Hivi hii ya serikali nzima kuhamia kwenye mazishi imekaaje?

Ni jambo la kushangaza sana unakuta Rais anakwenda kuaga msiba Muhimbili wa Muandishi wa Habari...kwa haraka haraka utaona jinsi vioongozi wasivyojittambua Rais misiba mingine anaweza hata kuwakilishwa lakini sasa imekua kama jambo la kawaida kwa Kiongozi kuanzisha ratiba hata isipokuwepo....mi sielewi hawa viongozi wanajitambua au ndio bora liende? Ndio maana unakuta viongozi wote wa Nchi wanajaa kwenye Msiba mmoja naomba sana Hawa Boko haramu wasije kuja Tanzania tutakuja kuwa na misiba mingi.
 
kila mtanzania ana umuhimu wake na mchango wake , mbona juzi Jk alimtembelea comedian Vengu, Mwanamziki Mgurumo na mwanamichezo na kocha wa zamani wa yanga? sasa posho za viongozi zinapatikanaje kama sio misiba na tafrija? acha wanaolinda viongozi wafaidike nchi isonge mbele
 
Yaani great thinkers mnaniangusha jamani, HAMJUI KUWA KUHUDHURIA MSIBA NAPO KUNA POSHO?

Hapo mwenye roho ya utu ni kikwete tu, yeye ndio anakwenda kwa hobby
 
Me sijawahi ona duniani serikali yote kwenye kila msiba ipo,si duniani tu hata hapa kwetu kwa awamu zilizotangulia sijawahi kitu kama hiyo,nafikiri salamu za rambi rambi zingekua zinajitosheleza sana!style hii itawafanya wananchi waamini kua kodi zao zinatumika isivyopasa,na hata kuamini kua serikali haiko busy na mambo ya msingi!
 
Ninyi mnalalamika kwa kuwa aliyekufa ni mbunge wa CCM.Angekufa wa CDM msingelalamika.Mbona kwa Regia hamkulalamika?

Hapa haijatajwa msiba ni misiba,na si kua serikali ndio mara ya kwanza kuudhuria misiba hovyo hovyo!tumia akili kidogo tu kufikiri
 
Hizi ni mbinu za kisiasa kuelekea uchaguzi. Viongozi wanatafuta majukwaa ya kuwasahaulisha watanganyika shida zao, na maovu yao yasahaulike! Wanajaribu kutuonyesha wapo karibu na misiba, wakati mahospitalini wagonjwa wanalazwa sakafuni!!
 
Jk anawatembelea wananchi kiujanja wakiwa na uzuni, make mda huo hawawezi kumpopoa
 
Jibu rahisi, lack of priorities!!!! JK hana priorities. Inaweza kueleweka kwa bi Kiroboto kwani ni mtumishi aliye chini yake, Waziri Mkuu kwa sababu alikuwa Naibu Waziri, lakini utakuta JK ananusa kila msiba!!! Hii inaonyesha ni kiasi gani mezani mwake hakuna mambo ya maana ya kufanya zaidi ya misiba na safari za nje (Ni rais pekee ambaye ameteua Waziri wa Mambo ya nchi za nje, lakini yeye ndiye anayefanya wizara ya mambo ya nchi za nje...Membe Jobless!!!!
Huyo ndiye mnayemtegemea ashughulike mambo yenu ya uchumi wakati mwenyewe alishashindwa. Nasikia keshakwea pipa kwenda Davos maana madaktari na Blandina wanaleta longolongo. Mkuu akionaga mambo mazito hukwea pipa upesi na kuondoka ili apigiwe simu.

Hatua nyingine wanataka kuchukulia misiba kisiasa. Wanataka wananchi waamini kuwa wako karibu nao hata katika nyakati ngumu wakati wakifumbia nyakati ngumu macho (mfano wa nyakati ngumu ambazo ningewaheshimu viongozi wetu iwapo wangeshughulikia ni uchumi, inflation, miundo mbinu, hali ya umaskini, na mambo kama hayo). Wajinga ndiyo waliwao!

Nawasilisha.
 
Hii haijakaa vizuri, ukizingatia utabiri wa mrithi wa marehemu mnajimu mkuu wa afrika mashariki nakati (SHEIKH YAHYA HUSSEIN), nanukuu " MWAKAHUU UTATAWALIWA NA VIFO VYA WANBUNGE PAMOJA NA WAKUU MBALIMBALI SERIKALINI". Sasa ninachotaka kusema ni kwamba, misafara ya hao viongozi (nimeona hapa arusha) inaligharimu sana taifa katika wakati huu wa ukata, wakati ambao hazina inatumika kama transit ya fedha toka TRA. wakati ambao serikali inakopa kwa ajili ya mishahara ya watumishi wake, wakati ambao mfumuko wa bei umekuwa mkubwa sana, ni wakati ambao wananchi wa kipato cha chini wamepunguza idadi ya milo kwa watu wazima, wakati ambao kwa bahati mbaya baadhi ya ndugu zetu wamekumbwa na maafa na serikali hiyo hiyo imewapeleka porini ambako wao hawawezi kuishi huko hata kwa mtutu wa bunduki. Ninaiomba serikali hii iachane na misafara ghali kiasi hicho na ifikirie kutumia wawakilishi wake walioko maeneo husika japo kwa kipindi hiki kigumu.
 
Nimegundua Ushabiki Na Mapenzi yanapunguza uwezo wa kufikiria sahihi,
inasikitisha Great Thinker akili yake imetawaliwa na siasa za ushabik,Uwezo wao wa kuchambua na kuchangia mada umepongua.
kwa hali hii tutapata viongozi wenye kufuata mkumbo wa chama zinazopofusha uwezo wa kufikiri katika kuleta maendeleo binafsi na kwa taifa letu kwa ujumla,
Hayo tumeyaona bungeni na hapa kwenye Jf wengi wetu tumekatwa na ushabiki.
great thinker toroka huko coz tuanjua uwezo wa kujadili saiasa na maendeleo ya taifa upo pasipo kuhusisha ushabiki,
CCM,CHEDEMA,CUF,NCCR etc vikikosea tuseme ukweli.

nawakilisha
 
tena walisema ooh tuachieni msiba wetu

ndio maana huwa nasema humuJF wana CDM wengi ni vuvuzera tu hawanamadhara saana,kwani wao kila jambo ni kulalamika,kutukana,kuponda,mbili hawakai na hata moja hawasimami hawana msimamo,
kila jambo wao wamekuwa wakulalama tu,sasa hapo ndipo huwa nawatofautisha sana na wenzao wa CCM kwenye nzuri wata sema na kwenye baya watasema

jamani tukubari tu kuwa kunakipindi hata ukikubari udhaifu wako ufii

Nimependa na hii. kuna watu wanabagua na kuona misiba fulani ndiyo okay na mingine inafuja pesa. Mungu tunusuru na siasa uchwara za Tz na jf.
Sasa mmejua kwa nini threads za mapenzi ndizo ziko juu humu JF. kwa akili hizi unatarajia nini?
 
Hapo mwenye roho ya utu ni kikwete tu, yeye ndio anakwenda kwa hobby[/QUOTE]
JF pana mambo, kuhudhuria misiba ni HOBBY, JK ana shughuli na nch hii,mwanitekenya kwa kweli
 
Back
Top Bottom