Hivi haya ya maaskofu na mashehe ni umbumbumbu au mawazo finyu?

Expedito Mduda

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
522
239
Tusipoangalia vizuri na kwa jicho la pekee na kama watu wenye akili zuri na upendo na nchi hii hawatajitokeza na kuweka mambo sawa, nadiriki kusema nchi hii si muda mrefu itaingia kwenye matatizo!! Tazama muegemeo unaoonekana mashehe wanapotoa matamko. Pia angalia maaskofu wanapotoa matamko! Eti maaskofu wanakemea uozo uliotokea na kusababisha vifo vya wenzetu, kikundi kingine kinasema wanaingiza udini! Je, mimi mpagani nikisema nimeingiza upagani?
Mashehe wanasema maaskofu hawakufanya vizuri kutomtambua meya wa Arusha! Wanasema kuna mwelekeo wa udini kwa sababu eti maaskofu ni watu wa dini.
Sijui kama ni kwa kutofahamu au fikira kidogo mno mimi sielewi. Chitanda na Makamba nao wanakejeli maaskofu!
Mimi nawauliza, kwani mimi wanasiasa ni nani na maaskofu ni akina nani? Hivi hawa wote si Watanzania? Mimi naona tuache ushabiki wa kipumbavu na usokuwa na maslahi kwa taifa letu. Maaskofu na mashehe ni Watanzania ambao kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi wanaweza kutoa maoni yao na misimamo yao kama Watanzania wengine.
Kinachonipa shida kubwa ni kitu kimoja: Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa maaskofu wanakemea bila kuingiza kwamba eti ni udini fulani. Lakini watu wengine wanaona matamshi yao eti ni udini. Sasa kweli huu ni ufinyu wa mawazo na nafikiri kama hapa Tanzania kuna watu wenye busara basi watashughulikia suala hilo liishe. Hakna cha ushehe wala uaskofu, hapa wote ni Watanzania na tunatakiwa kukemea chochote ambacho tunaona kinaashiria upotevu wa amani ya nchi yetu.
Halfu nyie viongozi wenye dhamana, sisi wananchi tumewaweka hapo si kwa maslahi yenu na matumbo yenu na watoto wenu na ndugu zenu! Mpo hapo kwa ajili yetu sisi wote kama Watanzania. Hivi inakuwaje mlinde maslahi yenu kwa kulazimisha mpaka mnatuma polisi waue binadamu wenzenu. Mnataka kusema hayo madaraka mliyonayo ni muhimu kuliko uhai wa binadamu wenzenu? jamani nashindwa tu niseme nini lakini ukweli ni kwamba mimi binafsi nimeshangazwa sana kuona hamjali kabisa na mnaona waliokufa kama sisimizi hivi!
Hivi inakuwaje mtu anasema eti tatizo lililotokea Arusha ni la kisiasa baada kuona watu wamekufa? Kwa nini hilo halikushughulikiwa mapema kabla haya mambo ya ajabu nchini kwetu hayajatokea? Hebu nyie wote mliosababisha haya mambo achieni ngazi mlizonazo ili wale wanaowenza kuongoza na kuthamini jutu wa wenzao washike hayo madaraka.
ETI MAASKOFU WAVUE MAJOE WAENDE KWENYE SIASA!! HUU NI UPUMBAVU KABISA, MAITI ZA WATU ZIKO NDANI< WATU WANAHUZUNIKA< WAMEACHA WATOTO. WEWE KWA SABABU YA UROHO WA MADARAKA UNAENDELEA KUTETEA TUMBO LAKO! UKOME KABISA.
Halafu kitu kingine, hivi nyie mnaojiita wasomi wa chuo kikuu mko wapi? Hivi usomi wenu wote na akili zenu zote mmekaa kimya tu siasa Tanzania inaenda visivyo mpaka watu wanauawa. Nyie mnaendelea kukaa tu na hamsemi chochote? Hapana mimi naona nchini kwetu sasa kuna kitu fulani kinakosekana. HIVI MPO TAYARI KUONA MTU ANAKUFA KWA UPUMBAVU HUU KWELI? JAMANI MAISHA YA MTU KUPOTEA SI MCHEZO!! Acthari zake ni mbaya. TUREKEBISHE HAYA HARAKA SANA. Hapa tuhusike wote hakuna cha askofu, padri, mchungaji, shehe au rais, waziri, sijui chama gani. Wote tuje pamoja tuone shida iko wapi na mambo haya yakome kabisa kabisa.
Hivi nyie viongozi wetu tafadhari sana suala hili liwe mwisho! Uonevu huu uwe mwisho kabisa kabisa. Maisha ya mtu ni kitu kisichotakiwa kuchezewa hivyo!
Watu wanakufa na majambazi, mnasema polisi hawana vifaa vya kutosha! Vipi mngechukua hizo fedha za DOWANS mkawanunulia polisi vifaa vizuri kwa ajili ya kulinda amani watu wasiuawe na majambazi hamwoni mngekuwa mmefanya kitu chema zaidi kuliko kuwalipa DOWANS ambao mliwaleta nchini halafu tena mnasema hamuwajui hivyo mnawalipa kivuli. Jamani msituharibie nchi yetu.
TAFADHALI SANA TUWE SERIOUS NA NCHI YETU!!!
 
Back
Top Bottom