Hivi hii ni sahihi kweli? nini kazi ya bwana harusi?

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865
Habari zenu wanandugu!!!

Nimekuwa mshenga nasimamia harusi ya ndugu yangu. Jana tulikuwa tunawaza zawadi ya bibi harusi tukataja mambo mengi sana. Kisha nikawaza..
1. kuna haja kweli ya familia ya bibi harusi kumnunulia kila kitu binti yao wakati anaenda kuolewa? yaani kitanda, kabati, vyombo, mashuka hadi nguo za ndani night dress etc

2. Sasa kazi ya bwana harusi ni nini? yaani unampa binti yako na sehemu ya kumkazia pia?

3. Hatuoni ya kwamba ile hali ya maharusi kuanza kwa pamoja wanajichanga kidogokidogo wanafanikisha kitanda kabati tv mpaka wanakuwa wakubwa hujenga bond nzuri katika mahusiano?

4. Hatuoni ya kwamba kumpatia kila kitu ni sawa na kumuambia kaa ukiwa tayari kusepa kwenda kupanga?

5. Kwa wanaume ambao mmeoa mkakuta kila kitu uanaume wenu unakaa wapi? au mnajisikia hali gani?

karibuni wadau
 
Hivi wewe ukichangiwa utakataa?

Duniani kote kijana anapooa au anaagwa "sendoff" huwa anapata kazawadi angalau aende nako huko anakokwenda ndio Upendo tunaounyesha kwao.

Sioni kama ni tatizo eti uanaume wako utaisha kwasababu umepewa kila kitu cha kuanzia maisha.

Hebu tuache tabia za kimaskini.
 
Umaskini unatesa watu wengi sana kisaikolojia.

Ulitaka apewe peremende au toy.
Niliona harusi ya mtoto wa mkimbiza upepo maarufu tz enzi hizo(Bayi)
Mwanae alipewa Kila kitu.
Nyumba ina asset zote za ndani.

Mwanao umnyime zawadi kisa atatafuta na mmewe?
Mzazi wa namna hyo atakuwa na matatzo ya akili.
 
maisha ya ndoa...ni ukurasa mpya kwa kila mmoja na huwezi kukaririsha na kuishi ukurasa wa mwenzio

..kikubwa ukiona mwenzio anafoka we fungua fridge pata glass moja ya maji baridi kisha "WEKA MAJI MDOMONI" manake usipofanya ivo gunia la mkaa lakuhusu
 
Hivi wewe ukichangiwa utakataa?

Duniani kote kijana anapooa au anaagwa "sendoff" huwa anapata kazawadi angalau aende nako huko anakokwenda ndio Upendo tunaounyesha kwao.

Sioni kama ni tatizo eti uanaume wako utaisha kwasababu umepewa kila kitu cha kuanzia maisha.

Hebu tuache tabia za kimaskini.
Mimi nilimuambia bibi harusi mapema kwamba nyumba yangu imejaa vitu so hakuna pakuviweka vyake. akaviacha kwao. This is my home and she is my wife. I am obligated to shelter, feed, bed and dress as well as to protect her....
Kwanini wazazi wahisi mimi sina kitanda? sina godoro?
 
maisha ya ndoa...ni ukurasa mpya kwa kila mmoja na huwezi kukaririsha na kuishi ukurasa wa mwenzio

..kikubwa ukiona mwenzio anafoka we fungua fridge pata glass moja ya maji baridi kisha "WEKA MAJI MDOMONI" manake usipofanya ivo gunia la mkaa lakuhusu

Hahahahaa! Au imba tu moyoni
 
Mimi nilimuambia bibi harusi mapema kwamba nyumba yangu imejaa vitu so hakuna pakuviweka vyake. akaviacha kwao. This is my home and she is my wife. I am obligated to shelter, feed, bed and dress as well as to protect her....
Kwanini wazazi wahisi mimi sina kitanda? sina godoro?

Na umtunze kweli sio blah blah ukiombwa laki unatoa mijicho!
 
1. kuna haja kweli ya familia ya bibi harusi kumnunulia kila kitu binti yao wakati anaenda kuolewa? yaani kitanda, kabati, vyombo, mashuka hadi nguo za ndani night dress etc

Haina haja ila wakipenda wanunue tu bila kushinikizwa/kulazimishwa.

Mimi mke wangu alijiandaa na vitu vichache tu kama vyombo vya muhimu ingawa na mimi nilikuwa nishajiandaa.

Kuhusu nguo, zile za zamani alizigawa zote kwa wadogo zake zikabaki alizonunua mpya na zile alizozawadiwa.

Nguo za siku ya harusi, niliandaa mwenyewe(nilitoa hela, kamati ya mapambo ikawajibika), siku ya ndoa tulimvisha nguo zetu nilizogharamia mimi na kumchukua.

Mengine kama kabati, viti anaweza kupewa kama zawadi kwa mapenzi yao ila sio lazima.
 
Kama wanauwezo wa kufanya hivyo hakuna tatizo hiyo ni zawadi kwa bint yao.
Kwenye suala la vyombo wazazi wa bint wanawajibika kufanya ivyo ni lazima kumnunulia bint yao vyombo vya kupikia na mashuka
 
asilimia kubwa wanachangisha watu kwenye send-off.
 
Habari zenu wanandugu!!!

Nimekuwa mshenga nasimamia harusi ya ndugu yangu. Jana tulikuwa tunawaza zawadi ya bibi harusi tukataja mambo mengi sana. Kisha nikawaza..
1. kuna haja kweli ya familia ya bibi harusi kumnunulia kila kitu binti yao wakati anaenda kuolewa? yaani kitanda, kabati, vyombo, mashuka hadi nguo za ndani night dress etc

2. Sasa kazi ya bwana harusi ni nini? yaani unampa binti yako na sehemu ya kumkazia pia?

3. Hatuoni ya kwamba ile hali ya maharusi kuanza kwa pamoja wanajichanga kidogokidogo wanafanikisha kitanda kabati tv mpaka wanakuwa wakubwa hujenga bond nzuri katika mahusiano?

4. Hatuoni ya kwamba kumpatia kila kitu ni sawa na kumuambia kaa ukiwa tayari kusepa kwenda kupanga?

5. Kwa wanaume ambao mmeoa mkakuta kila kitu uanaume wenu unakaa wapi? au mnajisikia hali gani?

karibuni wadau
Wewe ulivyoolewa hukupewa vyote hivyo?Kama ndiyo kwanini hutaki mwenzio apewe?
 
Hapo Namba 5
Hujui kweli uanaume wetu uko wapi ??
 
Back
Top Bottom