosa la bendera ya kwanza ni rangi ya bluu inapaswa kuwa bluu ya bahari ambayo ipo bendera ya mwisho, na kosa la bendera ya mwisho ni rangi ya njano badala ya rangi ya dhahabu. Rangi ya njano ipo bendera ya kwanza.

Kwa hiyo rangi zinazokosewa ni njano na bluu.
 
Hapo nimeona bendera mbili za Tanzania na nyingine moja ya SA na nyingine ya Jamaica
 
Hero,
Sasa hapo kosa la nani ? La msanifu au serikali? Je hizo picja umezipata wapi ? Tika kwa wahusika au watu tu tofauti wenye kusanifu hizo bendera ?

Kama zote umezipata serikali kuu hapo tuna paswa kuhoji na kupewa muafaka, ila kinyume na hapo wewe ndio mwenye makosa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom