Baada ya kuingia madarakani kwa JPM na staili ya kutumbua majipu na kuwabaini wakwepa kodi kumekuwa na ongezeko la makusanyo kwa mwezi ukilinganisha na vipindi vilivyopita. Je ongezeko hili kwa kiasi kikubwa halichangiwi na ARREARS ( kodi ambayo haikukusanywa kipindi cha nyuma)? Kwa miezi ijayo tutegemee kuona ukusanyaji utakuwa kama wa miaka iliyopita na hata kama ni ongezeko litakuwa kidogo kwa sababu hakuna vyanzo vipya vya mapato bali ni vile vile vya zamani.