Hivi hii shahada yangu kuiweka kwenye chips ni halali kweli?

wewe unazungumzia chips??? me nimeamua degree yangu niipeleke kwenye kuuza kahawa baada ya kuona ajira ngumu,,, cha muhimu aanzia pale ulipo kufika unapohitaji
 
Karibuni Wana zuoni, wachambuzi, Wanafalsafa, Wana saikolojia mniweke Sawa hapa nataka kuanza Choma chips baada ya kuona milango ya ajira migumu lakini nahisi najipeleka kwenye kada isiyo yangu na kutoitendea Haki my hanorable bachelor. Nawasilisha
Je ukikosa msosi kwa kutofanya kazi ya kuchoma chips unaweza kula hiyo degree?

Nilitegemea hiyo elimu/degree ndio ikushawishi kuingia kwenye biashara ya kukuingizia kipato, kumbe ndio inakufanya ukimbie kazi

Bado swali la msingi, ni je hiyo bachelor ulienda kusoma kwa sababu gani?
 
Ni kweli mkuu lakini akili yangu ilishaathiriwa na mfumo wa elimu yetu Tanzania
Usisingizie mfumo wa elimu yetu Tanzania kwani katika wa Tanzania wote waliosoma kwenye huo mfumo wameajiriwa? Unazo takwimu ni idadi kiasi gani cha wahitimu kuanzia a level mpaka bachelor degree wanahitimu kwa mwaka na kiasi gani kati yao wanaingia kwenye formal employment?

Me naona tatizo lako ni either wewe ndio pekee umefika University kwenye family au ukoo wenu au kijiji chenu chote na mmekua na mindset kwamba ukifika level hiyo ya education ni lazima upate white color jobs

Maisha yanabadilika kuna nchi nyingine kuwa na bachelor degree ni kama kuwa na primary education qualification tena sio mbali sana ni Nigeria tu Africa hiii hiii

Tanzania tunaona University education ni bab kubwa sababu elimu imefika jioni machweo kuna nchi elimu ilishawahi siku nyingi kwa hiyo mambo ya degree walishayazoea wakati Tanzania wenye degrees unaweza kuwahesabu kwa number.
 
KISOMO AMBACHO KINAMFANYA MTU AONE TABU KURUDI KIJIJINI SI KISOMO BALI NI MAPAMBO.KUPATA SHAHADA NI MATOKEO TU NA SI MSINGI WA ELIMU YA CHUO KIKUU."IBRAHIM KADUMA JULY 4 1977
 
Lengo lako la kusoma ni ili baada ya kuhitimu uajiriwe au ujiajiri ili utafute pesa...

Kama kuajiriwa kumeshindikana, jiajiri, kama chips ndiyo fursa ilipo fanaya...


Cc: mahondaw
 
Nini kuchoma chips,nimetembeza mitumba katikati ya jiji la dodoma baada ya kuhitimu+Kupokonywa mtaji na manispaa+Kurudi kumuuzia mtu wa la saba nguo,pale nyerere square ananilipa day waka,

Kijana una deka Sana wewe.
Bado upo Dom? Nyerere square?
 
Dah...nafarijika kuona kumbe kuna degree holders wenzangu kama mimi tunaofanya vijishughuli kama hivyo, maana kuna wakati najiuliza nilimkosea wapi Mungu. Mimi na vyeti vyangu vizuri tu lakini shughuli ninayofanya naona hata aibu kuisema hapa, ni nafuu hata yako unayetaka kuuza chipsi
 
What is bachelor degree by way? Have you tried to figure out the realism of what you have studed with life realities? Why being a slave minded like that! Your mind here is your problem!! First positive then other decisions will smoothly flow. Shida vijana tunafika mpaka vyuoni alafu hatutambui kuwa njama zimebadilika na Educational aims za kipindi hicho kutengeneza managerial works tunaruhusu zituendeshe mpaka LEO HII? That's why we are failing even to PLAN
Karibuni Wana zuoni, wachambuzi, Wanafalsafa, Wana saikolojia mniweke Sawa hapa nataka kuanza Choma chips baada ya kuona milango ya ajira migumu lakini nahisi najipeleka kwenye kada isiyo yangu na kutoitendea Haki my hanorable bachelor. Nawasilisha
 
Back
Top Bottom