Hivi Hizi Habari za Arumeru kupitia Runinga ya ITV zikekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Hizi Habari za Arumeru kupitia Runinga ya ITV zikekaaje?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Kiresua, Mar 28, 2012.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,202
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wanajamvi?

  Nimekuwa nikifuatilia kwa makini siasa za Arumeru Mashariki kupitia vyombo mbalimbali vya Habari, lakini nimedauti sana juu ya taarifa zinazorushwa na ITV kuihusu CCM, mara nyingi sana warudia picha za mikutano iliyopita kurusha habari mpya. Nafadhaika sana na hawa watangazaji wavituo vya habari binafsi (tilitegemea wangekuwa huru lakini Ka-badasha? mashalaaa!!!) hakuna asiyependa hela lakini miiko ya kazi lazima ingezingatiwa ili kulinda utu na fani husika!!! hebu hata leo angalia taarifa ya habari ya leo kama sio picha ambazo iliwahi kuziona au kama sio basi leo wamekuwa na turnout nzuri!!

  Hili limetokea maranyingi sana nikavumilia sana laikini imezidi sasa na nimeona niliweke hapa... au ni mm mwenyewe naona vibaya? kuna jamaa aliwahi kupost kuhusu picha iliyoonyeshwa ikiwa ni kiangazi wakati siku hiyo kulikuwa na mvua na zaidi baridi ya kufa mtu.

  Mambo haya yangeonyeshwa na TBC nisinge shangaa kabisa kwani tunajua ni kituo kilichoolewa na nani! lakini ITV shame on you!!!
   
 2. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mh! Mh! Mh!
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Ulisafiri? Zipo poa tu na ufo sarooooo!
   
 4. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Sio hao tu, jana Star Tv waliweka picha za cloud kuuuubwa ya watu na Siyo akiwa kwenye Lorry la TOT lakini walipomuonyesha anaongea alionekana akiwa chini ya mti na watu wachache tuuu....
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  pesa ya sisiemu ni shetani mkubwa!
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,087
  Trophy Points: 280
  Ndo maana wakenya waliwachora waandishi wa Tanzania wakimlamba Mkapa miguu

  Kiukweli waandishi wetu wa hapa ni mabomu na ni janga kama majanga mengine tuliyonayo hapa Tz,mfano,jana tu nimeona habari kuhusu CDM na katika ile habari nikashangaa wanaacha habari nzuri ya kisiasa pale Nassari alipokuwa anavalishwa Mgolora na Morani wa kimaasai ikiwa ishara ya kukubalika wao wakaidonyoa ile habari na ikarushwa kana kwamba hiyo siyo habari badala yake wanaonesha helikopta ya CDM

  Hivi kweli unaamua kurusha habari za kisiasa ama kampeni ni kipi kina mantiki kati ya kuonesha ndege imesimama na kuonesha tukio la mtu kupewa heshima ya kukubalika,lipi ni tukio hapo kisiasa?kama kuna waandishi wa ITV humu ndani waje hapa wakanushe ama wanikosoe kwa hili jambo

  Waache kukimbilia pipi na biskuti ipo siku mambo yatawaharibikia hata huku street tu hatutawajali na sie make kwenye social context kila kitu kinaweza kutokea
   
Loading...