Mbalamwezi1
JF-Expert Member
- Dec 20, 2013
- 2,071
- 2,010
Habari wakuu, mida ya saa12 asbh nipo zangu Kituoni pale Miyuji nasubiri basi la Machame niende zangu 'R Chuga' saa12 kama na dakika 20 hv Shabiby likapita, dakika km ishirini bdae Machame likapita nikapanda nikaanza safari! Tumekwenda huko katikati ya safari kabla ya kufika wilaya ya chemba naona mshine(arusha express ) inatuovateki, wkt huo Machame limeshafikia spidi ya mwisho mpk kale ka mlio ka wiu wiu wiu wiu wiu!! ka kidhibiti mwendo kakawa kanalia wkt huo arusha express Scania Marcopolo la enzi hizo namba A linaovateki Yutong namba D, nikasema poa!! Tukatembea kufika mbele tukakuta limemishwa check point ya trafiki na sisi pia tukasimamishwa, baadae sisi tukawa wakwanza kuondoka pale, dereva wetu kapiga kiatu wee mpk kale ka alarm kakawa kanalia tena mara paaap! Arusha express hili hapa tena ubavuni likatuovateki tena!! Sasa hapa ndo najiuliza hizi ovateki za scania(ars xpress) ni uwezo wa gari au kuna kitu nyuma ya pazia?! Mimi ninachojua mabasi yote ya safari ndefu yamedhibitiwa yatembee max 80km/hr kwa hyo mwenzako akikutangulia akiwa ktk hyo max spidi huwezi kumuovateki, hii imekaaje wadau km kuna mwenye wazo la tofauti!!