Hivi hii nauli ya daladala ya Tsh 200 kwa Mwanafunzi ni kwa siku za week Pekee au napia siku za weekend?

SEMARK2020

Senior Member
Feb 7, 2015
171
123
Juma pili ya leo nimepanda Daladala T784 DJQ kwa usajili number S108078G kwa Safari ya Makumbusho to G/mboto (kwa mujibu wa tickets). Safari yangu ikianzia Mwenge kwenda G/mboto .

Muda mchache kupita nikiwa ndani ya daladala Yakaanza mabishano Kati ya Konda na mzazi alie tokea Kanisani akiambatana na watoto wake wawili ambapo kwa kuwatazama age yao ni kati ya 12-15
MABISHANO:

KONDA :
(Kwa Ukali)
Hata kama ni wanafunz kwakuwa leo ni weekend wanapaswa kulipa Tsh 600 (nauli ya mtu mzima)

MZAZI:
(Akizungumza kwa sauti ya juu huku akizungusha kichwa kana kwamba akisubir support toka kwa sisi abiria wengine)

Huyu Konda anaakili kweli!!!?
Kwaiyo leo kama ni weekend ukimbaka mwanangu pale mahakamani mbele ya hakimu utajitetea hakuwa mwanafunz kwakuwa ilikuwa weekend?

SISI ABIRIA:
( vicheko!!!!!!

HITIMISHO:
Hapa mwanafunz yu pamoja na mzazi
Najaribu kuwaza ingekuwaje iwapo hawa watoto wangekuwa peke yao ndani ya daladala hii ??

Natamani namimi kujifunza hapa Kwani Kisheria imekaaje hii kwa Upande wa hizi daladala ?

Naomba kuwasilisha
 
Mlangon kwa pale kwenye gari pameandikwa nauli tsh 400 na 200 kwa wanafunz siku za wikend Yale maandishi yapo hayafutwi hvyo naul ya mwanafunz n tsh 200 haijalish siku za wiki au za wikendi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo ni latra Sasa hivi daladala wamekuwa huru kujipangia nauli Kama hamna mamlaka husika halafu unakuta abiria wanawaunga mkono huwa nikishuhudia najiuliza ndio Hawa watanzania wanaodai katiba mpya kweli
 
Back
Top Bottom