Hivi hizi habari kuhusu hati fungani ni za kweli?

Huwa naskia tu mambo ya hati fungani huko serikalini kuwa kuna 15.6% unaweza ipata kwa kiwango ulichowekeza kila mwaka! Je, kuna ukweli wowote juu ya jambo hili maana hii serikali ya michongo isije ikawa ni mambo ya kalenda kama NSSF wakati mzigo mlikabidhiana kisheria.
View attachment 2052217View attachment 2052218
Kwanini serikali isiunde wakala wa kuwekeza kwenye hati fungani zake yenyewe ili ipate faid yenyewe? 😂🤣
 
Zilonga mbali zitendwa mbali...

ukiona imetajwa hela tena nono inayokuvutia, vuta park-brake kwanza utulie..
 
Wamekuwekea jedwali la muda wa miaka ya kuwekeza na riba za faida ya pesa unayoweza kuwekeza katika muda wa mafungu ya miaka waliyoyaonyesha kwenye jedwali lao. Kiasi cha kuwekeza unachotakiwa kujaza kwenye jedwali hilo ni pesa yako uliyoanyo wewe ambayo ungependa uwakopeshe Serikali.

The moment you invest, you become a very big person kwa sababu:
------Unakuwa umeikopesha Serikali
------Serikali ipo miaka yote na uhakika wa pesa yako kuwepo ni zaidi ya asilimia 100
Yaani hata ikitokea kwa bahati mbaya wewe haupo tena, Serikali yenyewe ipo na pesa yako itaendelea kuwepo!
Kila lakheri
Vipi kama serikali itapata hasara?
 
yaani yule bwana ndio aliwafanyia Hivyo, basi lile jiwe kuu hakika lilipasuka Kwa kishindo kikuu maana sio Kwa kuwakunjia Hivyo aisee
Hebu kadaini mzigo wenu maana zama za washamba na wenye roho mbaya zilishazikwa pale chattle!
Poleni sana ingawa walinda Legasi watasema zilikua pesa za mchongo hata wasikutetemeshe!
Faza wale wamebadilika majina tu vitu ni vile vile!
 
Serikali yenyewe hii ya kuvunjia watu nyumba zao bila kujali wataishi wapi?
Hebu tuwaulize waliowekeza NSSF kwa Maisha yao yote ya kazi mziki wanaousikiliza Mara baada ya. Kustaafu
 
Kwanini usiweke fixed?
Fixed ina muda mfupi na haupati pesa hadi muda utakapofika. Kama ni miezi mitatu, sita au mwaka.

Bond unaweka muda mrefu na hapo katikati unapiga udambwidambwi kwa rate nzuri tu.
 
Fixed ina muda mfupi na haupati pesa hadi muda utakapofika. Kama ni miezi mitatu, sita au mwaka.

Bond unaweka muda mrefu na hapo katikati unapiga udambwidambwi kwa rate nzuri tu.
Hivi fixed huwezi kuweka Muda mrefu say miaka Kumi?
 
Kwanini usiweke fixed?
Fixed ina muda mfupi na haupati pesa hadi muda utakapofika. Kama ni miezi mitatu, sita au mwaka.

Bond unaweka muda mrefu na hapo katikati unapiga udambwidambwi kwa rate nzuri tu.
Hivi fixed huwezi kuweka Muda mrefu say miaka Kumi?
Inawezekana ila ndio kama nilivyosema awali, ukichukua katikati, unaharibu utaratibu huenda usipewe interest mliyokubaliana. Fixed kama fixed inamaana wewe utakuja kuichukua hiyo pesa na interest siku ikiiva (mature).
 
Ili kulinda heshima yako kwa watu waliomo humu jukwaani, tafadhali nakusihi sana usiendelee tena kuchangia kwenye thread hii. Kufanya hivyo kutawafanya wasomaji waendelee kusoma posts zako utakazokuwa unaendelea ku-post humu jukwaani; sawa baba yangu?
Tusipangiane cha kuchangia hapa ama sehemu nyingine.........hunichangii bando
 
katika biashara ukipewa mahesabu rahisi kiasi icho ogopa sana pia ichambue sana iyo biashara au uwekezaji kabla ya kuweka mguu au pesa,
 
Vipi kama serikali itapata hasara?
Hata wakipata hasara hawawezi kushindwa kukulipa wewe kwa sababu wanao uwezo wa kuchukua fedha hata mahali pengine palipo na faida. Kwa mfano, mifuko ya jamii huwa haina hasara kwa sababu ni michango ya watu wanachangia kila mwezi. Bonds zina security guarantee ya 100% kuzidi hata mabenki. Benki huwa zina uwezekano wa kufilisika
 
Back
Top Bottom