Hivi hizi habari kuhusu hati fungani ni za kweli?

Hata wakipata hasara hawawezi kushindwa kukulipa wewe kwa sababu wanao uwezo wa kuchukua fedha hata mahali pengine palipo na faida. Kwa mfano, mifuko ya jamii huwa haina hasara kwa sababu ni michango ya watu wanachangia kila mwezi. Bonds zina security guarantee ya 100% kuzidi hata mabenki. Benki huwa zina uwezekano wa kufilisika
Kabisa mkuu,nmegundua watu wengi hawana uelewa na masuala ya Bonds,wao ni kuponda tu.
Nina jamaa yangu yeye kaweka mil kama 300 hivi..kila mwaka anachukua mil 45 na pia hyo mil 300 inamuwezesha kukopa benki yoyote ikiwa kama dhamana..hvyo kakopa kama mil 100 kwa ajili ya biashara zingine.Nashauri wabongo tuwe tunafuatilia mambo na sio kupinga tu kila jambo.
Hizo hela wanakula hata watoto na wajukuu baadae endapo ukitoweka duniani.
 
dawa ya watu kama hawa ni kuwanyima ubunge, tuone wanavyopractise hayo awazo yao
 
yes nafahamu boss wangu alikua akiweka gawio la faida yake mwisho wa mwaka UTT Amis..na huko akawa anapata around 25m to 30m per annum kwa prior investment ya 300m..na alikua ana option biashara zikyumba anaenda anapunguza 50m letsay anatukopesha
 
Benki kuu za nchi mbalimbali huwa zinauza hatifungani yaani treasury bond,mimi nimewahi kwenda BOT kwa issue nyingine,niliweza kuona ubao wao wa matangazo ukielezea kuhusu hati fungani ambazo tayari zilikiwa zime mature.
 
Sawa mkuu ila nimeskia kuna habari za brokers sijui anataka 2% mara blaah blah gani zingine mara unaweza sijui ukanyimwa percent unayotaka wewe ukaambiwa nafasi zimejaa
Hakuna ukweli wowote.

Inauzwa kwa auction. Ukipata unapewa chako.
 
Bilioni 1nikiamuwa kuanzisha kampuni ya usafirishaji ntabutua faida zaidi ya hiyo.
Inaweekana kweli ukawekeza na ukaingiza fedha zaidi lakini unapaswa utofautishe
Faida kwa jasho lako na
Faida bila jasho lako

Faida na maxmum risk na
Faida na minimum risk

Haziwezi kulingana

Ukiwekeza kweye gvt bonds hauhitaji usimamizi wako wewe unafanya mambo megine unasubiri faida.
Ukiwekeza mwenyewe ni lazima utoke jasho, upambane ili upate faida.

Gvt bond ni kwaajili ya watu wenye mitaji mikubwa
ambao wana uwezo wa kutoa mill 500 bond zikazalisha bila stress na huku wakiendelea na mambo yao mengine.
Lengo ni kupunguza stress pindi biashara ikiyumba nk bado unakuwa na uwezo wa kupata mahitaji yote muhimu huku ukikazana kuweka mambo sawa.

Lakini pia kuna kundi la wastaafu ambao wamefanya kazi kwa muda mrefu wanahitaji kupumzika hii inawafaa sana.



Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Bilioni 1nikiamuwa kuanzisha kampuni ya usafirishaji ntabutua faida zaidi ya hiyo.
Biashara ya bilioni moja bila usimamizi inapukutika yote, kama huwezi kusimamia mwenyewe ni bora kuwekeza kwenye bond unapata faida kidogo lakini ni uhakika kwa asilimia 100.
 
Back
Top Bottom