Hivi hili swala limekaaje, naomba nijuzwe

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wana JF!

Leo nataka tuzungumze swala la wanyama na wanyamapori.

Katika shughuri zangu za kubangaiza za udalali wa nyumba nilimpeleka mama mmoja kupanga nyumba mjini Dar cha ajabu yule mama akumaliza hata mwezi alinipigia sim akitaka nimtafutie sehemu nyingine sababu yule mzee alikuwa anafuga mbwa takribani sita harafu ikifika saa 3 usiku anawafungulia kwa hiyo mama alikuwa anashindwa hata kutoka nje au kuingia ikifika usiku wa mida hio mpk awasiliane na mwenye nyumba.

Hoja yangu ni hii hawa wanaofuga mbwa wote wanapata vibali kutoka serikali,wanavitoa wapi??.Maana nilisikia kwamba kifo cha Kingunge Ngombaru kilitokana na ajari ya mbwa.

Pia nimeona Durbai kule nilipoenda kula bata zangu kuna maboss wanamiliki Chui au Tigger ama Simba ,nchi nyingine mtu anamiliki Tembo .

Kwa hapa Tanzania haya maswala yapo vipi wadau maana nina mpango wa kumiliki Tembo wawili kwa ajiri ya kilimo na Chui mmoja kwa ajiri ya ulinzi badala ya mbwa,nitawachukua wakiwa watoto kabisa niwafuge.

Je Tanzania naweza kufanya hivyo naomba nipewe ufafanuzi jamani.
 

Muone mzee wa field (Kingwa) atakupa majibu mujaarab kabisa kuhusu masuala ya Tembo, hata masuala ya Faru Ndugai utapata kabisa habari zake
 
Mtu kufuga mbwa hakatazwi ila anatakiwa kutoa tahadhari (onyo) kuwa nyumbani kwake kuna mbwa wakali ili anayetaka kupita au kuingia eneo lile ajuwe kuna hatari kama hiyo. Hivyo, hata wakati anapangisha nyumba alitakiw akutoa taarifa hiyo kwa mpangaji wake mapema. Kuhusu ufugaji wa wanyapori kama Simba/ Chui na wengineoo lazima upate kibali kutoka Mamlaka husika (Wizara wa Utalii na Maliasili). Lakini pia unatakiwa kuweka ulinzi mkali kwa wanyama hao ili wasijehatarisha maisha ya watu wengine kama majirani, wapita njia kwa kuweka uzio na kutoa onyo/ tahadhari kama unavyoona katika nyumba za walioweka uzio wa umme, lazima waseme uzio huu ni wa umeme .
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom