Hivi hii ya serikali nzima kuhamia kwenye mazishi imekaaje?

unategemea kikwete anaweza kukanyaga Arusha au Kilombero hivihivi tu bila kwenda na gari ya msiba? Ndio wanakotokea na wao waonekane wamekwenda mikoani kuonana na wananchi.
 
Ninaamini kabisa kuwa kama wasingeenda, basi kungekluwa na malalamiko kuwa viongozi wa serikali wakacha mazishi ya mbunge
Hata na mimi nilikuwa ninafikiri hivyo hivyo. Tumeona hivi karibuni JK alipochelewa tu kufika kwenye mazishi ya Mpendwa wetu Regia (Mungu Amrehemu), wapo walioanza kusema. Vilevile kutoonekana kwa viongozi wa CUF katika mazishi yale, watu walianza kusema na kuhusisha kutokuwepo kwao na uhasama uliopo baina ya CDM na CUF.

Lakini pia, pamoja na viongozi kutekeleza wajibu wao kama wanajamii, vilevile wanahudhuria mazishi ya viongozi na watu maarufu kama "mtaji wa kisiasa"; waonekane, watajwe, waeleweke kama "wanawajali" raia yao. Kwa nini hatuwaoni wakihudhuria mazishi ya wanaofikwa na majanga? Kwa nini wahudhurie mazishi ya viongozi na watu maarufu tu?
"Waacheni Wafu wazike Wafu wenzao" [Source: Abdallah Hassan#4]
 
Ninyi mnalalamika kwa kuwa aliyekufa ni mbunge wa CCM.Angekufa wa CDM msingelalamika.Mbona kwa Regia hamkulalamika?
 
Lack of Confidence, walianza kama plan ya makinda kumuonyesha JK kwamba yeye ana strategy ya kuwabana Chadema, katika msiba wa Regia kwa kuwa walijua kwamba watu wengi sana watajitokeza kumzika Regia. Wakataka ku dilute issue ionekane watu wallijaa kwa sababu ya msiba wa mbunge kwa hiyo bunge na serikali ndio ionekane imefanya mambo. Hawakujua kwamba mungu hajaribiwi ndio maana akamuondoka Sumari immediately, sasa manunga ya embe na magamba wakabaki hawana jinsi bali kuonekana kwamba huo ndio utaratibu mpya wa mazishi ya kiserikali. Ndio maana hata baada ya kukosa watu kanisani na Karimjee walitumia mtindo wao wa kubeba watu waonekane wamejaa jambo ambalo walishindwa maana tunajua haikuchukua zaidi ya dk 45 kumaliza kuaga. Kwa Regia watu walitaka hata kumkata pua Yakubu aliyejifanya kuwa na haraka ya kuondoa msiba wakati huo huo akitangaza kwamba watu wawapishe wabunge waage. Magamba wakaendelea kubuku ndege zote jana kwa staili ya kubeba waombolezaji ticketi za bure zikiwa kila mahali, ndio maana watoto wa mjini wanasema serikali hii sasa imekua ya misiba, Raisi wetu JK Raisi wa Misiba, acheni nao waandike kitabu chao, maana najiouliza kama mwenyekiti wa chama alishakwenda, Msekwa nae allfuata nini? Kama Anna Makinda alishakuwepo, Ndugai alifuata nini? kama ni ushiriki binafsi sawa, lakini ukishatangaza kuwa ushiriki wa kiserikali hapo napo kuna jambo. Halafu sikumuelewa bibi kiroboto kutumia wakati huo kueleza habari ya kufiwa na wafanyakazi wa ofisi ya bunge, alitaka kuashiria kuna bundi ama kidudu mtu, ama kumtaka mungu ahamie kwenye taasisi nyingine? Hapa ndio matumizi ya siasa misibani yanapowarudia magamba, mwenzao mbowe pale Karimjee alikua relevant, kwamba msimpambe mpambanaji leo, vingaavyo vimeundwa waacheni wanafunzi wa vyuo wafanye siasa ilimradi hawavunji sheria.

Mfumo wa vyama vyangi vya siasa ni balaa tupu kwa nchi zetu za kiafriika. Kila kitu ni kufanya kwa ushindani tu hata misiba jamani e mola tuepushe na hili balaa la vyama vingi
 
Sawa kabisa ulichokisema na ndo ukweli wa mambo.... ushiriki wao kwa mazishi ya Regia kulikuwa ni mbinu zao chafu za kisiasa..
 
kwa kweli hata mimi imenisikitisha sana kuona viongozi karibu wote wa nchi wanaenda kwenye msiba mmoja. ivi kwa nini wasipange utaratibu wa uwakilishi. kwa mfani Kikwete akienda ina tosha, sio lazima na waziri mkuu awepo jamani. yaani this is so ridiculous.
 
Lack of Confidence, walianza kama plan ya makinda kumuonyesha JK kwamba yeye ana strategy ya kuwabana Chadema, katika msiba wa Regia kwa kuwa walijua kwamba watu wengi sana watajitokeza kumzika Regia. Wakataka ku dilute issue ionekane watu wallijaa kwa sababu ya msiba wa mbunge kwa hiyo bunge na serikali ndio ionekane imefanya mambo. Hawakujua kwamba mungu hajaribiwi ndio maana akamuondoka Sumari immediately, sasa manunga ya embe na magamba wakabaki hawana jinsi bali kuonekana kwamba huo ndio utaratibu mpya wa mazishi ya kiserikali. Ndio maana hata baada ya kukosa watu kanisani na Karimjee walitumia mtindo wao wa kubeba watu waonekane wamejaa jambo ambalo walishindwa maana tunajua haikuchukua zaidi ya dk 45 kumaliza kuaga. Kwa Regia watu walitaka hata kumkata pua Yakubu aliyejifanya kuwa na haraka ya kuondoa msiba wakati huo huo akitangaza kwamba watu wawapishe wabunge waage. Magamba wakaendelea kubuku ndege zote jana kwa staili ya kubeba waombolezaji ticketi za bure zikiwa kila mahali, ndio maana watoto wa mjini wanasema serikali hii sasa imekua ya misiba, Raisi wetu JK Raisi wa Misiba, acheni nao waandike kitabu chao, maana najiouliza kama mwenyekiti wa chama alishakwenda, Msekwa nae allfuata nini? Kama Anna Makinda alishakuwepo, Ndugai alifuata nini? kama ni ushiriki binafsi sawa, lakini ukishatangaza kuwa ushiriki wa kiserikali hapo napo kuna jambo. Halafu sikumuelewa bibi kiroboto kutumia wakati huo kueleza habari ya kufiwa na wafanyakazi wa ofisi ya bunge, alitaka kuashiria kuna bundi ama kidudu mtu, ama kumtaka mungu ahamie kwenye taasisi nyingine? Hapa ndio matumizi ya siasa misibani yanapowarudia magamba, mwenzao mbowe pale Karimjee alikua relevant, kwamba msimpambe mpambanaji leo, vingaavyo vimeundwa waacheni wanafunzi wa vyuo wafanye siasa ilimradi hawavunji sheria.
we ni mjinga wa kwanza,toa siasa zako za mataji taka na ushabiki wa kijinga ata km ni wacdm,ruhusu akili yako kufikiri,ndyo maana utakufa masikini kwa kushabikia wafanyabishara(mbowe).kweli wamekosea lakini toa haja hoja usitukane watu
 
Msiba si jambo jepesi, lakini kwa huku tulikofika acha tu nithubutu kusema ni upumbavu.
 
Ninyi mnalalamika kwa kuwa aliyekufa ni mbunge wa CCM.Angekufa wa CDM msingelalamika.Mbona kwa Regia hamkulalamika?
  1. Kwa JK, he is naturally “mtu wa watu na mwenye huruma” - a typical culture ya waafrika wengi, na ni nzuri!! Tatizo langu ni mara nyingi kushindwa kwake ku –prioritize! Mana hata kama una huruma , kama rais kuna mamna nyingi yaku –express hiyo huruma yako, na watu watajua tuu!
Kama alishakwenda nyumbani kwake Mbezi mie naona inatosha, na kwa kuwa Pinda alikuwa ziarani Arusha nadhani ingetosha! Na ndo mana hatukusema alipojitokeza Moro kwa mara ya pili – mana pia alikuwa ziarani Moro!
  1. Lakini pia, hivi vitendo vyao vina refelect sisi wananchi tulivyo kwa ujumla wetu!! Na ninaaamini wakati mwingine huwa wana-act kutokana na feedback za vyombo vyao! Najua kama JK asingeenda Arumeru watu kibao wangesema kuliko hawa tunaosema sasa!! Na JK huwa hafanyagi kosa katika anga hizo – mana ungesikia – “JK hana dili na Arusha! Mbona Moro alienda” ,mara “JK ana bifu na Lowasa hadi keshawatosa Wamasai na Wameru” – si unajua Lowasa yuko related na Marehemu!!!, na mengine mengi ambayo yengewa affect kampeni za chaguzi ndogo huko Arusha!!
  2. Funzo kwa voingozi wetu kama wanaosoma JF, au sisi kama tutakuwa viongozi kesho!!
Lets concentrate in doing the right thing - hata kama majority hawatuelewi – facts don’t lie, wapo watakao elewa.Mmwaka una miezi 12, na sasa mwezi mmoja umeondoka, Je serikali imesha achieve nini?? Kwa nini huu muda usingetumika hata ku solve mgogoro wa madaktari na msongamano wa wagonjwa Muhimbili for good???

Mfano! Kuna mambo mengi Mwalimu alifanya watu waka koroma kwa miaka na miaka, lakini akawa shupavu akafanya na sasa ni nguzo na hata hao woote waliofuata wameshindwa mpita, pamoja na kufuata the “right economic model” – Ubepari!!!!
 
kiongozi lazima ashiriki masuala ya kijamii na hasa matatizo ya watu wake,kwani we ulitaka kusemaje.

Mie naona si sahihi kusema lazima ashiriki kwani rais ni wa Watanzania wote lakini hawezi kushiriki kila msiba. Huwa kuna kuwakilishana! Spika na naibu wake,rais na makamu wake inakuwaje?
 
acheni wende huko wananchi nao wawaone maana tangu wachaguliwe hawajawahi ruka maeneo hayo, zaidi wanaenda kupumzika n kupiima joto la kisiasa, utendaji wao hauna muongozo siyo ajabu mkuu wa kaya hakujua kuwa prime ninister atkuwa huko tena wanamshukuru Mungu kwa kuwa waandishi vilaza watawapongeza nakuwaandika magazetini kwa herufi kubwa na mbwe,mbwe nyingi sana kuwa serikali hii inajali watu wake!

ni fedheha kumjali marehmu mmmoja kwa gharama yakuhudumia waliohai milioni mja na zaidi kwa kuwa garama za ulinzi, usafiri etc kwa viongozi wetu wanapokuwa nje ya sehemu za ofisi zao ni kubwa mmno!

walio vilaza wataendelea kuwapongeza!
 
Ni jamii iliyopoteza mwelekeo hii....Maana tatizo ni kubwa zaidi kuliko hata mnavyoliona. Watanzaia tumepoteza mwelekeo kama taifa, au kama jamii. Akili zetu zinazidi kuzorota kila kukicha, kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu imekuwa kitu cha kawaida. Badala ya kuangalia jinsi ya kuboresha huduma za afya ili kupunguza gharama kubwa za kutibu wagonjwa India, tunahudhuria misiba, wakati madaktari wamegoma na wagonjwa wanazidi kufa mahosipitalini.

Kwa kifupi, tunatakiwa tujitazame upya kama Watanzania, kama jamii iliyopoteza dira na mwelekeo. Tusiishie kulalamika tu, na kuwanyooshea vidole viongozi wetu.
 
Kama kuna ukweli fulani hivi, maanake hata kama ni msba, lakini hizo gharama!!! KUna kipindi kulikuwa na tabia ya Seikali kuwakilishwa na Kiongozi wa ngazi ya juu mmoja, sijui imeishia wapi.
 
Ninyi mnalalamika kwa kuwa aliyekufa ni mbunge wa CCM.Angekufa wa CDM msingelalamika.Mbona kwa Regia hamkulalamika?

tena walisema ooh tuachieni msiba wetu

ndio maana huwa nasema humuJF wana CDM wengi ni vuvuzera tu hawanamadhara saana,kwani wao kila jambo ni kulalamika,kutukana,kuponda,mbili hawakai na hata moja hawasimami hawana msimamo,
kila jambo wao wamekuwa wakulalama tu,sasa hapo ndipo huwa nawatofautisha sana na wenzao wa CCM kwenye nzuri wata sema na kwenye baya watasema

jamani tukubari tu kuwa kunakipindi hata ukikubari udhaifu wako ufii
 
Ndiyo hapo CDM wanapowazidi akili. Mmezoea sana kuiga. Hamuwezi kuja na jipya kazi kusubiri CDM wamesema nini au wamefanya nini na nyinyi mfanye.

Sasa wenzenu wamewapiga bao. Wamepeleka wawakilizi Zitto na Lema, nyinyi bado mnapeleka Serikali yote.
 
Viongozi wetu wengine wanakwenda misibani ktk motive ya kisiasa zaidi. 2015 siyo mbali; baadhi ya wapiga kura hasa wa vijijini wako radhi kumpigia kura mtu anayeshiriki sana mambo ya kijamii kama harusi, misiba n.k. hata kama hafanyi chochote lolote la maendeleo. Hii ndio Tanzania bana!
 
Back
Top Bottom