DASA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 1,031
- 301
Kuna majamaa wawili ambao wanafahamiana kwa muda mrefu tangu wakiwa masomoni, kwa bahati nzuri au mbaya wamejikuta kila mmoja anatarajia kufunga ndoa kwasababu zisizozuilika mwezi wa kumi na moja mwishoni. Sasa kila mmoja ana tatizo la pesa, kwahiyo maandalizi kwao yanakuwa magumu ukizingatia na gharama za kufanya harusi hapa Dar. Sasa walipogundua kwamba matatizo yao yanafanana wameamua kufanya harusi kwa pamoja siku moja na kwamba watashare ukumbi na mambo mengine yote yatakayowezekana kushare. Sasa katika harakati za kupunguza gharama wanafikiria pia kila mmoja awe bestman wa mwenzie na wake zao watarajiwa kila mmoja awe matron wa mwenzie hiyo siku ya harusi.
Sasa jamani hivi hili kweli linawezekana!, kuna mtu ameshawahi shuhudia kitu kama hiki!, na kama inawezekana nashindwa kupata picha kanisani na ukumbini shughuli itakuwa inaendeshwa vipi!.
Sasa jamani hivi hili kweli linawezekana!, kuna mtu ameshawahi shuhudia kitu kama hiki!, na kama inawezekana nashindwa kupata picha kanisani na ukumbini shughuli itakuwa inaendeshwa vipi!.