Shida iko wapi hapo? Na mwenye kutenda hayo alishakiri hadhaharani kwamba urais ni kazi ngumu na yeye ali-beep tu lakini Kivuitu alipokea simu.Kika siku tunaona watu wanachinjwa kwanza halafu baadaye ndio tunaambiwa walichinjwa kwa sababu wali iba, inakuwa kama vijisababu tuuu.
Naona mwaka unausha hivo mambo ndio hayo hayo.
Kuna shida hapa
Sasa lililobakia ni kuisoma tu namba na kumuombea ili atutumbue bila ganzi.
Uchumi unakuwa kwa mwendo kasi na unategemewa katika robo ya mwisho kukua kwa asilimia 7.9, viwanda vinajengwa kwa kasi, kuliko mwendokasi wenyewe. TRA wanakusanya fedha kutoka kwa naniii na zimekuwa nyingi kiasi ambacho wanazipandikiza kwenye mabenki ili zitoe matunda.
Wahanga wa Tetemeko wameshapatiwa misaada na mahitaji yao. Elimu bure, kuwatoza kodi bure. Hapana kazi tu. Mnataka nini zaidi, enyi wadanganyika?
Mfumo wa ukusanyaji mapato umeboreshwa na wananchi wamehamasika kuekeza vitega uchumi na kufurahia maisha yao ya kimalaika na mwendokasi.
Hakuna shida hapa, kila kitu kinaenda kwa mtindo wa kubana matumizi. Jipange ili ukaze mkanda.
Hivi karibuni zoezi la kuhakiki watu hewa litaanza.