Hivi hii mifumo inaanzishwa kisiasa au hatuna direction?

Mapambano Yetu

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
1,124
2,092
"
NACTE



10TH MAY 2017 19:26:49

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Date Posted: 10th May 2017 19:26:49 Posted By:NACTE



BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)





TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UDAHILI WA WANAFUNZI WA ASTASHAHADA NA STASHADA KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini. Sheria hii inazitaka Taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kusajiliwa kabla ya kuanza kuendesha mafunzo yoyote. Baraza pia huidhinisha mitaala kabla haijaanza kutumika. Hivyo taasisi zote haziruhusiwi kuanza kutoa mafunzo yoyote bila kibali maalumu kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).



Baraza linapenda kuwataarifu wadau wa sekta ya Mafunzo ya Ufundi na Umma kwa ujumla kuwa udahili na uchaguzi wa wanafunzi kwa ajili ya masomo ya Astashahada na Stashahada mbalimbali yanayotolewa na vyuo vyote hapa nchini,utafanyika moja kwa moja vyuoni, isipokuwa kozi za afya na ualimu zinazotolewa na vyuo vya Serikali tu. Hivyo maombi yote ya nafasi za masomo yatumwe kwenye chuo husika.



Udahili wa kozi za Afya na Ualimu katika vyuo vya Serikali utaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia kwa kushirikiana na Baraza (NACTE). Hivyo maombi ya Udahili kwa kozi za Afya na Ualimu kwa vyuo vya serikali tu yatumwe kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz) au kupitia vyuo husika vya Afya na Ualimu ambavyo vitashughulikia maombi hayo na kufanya udahili kwa njia ya mtandao kupitia ‘Institutional Panel’ zao.



Aidha vyuo vyote vitatangaza au kuwafahamisha moja kwa moja waombaji majina ya watakaochaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali; na wale wa kozi za Afya na Ualimu watatangazwa na Wizara husika na kupitia tovuti ya NACTE.



Baraza linapenda pia kuwafahamisha kuwa Vyuo vitaanza kupokea maombi ya udahili wa wanafunzi kuanzia tarehe 15 Mei, 2017 hadi tarehe 20 Agosti, 2017. Majina ya waliochaguliwa yatatangazwa tarehe 14 Septemba, 2017. Masomo kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 25 Septemba, 2017.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 10/05/2017

"

Hii ni movement from digital to analog. Kama gharama ya kuapply Chuo kimoja ni Tsh. 20000 basi kila mhusika aandae not less than 80000 kuapply angalau vyuo 4. Yaani ni mwendo wa kukurupuka kila idara.
 
Back
Top Bottom