Hivi haya ya maaskofu na mashehe ni umbumbu au mawazo finyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi haya ya maaskofu na mashehe ni umbumbu au mawazo finyu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Expedito Mduda, Jan 10, 2011.

 1. Expedito Mduda

  Expedito Mduda JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Tusipoangalia vizuri na kwa jicho la pekee na kama watu wenye akili zuri na upendo na nchi hii hawatajitokeza na kuweka mambo sawa, nadiriki kusema nchi hii si muda mrefu itaingia kwenye matatizo!! Tazama muegemeo unaoonekana mashehe wanapotoa matamko. Pia angalia maaskofu wanapotoa matamko! Eti maaskofu wanakemea uozo uliotokea na kusababisha vifo vya wenzetu, kikundi kingine kinasema wanaingiza udini! Je, mimi mpagani nikisema nimeingiza upagani?
  Mashehe wanasema maaskofu hawakufanya vizuri kutomtambua meya wa Arusha! Wanasema kuna mwelekeo wa udini kwa sababu eti maaskofu ni watu wa dini.
  Sijui kama ni kwa kutofahamu au fikira kidogo mno mimi sielewi. Chitanda na Makamba nao wanakejeli maaskofu!
  Mimi nawauliza, kwani mimi wanasiasa ni nani na maaskofu ni akina nani? Hivi hawa wote si Watanzania? Mimi naona tuache ushabiki wa kipumbavu na usokuwa na maslahi kwa taifa letu. Maaskofu na mashehe ni Watanzania ambao kwa mtu mmoja mmoja au kwa makundi wanaweza kutoa maoni yao na misimamo yao kama Watanzania wengine.
  Kinachonipa shida kubwa ni kitu kimoja: Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa maaskofu wanakemea bila kuingiza kwamba eti ni udini fulani. Lakini watu wengine wanaona matamshi yao eti ni udini. Sasa kweli huu ni ufinyu wa mawazo na nafikiri kama hapa Tanzania kuna watu wenye busara basi watashughulikia suala hilo liishe. Hakna cha ushehe wala uaskofu, hapa wote ni Watanzania na tunatakiwa kukemea chochote ambacho tunaona kinaashiria upotevu wa amani ya nchi yetu.
  Halfu nyie viongozi wenye dhamana, sisi wananchi tumewaweka hapo si kwa maslahi yenu na matumbo yenu na watoto wenu na ndugu zenu! Mpo hapo kwa ajili yetu sisi wote kama Watanzania. Hivi inakuwaje mlinde maslahi yenu kwa kulazimisha mpaka mnatuma polisi waue binadamu wenzenu. Mnataka kusema hayo madaraka mliyonayo ni muhimu kuliko uhai wa binadamu wenzenu? jamani nashindwa tu niseme nini lakini ukweli ni kwamba mimi binafsi nimeshangazwa sana kuona hamjali kabisa na mnaona waliokufa kama sisimizi hivi!
  Hivi inakuwaje mtu anasema eti tatizo lililotokea Arusha ni la kisiasa baada kuona watu wamekufa? Kwa nini hilo halikushughulikiwa mapema kabla haya mambo ya ajabu nchini kwetu hayajatokea? Hebu nyie wote mliosababisha haya mambo achieni ngazi mlizonazo ili wale wanaowenza kuongoza na kuthamini jutu wa wenzao washike hayo madaraka.
  ETI MAASKOFU WAVUE MAJOE WAENDE KWENYE SIASA!! HUU NI UPUMBAVU KABISA, MAITI ZA WATU ZIKO NDANI< WATU WANAHUZUNIKA< WAMEACHA WATOTO. WEWE KWA SABABU YA UROHO WA MADARAKA UNAENDELEA KUTETEA TUMBO LAKO! UKOME KABISA.
  Halafu kitu kingine, hivi nyie mnaojiita wasomi wa chuo kikuu mko wapi? Hivi usomi wenu wote na akili zenu zote mmekaa kimya tu siasa Tanzania inaenda visivyo mpaka watu wanauawa. Nyie mnaendelea kukaa tu na hamsemi chochote? Hapana mimi naona nchini kwetu sasa kuna kitu fulani kinakosekana. HIVI MPO TAYARI KUONA MTU ANAKUFA KWA UPUMBAVU HUU KWELI? JAMANI MAISHA YA MTU KUPOTEA SI MCHEZO!! Acthari zake ni mbaya. TUREKEBISHE HAYA HARAKA SANA. Hapa tuhusike wote hakuna cha askofu, padri, mchungaji, shehe au rais, waziri, sijui chama gani. Wote tuje pamoja tuone shida iko wapi na mambo haya yakome kabisa kabisa.
  Hivi nyie viongozi wetu tafadhari sana suala hili liwe mwisho! Uonevu huu uwe mwisho kabisa kabisa. Maisha ya mtu ni kitu kisichotakiwa kuchezewa hivyo!
  Watu wanakufa na majambazi, mnasema polisi hawana vifaa vya kutosha! Vipi mngechukua hizo fedha za DOWANS mkawanunulia polisi vifaa vizuri kwa ajili ya kulinda amani watu wasiuawe na majambazi hamwoni mngekuwa mmefanya kitu chema zaidi kuliko kuwalipa DOWANS ambao mliwaleta nchini halafu tena mnasema hamuwajui hivyo mnawalipa kivuli. Jamani msituharibie nchi yetu.
  TAFADHALI SANA TUWE SERIOUS NA NCHI YETU!!!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MASKOFU NA MASHEHE, KABLA YA WADHIFA WAO KWANZA NI WATANZANIA HIVYO KUKEMEA MAOVU HAKI YAO

  Nashangaa sana harufu ya udini anayoweza mtu kulazimisha katika hoja ya MAASKOFU KULE MJINI ARUSHA ni upi huo hasa? Maana mpaka dakika hii MAASKOFU wametangaza wazi kwamba hawamtambui MEYA WA CCM JIJINI ARUSHA, ambaye naye ni MKRISTO SAWASAWA na hao Maaskofu, KWA KUZINGATIA JINSI ALIVYOINGIZWA OFISINI KIMABAVU.

  Kimsingi MAASKOFU walisema wazi kwamba wanachokipinga kwa meya huyu wa CCM wala si maovu ya kuwa mwana-CCM, si maovu ya UKRISTO wake isipokua MAOVU WANAYOYAKEMEA ni sheria na taratibu za uchaguzi zilivyopindishwa kumuingiza madarakani kupitia mlango wa nyuma.

  Sasa viongozi wetu wa kiroho wasipokemea maovu kama haya, ukimya wao juu ya jambo hatari kama hili tafsiri yake ni kwamba wameunga mkono huo uchafu na ubakaji wa DEMOKRASIA, ndivyo watu mnavyotaka????????????????

  Kama shida ni kuhusu vifo vya raia wa Tanzania na hata yule wa nchi rafiki na jirani Kenya, nadhani mtu asijaribu kuziba wengine midomo. Mauaji ya pemba 2001 vingozi wa dini walipiga kelele sana na kuikemea serikali ya Mhe Mkapa wakisema nguvu nyingi kupita kiasi imetumika dhidi ya wananchi. Katika kundi hilo kulikwepo Mashehe, Maaskofu, Mapadri na Wachungaji kwa mchanganyiko wake.

  Hivyo kutokana na ukweli huu ambao iko mikononi mwao waandishi wa habari mpaka leo hii, ni matumaini yangu kwamba hauna maana yoyote kutaka kutuambia ya kwamba kama kilio cha Watanzania hakikusikilizwa tulipoipigia kelele mauaji ya Pemba basi leo hii raia tunapouaua tusiseme kwa sababu kule hatukusilizwa vile vile.

  Pia, sitaki niaminishwe ya kwamba mweka hoja hii anajaribu kutuambia kwamba MAUAJI YA KINYAMA ARUSHA kwa vyovyote vile yalitekelezwa na MTU AU WATU anaowajua yeye ILI KUSAIDIA KUMLIPIA KISASI CHA MAUAJI YA PEMBA leo hii hivyo anaona hadi sasa ngoma ni droo na wala kusilalamike mtu?

  Mwisho, imekuaje mtoa mada umekwepa kujiuliza maswali yote ya msingi hapa; Je, MASHEHE NA MAIMAMU kukaa kimya bila kukemea mauaji ya kinyama Arusha hadi kujitokeza tu kutetea Mhe kwa sura nyingine ya ajabu ajabu tu inamaana wanayo agenda gani?????????
   
 3. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #3
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uchu wa madaraka ndiyo uliowaua hawa. wameshindwa uchaguzi sasa wanataka kuleta fujo.
   
 4. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Maaskofu wamefanya kosa ingawa hawataki kusikia hilo, kiongozi hahitaji mpaka kanisa limtambue wao ni kina nani mtaka kiongozi i.e rais, waziri mkuu, meya, mkuu wa mkoa au jaji mkuu akichaguliwa au kuteuliwa wao ni lazima wamtambue, maaskofu wamevuka mipaka ya kazi yao na wameingia katika malumbano ya kisiasa, unless wangetoa maoni binafsi tu.
  waislamu wanao wamejibu mapigo kwa kusema ukweli kuwa pamoja na kuwa si kazi ya madhehebu ya dini kutangaza kuwatambua viongozi wa kisiasa lakini kwa Vile wakristu wametoa tamko basi nao wamesema wanamtambua meya wa jiji la arusha na watampa kila aina ya ushirikiano katika kutenda kazi zake.

  Kweli watu wamekufa suala hapa wamekufa katika mazingira gani, binafsi naona viongozi wa chadema ambao hawaitakii mema nchi hii kwa sababu ya tamaa binafsi za kisiasa na bila kufikiria kwa kina waliwashawishi watu ambao pia uwezo wao ni mdogo katika kufanya risk analysis na kujitoa mhanga kwenda kinyume cha tamko halali la serikali, hivyo kuleteleza vifo vyao maana kama wangetii amri ya serikali hayo yasingetokea.
  Sasa kama kila mtu akiamua kujifanyia kitu anachotaka bila kufuata taratibu zilizowekwa tutafika wapi? kutakuwa tena na haja ya kuwa na serikali au tutakuwa kama somalia, na nini maana ya utawala wa sheria kama watu hawataki kutii amri za serikali au mnafikiri utawala wa sheria ni upande mmoja tu wa serikali????????

  Nasikitika watu wamekufa lakini tatizo na chanzo ni viongozi wa chadema wasioitakia mema tanzania kwa manufaa binafsi na wafuasi wao, hivyo wajilaumu wenyewe
   
 5. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Kabadilishe pedi weweee...
  Huna lolote unalojuwa zaidi ya kukariri taarab tu.
   
 6. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani mbona tunasahau kuwa Mashehe, Maaskofu na viongozi wote wa dini mbalimbali; pia wao ni wapiga kura za kuchagua viongozi!! Hivyo wana haki sawa ya kusema, kukosowa na kukemea jambo lolote ambalo liko kinyume na haki ya binadamu. Viongozi hawa wa Madhehebu/Dini mbalimbali wakati wa chaguzi huombwa kura na wagombea nao hupiga kura;hivyo ni haki yao kusema au kupinga wanapoona uchaguzi haukuwa wa haki. Sio kwamba wao wakubali tu hata kama kiongozi kawekwa kibabe au kwa kuchakachua.
   
 7. P

  Percival Salama Senior Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitahadharisha mengi kuhusu mustakabali wa nchi yetu. akafundisha mengi, akaonya mengi nk. nk. Mojawapo ya mambo aliyotufunulia mapema ni jinsi ya kujua VIONGOZI WALIOFILISIKA SERA NA FIKRA KICHWANI. kwa maneno yake alisema "Watu a.k.a Viongozi waliofilisika sera kichwa wakishindwa kujihalalisha kwa ubora wa uongozi wao, basi aidha wataanza kujihalalisha kwa UDINI, UKABILA, UKANDA, UMKOA n,k. Akasema wao kama awamu ya kwanza kuna mema walitenda na kuna ya kujinga walifanya. akatuambia LA AJABU NI KWAMBA VIONGOZI WETU WANAYATUPA YALIYO MEMA NA KUKUMBATIA YA KIJINGA!!

  Kwa mtu anayefuatilia kauli na matendo ya viongozi wetu katika Tanzania ya leo bila shaka atakubaliana na Mwalimu Nyerere kwamba hiki ndicho kinachotokea sasa TZ.
   
 8. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wenye akili timamu watakuelewa. Wenye akili timutimu hawatakuelewa.
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Jamani waandishi wa Habari watatupeleka pabaya kwa tamaa zao au ukosefu wa maadili ya kazi zao!!
  Kwa bahati mbaya taarifa ya Habari ya ITV siku ya Jumapili sikuweza kuingalia moja kwa moja lakini niliirikodi. Ni leo nimepata nafasi ya kuiangalia na bahati nzuri kulikuwa na taarifa inayohusiana na matamko ya viongozi wa dini kuhusu mauwaji ya Arusha. Kilichojitokeza ni kua mashehe walichosema ni kulaani vitendo vya machafuko kwa kusema kuwa wao Waislamu pamoja na wananchi wa madhehebu na dini nyengine wanalani vitendo vilivyoathiri shuguli zao.( mwandishi hakuwa tayari kuandika hivyo kwa vile alikwishaamuwa kuwa hilo ni suala la udini na kusema hasa kilchosemwa kungemuharibia lengo lake.

  Ikafuata hotupa ya Askofu Shayo ambaye alitaka Waziri Mkuu kusimamia mazungumzo ya wahusika katika mgogoro na Askofu Laizer alimpongeza Naibu Meya kwa kujiuzulu na akapendekeza hata Mheshimiwa Meya (Alitumia neno muheshimiwa) basi angefuata mfano wa Naibu Meya.
  Sasa wenzangu huo udini uliozungumziwa na mwandishi uko wapi hap? Hata mtiririko wa habari haukukaa sawa kwa vile kulikuwa na upotoshaji wa suala zima.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Mwalimu alituusia kuikemea kwa nguvu zote dhambi ya ubaguzi. Tusipokuwa makini, hatutaishia hapa.

  "Nyoka huyo!, ...na apite!"

   
Loading...