Hivi hii ni kweli kwamba mwanamke akiamua kuua harudi nyuma

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Kuna mada nimekutana nayo kijiweni jioni hii baada ya kutoka kazini ikanivutia sana
Hoja Kali ziliibuka wengine wakawatetea na wengine wakapigilia msumari
Mmoja alinistaajabisha sana na kuniogopesha mno katika harakati zangu hizi za kutafuta mwanamke anifaae ili kujenga maisha kwa pamoja pale aliposema kuliko kukutana na mwanamke mwenye hasira
Ni bora kukutana na simba chatu mamba unaweza kuokoa maisha yako lakini si kwa mwanamke mwenye hasira
Wadau kuna ukweli hapa au ni porojo tu

Kwamba mwanamke ni hatari kiasi hiki??!!
 
Mwanamke ni kiumbe wa ajabu sana! ukimchunguza hutammaliza ndugu yangu
Hakuna kiumbe dhaifu kama mwanamke
Hakuna kiumbe chenye mapenzi kama mwanamke
Hakuna kiumbe hatari duniani kama mwanamke
 
Sio kweli ndugu yangu kua mwanamke ni hatari hivyo na ndio maana wewe umewepo kakuzaa huyo huyo mwanamke la msingi mtafute mueleze usichokipenda nae hakueleze asichokipenda kisha maisha yanasonga mbele mpendane kweli na mungu atawatangulia mfikie malengo yenu
 
So hakitabiriki si ndio manaake?
 
Sio kweli ndugu yangu kua mwanamke ni hatari hivyo na ndio maana wewe umewepo kakuzaa huyo huyo mwanamke la msingi mtafute mueleze usichokipenda nae hakueleze asichokipenda kisha maisha yanasonga mbele mpendane kweli na mungu atawatangulia mfikie malengo yenu

Hivi ni kwanini mungu alituasa tuishi nao kwa makini?
 
mmmmh mbona hao wenye hasira ndio wanaupendo wa kweli hawa wengine maigizo mengi
 
Simba au mamba unaweza panda juu ya mti ukaokoka,mwanamke anakusubiri ulale ili akufinye maeneo yanayoleta maumivu makali.
 
Swali gani hili ndugu? Kwani we ulizaliwa na mwanaume? Muangalie tu mamiyo kwani alishajaribu kumuua babiyo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom