Hivi hizi nyumba zimetelekezwa?

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,200
1,747
ItNimebahatika kutembelea mkoani kwangu nilikozaliwa baada ya kukulu kakala kibao za kimaisha.

Nikaamua kucheki cheki mitaa ya uswazi maana nimekuta mabadiliko maeneo mengi huku kwetu, nilizaliwa tarehe 25 mtaa wa wa Bugando "B" sitaki ujue sana kuhusu hili, sasa nikaona ninyooshe mpaka mitaa ya Mchafukoga kata ya Igogo Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Kabla sijafika nilipita Pepsi nikapandisha mpaka viwanda vya pamba nikashangaa kuona kuna lami safi kwani since miaka hiyo kulikuwa na mabonde na vumbi ambayo ikipigwa mvua inakua tope jeusi kama lile wanakulaga bata karibu na vyoo.

Nilivyofika Mchafukoga nikawa nazama ndani ndani mpaka shede. Hizi nyumba zimenisikitisha sana sijui kuna watu wanaishi humu, naomba kujua mambo yafuatayo wenyeji japokuwa mimi sio mgeni mitaa hii but zile nyumba zilikuwa zinavutia miaka ya 2005 hivi lakini sasa hivi imekuwaje.

Je zinamilikiwa na nani kwa sasa na nini kinaendelea?

IMG_20191107_163144_0.jpg
IMG_20191107_163102_5.jpg
IMG_20191107_162851_5.jpg

Note
Hizi nyumba zilikuwa za shirika la reli
 
mathsjery mkuu mimi siifahamu hiyo mitaa wala nini ila nimevutiwa na kushangazwa na kitu kimoja,hizo picha mbili za juu,naona kama nyumba zimeezekwa na asbestos.

Sasa kama ni kweli ni asbestos na kwa post yako inaonekana kana kwamba zilikuwa zinavutia 2005,je hiyo 2005 kuna watu walikuwa wanaishi? Labda kwa kuwa upo maeneo hayo hebu ulizia kama ni kweli zimeezekwa kwa asbestos.

Kama ni kweli basi nakushauri tu uwe unapita mbali sana na maeneo hayo.
 
sio kwamba ziliuzwa...na walouziwa walikuwa wanasubiri wakistaafu na kupata kiinua mgongo ndo wazikarabati?
 
mathsjery mkuu mimi siifahamu hiyo mitaa wala nini ila nimevutiwa na kushangazwa na kitu kimoja,hizo picha mbili za juu,naona kama nyumba zimeezekwa na asbestos.

Sasa kama ni kweli ni asbestos na kwa post yako inaonekana kana kwamba zilikuwa zinavutia 2005,je hiyo 2005 kuna watu walikuwa wanaishi? Labda kwa kuwa upo maeneo hayo hebu ulizia kama ni kweli zimeezekwa kwa asbestos.

Kama ni kweli basi nakushauri tu uwe unapita mbali sana na maeneo hayo.
hiv madhara yake ni yap
 
Hizo nyumba ni kweli zilikuwa za TRC, baadaye,zikawa za serikali,ambayo ilianza kuwauzia wafanyakazi waliomudu kununua. Hivyo aliyemudu kununua sehemu alokuwa anaishi alinunua na ambae hakumudu alifanywa mpangaji na mpaka leo wanaendea kulipa kodi. Mambo ni mengi,muda hautoshi.
 
Ni kweli ila nyumba hizo zipo za serkal na trc mm ndio. Na kuna znazomilikiwa ns watu binafsi kwa kuwa waliuziwa na gvt au trc. Mm nilikaa hapo kwa kupanga kwa mtu aliekua akifanya kaz trc ambae alikua ameuziwa. Ila miaka ka 4 au 3 iliyopita serkali ilitaka kuzichukua zote. Mpka sasa cjui kiliendelea nn maana nishatoka huko kitambo.
 
Tetesi kutoka jikoni,, SGR ikitua Mwanza hizo nyumba hazitabaki kama zilivyo,, aidha zitabomolewa zote ili zijengwe za kisasa ama zitafanyiwa ukarabati mkubwa,,
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom