mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,652
- 1,238
Bila shaka wadau wote mpo poa baada ya kuzindushwa na kujivalentainisha vya kutosha.Mimi ndugu wadau kuna kitu nimeona juu ya hili tamasha kuu na zito kitaifa,binafsi sikuona mantiki yoyote ya kitu kama hii kufanyika usiku tena kwa kutozana fedha,nijuavyo mimi vitu vya kijamii kama hivi hufanyika mchana bila malipo yoyote sababu tuu kunakuwa tayari na mashirika husika ambayo yamechangia fedha za kutosha kuendesha shughuli nzima,nikitazama ki undani,malaria inawaathili na kuua watanzania wengi wasio jiweza,sasa hapa kutozana fedha hamuoni kuwa ni kugandamizana kimtindo?Malaria pia huathili sana kina mama na watoto,hivi mnafikiri ni baba gani angemruhusu mama na kichanga chake kwenda kuzindushwa usiku huoa?Ndio maana nikasema hii event nzima ingefanyika kuanzia mida ya asubuhi na kumalizika jioni,bure ili kila mmoja aweze jumuika,kama yalivyokuwa mengine,ya vita juu ya mauaji ya albino,kampeni za tokomeza ukimwi,saratani ya matiti etc!Haya ni mazingira ya kupeana lishe tuu,naona vijana wa bongo flava walikuwa wamechoka vibaya hivyo wakaamua kutengenezewa mazingira ya kula japo kuwa hawashibi,sasa nyie wasanii wetu,kweli kusoma hamjui ila hata picha ya nini kilitakiwa kufanyika nayo hamkuiona?Yaani ile issue ilikuwa batili ile mbaya,wasanii hawakujua wapo pale sababu ya nini,nahisi walijua ni FIESTA,kwasababu walienda nje na mada kabisa,walitakiwa hata kama wanaimba nyimbo zao,wagusie walau hata hako ka slogan ka malaria walau mwanzo au mwisho wa nyimbo zao,lakini wao ni shigide mara mwingine kaishiwa mistari anatupa yori yori,kwanini hatujifunzi kutoka kwa wanaojua?Sehemu kama hizo mshkaji alipoweka yori yori ndipo pa kuweka hizo mada husika,kama tunavyojua siku zote anayemlipa dj ndio huchagua nyimbo,kwa hiyo walistahili kutupa walau picha kuwa hapa ni malaria na si Fiesta.Mwisho napenda kushukuru sana Ray C kwa kumkatisha starehe mkulu kwa vivaz vyake Murua!!Vipi wenzangu mmelionaje hili?