Hivi hili agizo limefikia wapi

N'jomba-N'tu

Member
Aug 17, 2015
55
20
Habari zenu wakuu

Siku kadhaa zilizopita waziri wa kazi na ajira ( mh Jenister Muhagama ) alitoa agizo kwa waajiri kuwapa ajira za kudumu waajiri wao. Akatoa siku 14 kama sikosei ili agizo lake litekelezwe.

Hadi sasa nadhani siku 14 tayari zimeisha. Je lile agizo limefikia wapi?.

Vipi huko ulipo wewe mwajili wako ametekeleza?.
 
Mkuu akhsante sana kwa uzi wako makini.
Mimi kwa upande wangu nimewapandishia mshahara dada msaidizi wa nyumbani na mwangalizi wangu wa shamba langu la mifugo pamoja na kuandika mkataba maalumu kati yetu.Pia nimeanza mchakato wa kuwawekea akiba ya mfuko wa jamii.
Samahani kwa kuwa nje ya mada lakini naamini hizi hatua ni mojawapo ya majukumu ya yaliyo ndani ya Wizara ya Kazi na Ajira
 
Hongera sana, Mungu azidi kukupa uajir na wengine
 
Sidhani kama yatatekelezeka hayo ya Jenister, mbona hata yale ya Jumanne Sagini kule Morogoro hakuna lililofanyiwa kazi, zile kuta za hotel zilizozidi kiwanja halisi bado zipo na maroli makubwa zaidi ya tani 25 yanaingia mpaka kwenye kiini cha mji,

Cha kujiuliza ni je haya maagizo hutolewa ili wapate umaarufu kwenye media au kwa kiongozi mkuu wa nchi au wananchi au ni kweli hali hiyo inawakera toka mioyoni mwao.....,

Mimi nadhani kuna kitu kiongezwe kwenye hayo maagizo yao, kuwa watamke wazi "endapo agizo halitatekelezwa, mimi waziri au katibu mkuu najiuzuru nafasi yangu"
 
Haya maagizo ya jumla jumla na yanayotolewa kwa njia ya mdomo mara nyingi hayatekelezwi. Maana hutolewa kama maoni tu au wishes.

Wizara inapaswa kutembelea waajiri na wafanyakazi wao, kubaini upungufu uliopo, then kuwaandikia barua inayo wataka kurekebisha upungufu walio uona. Lakini ukikaa ofisini na kutoa maagizo ya jumla jumla basi ujue hakuna kitu
 
Hongera Mkuu huyo dada wa nyumbani msalimie sana tupiemo kapicha kake na sisi tumuone
 
Back
Top Bottom