tusipotoshane
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 730
- 693
Hehehe,umedadavua kweli!!!Kuna ujinga mwingi wanafundishwa kanisani.
Kwanza wanaambiwa asiolewe na mtu asiye na kazi ya kueleweka.
Wenye kazi za kueleweka ni wachache na wengi wameshaoa tayari.
Vijana wengi wanafanya shughuli za kubangaiza au umachinga.Hata hivyo wengi wa jinsi hii ndio wanaotoboa kimaisha.Kuna wafanya biashara wakubwa wametoka kwenye kundi hili ambalo linadharauliwa na wengi wakiwemo wasabato
Pili huwa wanajengwa kuamini kuwa ni lazima waolewe na msabato mwenzao.
Sasa tatizo linakuja tena kuwa kubwa pale wanapowekewa sharia na kibano hata cha kukutana wakiwa marafiki ama wachumba.Ikitokea wakawa wanakutana kanisa linaweza kuwafuta ushirika.
Kwa hiyo unakuta kutokana na mahitaji ya mwili,binti anakuwa na muhuni huko nje na anagongwa vilivyo na mvulana anakuwa na vibinti tofauti vya kujiliwaza kila anapopata mihemko ya kihisia.Wakikutana kanisani wote wanajidai wasafi na washika sheria.Mwisho wa siku binti anajikuta kazidiwa na kudungwa mimba.Hapo anakosa ujanja
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app