Hivi hii ZINDUKA ni njaa au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi hii ZINDUKA ni njaa au?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Feb 15, 2010.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Bila shaka wadau wote mpo poa baada ya kuzindushwa na kujivalentainisha vya kutosha.Mimi ndugu wadau kuna kitu nimeona juu ya hili tamasha kuu na zito kitaifa,binafsi sikuona mantiki yoyote ya kitu kama hii kufanyika usiku tena kwa kutozana fedha,nijuavyo mimi vitu vya kijamii kama hivi hufanyika mchana bila malipo yoyote sababu tuu kunakuwa tayari na mashirika husika ambayo yamechangia fedha za kutosha kuendesha shughuli nzima,nikitazama ki undani,malaria inawaathili na kuua watanzania wengi wasio jiweza,sasa hapa kutozana fedha hamuoni kuwa ni kugandamizana kimtindo?Malaria pia huathili sana kina mama na watoto,hivi mnafikiri ni baba gani angemruhusu mama na kichanga chake kwenda kuzindushwa usiku huoa?Ndio maana nikasema hii event nzima ingefanyika kuanzia mida ya asubuhi na kumalizika jioni,bure ili kila mmoja aweze jumuika,kama yalivyokuwa mengine,ya vita juu ya mauaji ya albino,kampeni za tokomeza ukimwi,saratani ya matiti etc!Haya ni mazingira ya kupeana lishe tuu,naona vijana wa bongo flava walikuwa wamechoka vibaya hivyo wakaamua kutengenezewa mazingira ya kula japo kuwa hawashibi,sasa nyie wasanii wetu,kweli kusoma hamjui ila hata picha ya nini kilitakiwa kufanyika nayo hamkuiona?Yaani ile issue ilikuwa batili ile mbaya,wasanii hawakujua wapo pale sababu ya nini,nahisi walijua ni FIESTA,kwasababu walienda nje na mada kabisa,walitakiwa hata kama wanaimba nyimbo zao,wagusie walau hata hako ka slogan ka malaria walau mwanzo au mwisho wa nyimbo zao,lakini wao ni shigide mara mwingine kaishiwa mistari anatupa yori yori,kwanini hatujifunzi kutoka kwa wanaojua?Sehemu kama hizo mshkaji alipoweka yori yori ndipo pa kuweka hizo mada husika,kama tunavyojua siku zote anayemlipa dj ndio huchagua nyimbo,kwa hiyo walistahili kutupa walau picha kuwa hapa ni malaria na si Fiesta.Mwisho napenda kushukuru sana Ray C kwa kumkatisha starehe mkulu kwa vivaz vyake Murua!!Vipi wenzangu mmelionaje hili?
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hivi kulikuwa na kuchajiwa kiingilio?? Yani hapo umenijuza vema kabisa Mchajikobe nilidhani ni kitu free entrance.
  Kwa kweli hata mimi sikuona mantiki yoyote hiyo kampeni ya kutokomeza malaria ifanyike usiku tena kwa entrance fee lol jamani mambo yanavyoendeshwa nchi hii ni balaa.
  Kampeni kama hii wangegawa mosquito nets za bure kwa wahudhuriaji au dawa zile za kufulia neti au bahati nasibu ya kushinda something which is related to malaria wagawe vitabu leaflets etc lakini waligeuza kuwa FIESTA.

  Damn administration of this poor country of mine...............!!!!!!!!!!!!
   
 3. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Ilitakiwa kuwa hivyo,lakini ni njaa ndugu yangu ndio zinatumaliza,we unafikiri hata mkulu alistahili kuwapo pale,kiusalama?ilikuwa ni kitu cha kutuma ujumbe tuu,mfano waziri husika na wapambe wake wangeweza maliza yote hayo,hii nchi bana people are always hypnotized!!!
   
 4. M

  Mundu JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watanzania tunapenda vitu vya bure... ule ulikuwa ni mchango tu wa maji ya kunywa ya wasanii wale.
   
 5. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Kwanini watumie mgongo wa malaria kushibisha wasanii,si wabuni mambo yao,bora wangeandaa tamasha kwa ajili ya kuwawezesha watoto wa babu seya,ingeleta maana kidogo nao wangepata kifuta jasho,Ila mitanzania mijinga inajifanya inajua kutumia wakati haina kitu,ilimradi ionekane tuu!!
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  ukiona clouds wapo kwenye jambo fulani, beware, ni walaghai, ni kundi ama genge la wenye kurubuni vijana....kwa malengo yao.
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hakupaswa kabisa kuwa pale wastage of time na resources angefanya salam kwa wananchi thru TV irushwe tu live basi na si kuwa pale tena usiku angetokea snipper akamtia kitu cha paji la uso ingekuwaje????? si pasingetosha????
  Ndo yale yale ya kwenda kwenye misiba sijui ya nani wakati angeweza kutumwa mwakilishi husika.
   
 8. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nahisi harufu nyingine ya kula hela katika hiyo campaign manake hapo wale wazee wa public health na maendeleo ya jamii hela nje nje. Tanzania zaidi ya uijuavyo! Mipango na malengo huwa yanakuwa ni mazuri lakini tatizo huwa linakuja kuwa utekelezaji yaani hapo zitatafunwa hele mpaka noma
   
 9. Prisoner

  Prisoner Senior Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:d
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Ni Kampeni ya Uchaguzi wa Raisi 2010 - Zinduka!
   
 11. JS

  JS JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Na wewe kuwa reasonable what world are you living in??? Vitu vya bure kampeni ya malaria ni vitu vya bure?? Wewe unaona nisawa kabisa kampeni ya jamii watu watozwe kiingilio??? Kwani walienda pale for entartaiment au kuhamasishwa waongeze nguvu kutokomeza malaria??
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,609
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Hicho kivazi cha Ray C kilikuaje mie sikukiona! Wakome kufanya haya mambo usiku ingekuwa mchana sidhani kama huyo binti Ray C angetinga hivyo
   
 13. M

  Mundu JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  he he he ! smile please...

  Hivi wewe pale pangekuwa bila kiingilio, afu ingekuwa mchana... pangetosha??
   
 14. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  kama pasingetosha basi hiyo ingekuwa baraka kuwa na mwitikio utawafikia walengwa anagalua kwa kuwapo kwao!
   
 15. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 30,320
  Likes Received: 29,044
  Trophy Points: 280
  niliona wasanii fulani wamepewa vile vyandarua vyenye dawa,im not sure kama waligawa kwa watu wote,je hamna fungu la hela za viingilio lililopelekwa kwenye mradi wa malaria?isije kuwa watu wanalaumu hapa bila kujua event nzima iliendaje.
   
 16. M

  Mundu JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Easy mchajikobe... sometimes tunakuwa serious sana hata kwa simple things. Was just thinking aloud.

  by the way, kwanini unasema ni heri wangechangiwa watoto wa babu Seya? and why specifically him? au ni mfano tu umetoa?
   
 17. JS

  JS JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,067
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Pangetosha sana kwani kampeni zingine zote za ukimwi sijui nini kwani watu hawatoshagi kwenye viwanja??? Ni kuwa tu na mipangilio mizuri ya ulinzi na logistical issues kila kitu kinaenda poa. all in all doing that thing usiku tena kwa kucharge was ridicolous.

  Na huyo Ray C anayevaa nguo za ajabu mpaka mkulu akasepa fasta kwenye kampeni ya jamii jamani it was not right honestly. hatukuwa kwenye show off of whatever you got under neath your half made clothes hata kama uko sexy kiasi gani ni ulimbukeni tu hakuna lingine.

  Aaaaaaaaaaaaaaaagh i get so pissed of na watu wa nchi hii saa zingine.wai
   
 18. M

  Mundu JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,720
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Unajua madhara ya overcrowding wewe?
   
 19. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wakuu JF
  Hivi Tz mtu akisema wasanii anamaanisha ni waimbaji wa muziki tu? Labda swali la msingi, wako wapi wasanii wa sanaa nyingine? Au hao hawahitaji kuzinduliwa?
   
 20. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hili nililiona sikuona sababu ya mkulu kuwatupia sifa nyingi wa bongo flava,anahisi akiwatumia hao mambo itakuwa byee,lakini mitanzania mijinga haioni hii itampa tuu kura,kisa ukijani na majani yao!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...