Hivi hivi vifaa vya kupima mimba (UPT) na vya kupima HIV huwa ni sahihi kwa asilimia 100 kwenye kutoa matokeo?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Habari zenu wana JF? bila kupoteza tym ninaomba kuuliza nilichotegemea kuuliza.

Et ni kwa asilimia ngapi hivi vifaa vya kupima mimba na HIV huwa sahihi katika kutoa matokeo?

Kuna jamaa yangu nilikuwa nikibishana nae ananiambia kuwa aliwahi kupima mkojo kupitia kile kifaa cha kupimia mimba (Urinary Pregnancy Test) na kikatoa matokeo kuwa yeye ni mjamzito wakati yeye ni wakiume (ME).

Ubishi ulianza mara pale nilipotaka kununua kifaa cha kupima HIV ili nicheck afya yangu ndo akawa ameniaminisha hivyo je ni kweli wakuu??
 
Nunua UPT na wewe ujipime kama uko na mimba.

Kile cha kupima HIV ukishamaliza kupima na kusoma majibu kitupe muda huo huo na usikitafute tena maana ukikiangalia baada ya masaa kadhaa kitakupa presha.
 
Nunua UPT na wewe ujipime kama uko na mimba..

Kile cha kupima HIV ukishamaliza kupima na kusoma majibu kitupe muda huo huo na usikitafute tena maana ukikiangalia baada ya masaa kadhaa kitakupa presha.
Ina maana haviko na usahihi wa kihivyo
 
Back
Top Bottom