Hivi haya ni maendeleo au matatizo?

Baba Kapompo

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
1,344
462
Kijana ana mshahara Gross TSHS 1,000,000/= baada ya makato NET yake TSHS 780,000/=

Baada ya probation period na kiu za kumeremeta kijana kachukua mkopo ofisini TSHS 12,000,000/= kachukua Altezza 9m, flat screen 1.5m iliyobaki kalia burudani, 12m yote imekata.

Makato kila mwezi ya mkopo TSHS 300,000/= so anabaki na NET income ya TSHS 480,000/=! Altezza 6 cylinder kila siku linataka wese la walau buku kumi, kwa mwezi ni laki 3 hiyo kwa hiyo balance toka kwenye ile laki nne 80 ni 180,000/=.

Hiyo ndo ale, alewe, girlfriends na kodi humo humo!! Hivi hii ni akili au ukwaju?
 
Wewe baki hivo hivo wenzio baada ya hapo wanafukuzia fursa zinazojitokeza km kukutana na suppliers nk maisha yanaenda!
 
Kama haji kukopa wala kukuibia pindi akiishiwa una haja gani kumsema?

Je wajua alihangaika kwa kiasi gani mpaka kufikia kupata kazi ya kumlipa hiyo 1,000,000.00, si ilikuwa ni mipango yake?

Angalia maisha yako achana naye
 
Kila mtu anaaamua kufanya kile anachoona ni bora kwake. Ukiuliza hapa kipi ni cha muhimu kwenye maisha, hautapata jibu moja. Kuna mtu atakwambia gari, mwingine nyumba, mwingine kuwekeza n.k

Tofauti tu ni kwamba, wamechukua muda kiasi gani kufikiria kwa kina kuhusu hayo maamuzi yao na wameomba ushauri kwa watu wa aina gani.

Mwisho wa siku, kila uamuzi tunaoufanya una gharama zake.
 
Uache kupotosha umma!
Matumizi ulieka hapo, baadhi yao ni matumizi ya mara moja kwa mwaka au hata miaka miwili na kuendelea!

Na sio matumizi ya kila mwezi kama unavyotaka tuamini!
 
Kijana ana mshahara Gross TSHS 1,000,000/= baada ya makato NET yake TSHS 780,000/=

Baada ya probation period na kiu za kumeremeta kijana kachukua mkopo ofisini TSHS 12,000,000/= kachukua Altezza 9m, flat screen 1.5m iliyobaki kalia burudani, 12m yote imekata.

Makato kila mwezi ya mkopo TSHS 300,000/= so anabaki na NET income ya TSHS 480,000/=! Altezza 6 cylinder kila siku linataka wese la walau buku kumi, kwa mwezi ni laki 3 hiyo kwa hiyo balance toka kwenye ile laki nne 80 ni 180,000/=.

Hiyo ndo ale, alewe, girlfriends na kodi humo humo!! Hivi hii ni akili au ukwaju?

Ndugu usichukue kipimo cha mtu mwingine ukajipima wewe utachanganyikiwa..
Kila mtu ana mtizamo wake na malengo yake pia..
 
Habari nyingine bwana utadhani wanaoleta hizi mada ni wazee wa vijiwe vya kahawa! sasa wewe tatizo lako nn au anapoishiwa anakukopa?, wivu ni tabia mbaya hasa kwa wanaumeee!!!!
 
Si kila kila aliyeajiriwa ni masikini unaweza kuta kapewa nyumba na hata biashara na baba yake hivyo hilo. gari na simu ndicho alichokiona cha msingi kilichobaki
 
We unashangaa mwenye gloss ya 1,000,000 wengine wanapata 600k na bado wananunua magari, tupo tofauti mwingne anaona kuwa na gari ndio furaha yake na mwingne ataona nyumba ni muhimu, cha msing wacha maisha yaendelee
 
Jadili hoja iliyowekwa mezani acha hasira kwasababu sikuzote ukweli unauma issue hapa ni namna ya kupangilia vipaumbele katika maisha ya mtu mwenge utimamu wa ability. Kwahiyo hoja ni ya msingi kabisa lazima ukiwa kama binaadamu mwenye utimamu wa akili ujue ku-set priorities otherwise huwezi kufanikiwa kimaisha.Ni sawa na mtu anskopa fedha bank unalipia nyumba ya kupangilia you must be stupid by100%
 
Ila mshahara wa 1m ni parefu ndugu yangu kwa mishahara ya serikal, mtu mpaka alipwe milion ujue kustaafu kunakaribia
 
Kijana ana mshahara Gross TSHS 1,000,000/= baada ya makato NET yake TSHS 780,000/=

Baada ya probation period na kiu za kumeremeta kijana kachukua mkopo ofisini TSHS 12,000,000/= kachukua Altezza 9m, flat screen 1.5m iliyobaki kalia burudani, 12m yote imekata.

Makato kila mwezi ya mkopo TSHS 300,000/= so anabaki na NET income ya TSHS 480,000/=! Altezza 6 cylinder kila siku linataka wese la walau buku kumi, kwa mwezi ni laki 3 hiyo kwa hiyo balance toka kwenye ile laki nne 80 ni 180,000/=.

Hiyo ndo ale, alewe, girlfriends na kodi humo humo!! Hivi hii ni akili au ukwaju?

aisee uzi wako umewagusa vijana wengi malimbukeni.
 
Habari nyingine bwana utadhani wanaoleta hizi mada ni wazee wa vijiwe vya kahawa! sasa wewe tatizo lako nn au anapoishiwa anakukopa?, wivu ni tabia mbaya hasa kwa wanaumeee!!!!

We huoni kuna tatizo hapo? ,unajisikiaje unapozungukwa na watu wenye madeni?,je unajua matatizo ya rushwa yanachangiwa na watu kama hawa...........
 
Back
Top Bottom