Hivi hii harufu ya baadhi ya mitaa ya jijini Dar naisikia peke yangu tu?

Karikoo mchikichini kule down Kuna nuka harufu za kashata, uvundo wa TBL na maji machafu

Still watu wanaishi na kupiga kazi Kama kawa

Ferry kunanuka samaki waliooza

Vingunguti Kuna nuka mavi ya mbuzi

Masaki,obey utapata harufu ya chumvi chumvi ya bahari
 
Karikoo mchikichini kule down Kuna nuka harufu za kashata, uvundo wa TBL na maji machafu

Still watu wanaishi na kupiga kazi Kama kawa...
Hata enzi zile alikuja mwanamuziki Michael Jackson alilalamika kwamba jiji linanuka, Alitukanwa sana kwamba anaringa, Limbukeni na kashfa nyingi tu tulimtupia, kumbe alikuwa sahihi, oh, we are very sorry for that !!
 
Ni kweli kabisa dar inanuka mno ni harufu ya kinyesi haswaaa. Wewe ni mtu wa 2 Sasa wa 1 alikuwa mfalme wa pop duniani. Mkuu dar siyo pa kukaa wamejaa omba2 wanajisaidia bara2ni mitaroni na kwenye maua! Yaani ni siwezi ishi apo kuna inzi wakubwa kama kumbi2! Dar ni majanga.
 
Ni kweli Dar ilikuwa hainuki hivi miaka michache iliyopita, nadhani baada ya ujenzi wa miundombinu, kuna vitu havijakaa sawa. Barabara ya kutoka Makumbusho hadi Mwenge hiyo harufu inasikika dhahiri, nahisi ni ule mtaro uliojengwa pembeni ya barabara hiyo
Ni kweli. Siku mbili zilizopita nilikuwa maeneo ya MWENGE . Kuna sehemu moja kwenye maduka ya pembezoni mwa bara
bara nilisimama kwa muda mrefu kidogo nikisubiri kuhudumiwa. Nilikuwa nasikia harufu ya mavi mavi.

Naangalia kwenye mtaro sioni mavi wala maji machafu Ila harufu ipo. Ile hali ilinishangaza sana. Mpaka nimeondoka baada ya kuhudumiwa niliacha hali Ile Ile ya harufu.
 
"...wapo wanayoipenda..."
"...siiongelei jambo hili..."
"...mji usiwe jiji la..."
"...kudhuru Zanzibar..."
Nk

Dah asante sana 'Taikuni la Fasihi'

Anyway hamia Olpopong' ndichi huko tuachie jiji letu
 
Wakuu kwema!

Aisee! Baada ya kutoka kuzurura huko Duniani, sitaki kupataja nisijeonekana najikosha hapa, na wenye nongwa zao na vijiba vya roho wasije nitolea mvuke wa ushubwada. Ila ifahamike tuu nimetoka huko Dunia ilipo.

Kwa kweli Dar inanuka vibaya mno. Inanuka vitu mfano wa mavi, sijasema ni mavi jamani Ila ni kama hivyo.

Yaani Asilimia kubwa ya Maeneo yananuka chemba za maji taka. Nashindwa Kueleza hapa. Sitaki kugombana na wenye Dar yao, sitaki kabisa. Maana najua wapo wanayoipenda, ikumbukwe siiongelei Jambo hili Kwa ni mbaya lakini naongea ili Jambo Fulani lifanyike.

Halafu ukiwaona wakazi wa Dar ni Kana kwamba hawaisikii hiyo harufu, pengine wamekuwa sehemu ya harufu yenyewe, sijasema watu wa DAR mnanuka chemba za maji taka 😃😃😃. Maana wenye hasira hamkosekani.

Hata hivyo akili yangu ikanambia sio rahisi watu WA DAR kuisikia hiyo harufu mbaya ya mavi Kwa maana maisha yao ni ya taabu sana. Taabu zimeua mishipa ya Nostril ndani ya pua. Hawezi kunususa tena.

Hasa watu masikini wapanda Daladala, hawa ndio wanaoonja joto ya jiwe, hata hivyo wenyewe ni Kama joto Hilo hawalisikii kwani taabu imewafubaza na kuwafanya waone kila kitu Kama kipo Sawa.

Kipindi nasoma pale UDSM wala sikuwa najua Dar inanuka, nimekaa zaidi ya miaka mitano kama sio sita sikuwa naona hizo harufu. Labda Maeneo ya Tandale huko na viunga vya makazi ya WALIA NA MUNGU watu fukara apeche Alolo.

Najiuliza niliwezaje kuishi miaka mitano kipindi kile?

Nafikiri serikali ipitie tena miundombinu ya taka hasa mitaro ya maji taka ili mji usiwe jiji la harufu mbaya.

Wananchi wa Dar nanyi mjitahidi kuwa wasafi hata kama mmezoea harufu yenu mbaya kumbukeni wageni kama Sisi tunaotoka Duniani tunakujaga pia kuwasalimu.

Muwe na Haya hata kidogo.

Taikon nitakuwa DAR Kwa wiki tatu mfululizo kabla sijaenda kudhuru Zanzibar nikielekea kuchumbia Visiwa vya Comoro.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dogo hizo harufu udsm zipo sana vyoo vya udsm nivichafu sana na chamber huwa zinaziba mno usitake kutudanganya
 
23 Reactions
Reply
Back
Top Bottom