Hivi haya maneno yanatoka wapi? "Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina"

Dini zote mbili zinaamini katika Mungu mmoja , kiongozi ni wa watu wote ni lazima aseme salamu zote mbili akisema moja tayati ubaguzi . Kutoa salamu sio lazima uwe muumini wa hiyo dini .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
wanasemaga alale kwa amani,, Kwani tukifa mbinguni tunaenda kulalaga tuuu... au tunaenda kupumzikaga
 
Kipindi cha kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wetu JPM kila aliyekuwa anatoa hotuba si muislamu si mkiristu alikuwa anahitimisha kwa hayo maneno. Sasa nimekuwa nikijiuliza hayo maneno ni ya kidini au ni ya kiserikali? Hebu tuacheni unafiki tuongee tu ule ukweli. Mkiristu haamini mambo ya uislamu na wala hakubaliani na Mtume Mohamad, hivyo hivyo kwa muislamu haamini "kihivyo" mambo ya ukiristu. Muislamu anaamini Yesu (Isa bin Mariamu) kama mmojawapo wa mitume na sio mwana wa Mungu au Mungu kama mkiristu anavyoamini. Sasa hayo maneno yenye kichwa cha habari ni ya kiserikali au ni ya kidini? Na kama ni ya kidini ni ya dini gani?

Pia hata hizi salamu za "Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristu na Salaam Aleykhum" zimekuwa zikitumiwa na viongozi wa dini zote, si waislamu si wakiristu. Kwa muktadha wa hoja yangu, Je inakuwaje mtu asiyeamini kwenye uislamu aseme "Salaam Aleykhumu, na asiyeamini kwenye ukiristu aseme Bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristu?" Hamuoni kama huu ni unafiki? Bora hata mama yetu ameamua kutoa salamu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana ni kama unafiki kusema Salam Aleykhumu wakati huamini mafundisho ambayo ndio chimbuko la hiyo salamu au kusema tumsifu Yesu Kristu wakati huamini kile wanachokiamini wale wanaotumia hiyo salamu.
Wana siasa wa Tanzania ni wanafiki katika Dini zao wanacho fuata ni kufarahisha wapiga kula wao, eti mwendazake nae alikua anava kanzu na kibaragashia aonekane kama muislamu, ila raho yake ilikua sio ya dini ya kiislamu.
 
Dini zote mbili zinaamini katika Mungu mmoja , kiongozi ni wa watu wote ni lazima aseme salamu zote mbili akisema moja tayati ubaguzi . Kutoa salamu sio lazima uwe muumini wa hiyo dini .

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
Kidogo nimekupata mkuu ila nakuomba utafakari kidogo hoja yangu. Labda nikupe starting point ya kuanza kutafakari. Let's say wewe ni mkiristu. Unaamini kuwa Yesu Kristu ni Bwana na Mwokozi, yeyote asiyemuamini hawezi kuurithi ufalme wa Mungu. Maana tunaambiwa Yesu ndie njia na uzima. Sasa unapotoa Salamu ya Salaam Aleykhumu huoni indirectly unautangaza uislamu, sijui kama unanielewa?
Kwa upande wa pili tena kama let's say wewe ni Muislamu na unaamini bila kuyakubali mafundisho ya Mtume Muhamad huwezi kuiona pepo maana tunafundishwa Quran ni kitabu kisichokuwa na shaka na uislamu haujaanza leo wala jana ulianza toka kipindi cha Ibrahim, so unaposalimu watu kwa salamu ya Bwana Yesu asifiwe huoni kama indirectly unaufundisha ukiristu?
 
Wana siasa wa Tanzania ni wanafiki katika Dini zao wanacho fuata ni kufarahisha wapiga kula wao, eti mwendazake nae alikua anava kanzu na kibaragashia aonekane kama muislamu, ila raho yake ilikua sio ya dini ya kiislamu.
Hongera mkuu. Yaani upo objective 100%. Kuna wengine hapa bado wanaleta unafiki. Hii hoja wanaiona eti ni ya udini. Sijui kusoma na kutafakari hawawezi au?
 
Maneno ni ya kidini..
Dini ya kiislamu na kikristo
Kuna mda inabidi uyatumie kwenye eneo husika kutokana mlengwa wa shughuli upande aliopo.mfano marehemu ni mkristo basi msiba ni wa kitaifa/kiserikali lakini wa kikristo
So kama NI was kitaifa watakuja watu mchanganyiko was imani zote.
Na kutumia salaam ya iman ya mwingine haidhuru.
Ni njia ya kuonyesha uungwana tu
Nakazia: Ni njia ya kuonesha uungwana na umoja i.e. tuko pamoja katika tukio hili.
 
Kipindi cha kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wetu JPM kila aliyekuwa anatoa hotuba si muislamu si mkiristu alikuwa anahitimisha kwa hayo maneno. Sasa nimekuwa nikijiuliza hayo maneno ni ya kidini au ni ya kiserikali? Hebu tuacheni unafiki tuongee tu ule ukweli. Mkiristu haamini mambo ya uislamu na wala hakubaliani na Mtume Mohamad, hivyo hivyo kwa muislamu haamini "kihivyo" mambo ya ukiristu. Muislamu anaamini Yesu (Isa bin Mariamu) kama mmojawapo wa mitume na sio mwana wa Mungu au Mungu kama mkiristu anavyoamini. Sasa hayo maneno yenye kichwa cha habari ni ya kiserikali au ni ya kidini? Na kama ni ya kidini ni ya dini gani?

Pia hata hizi salamu za "Bwana asifiwe, tumsifu Yesu Kristu na Salaam Aleykhum" zimekuwa zikitumiwa na viongozi wa dini zote, si waislamu si wakiristu. Kwa muktadha wa hoja yangu, Je inakuwaje mtu asiyeamini kwenye uislamu aseme "Salaam Aleykhumu, na asiyeamini kwenye ukiristu aseme Bwana Yesu asifiwe au tumsifu Yesu Kristu?" Hamuoni kama huu ni unafiki? Bora hata mama yetu ameamua kutoa salamu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana ni kama unafiki kusema Salam Aleykhumu wakati huamini mafundisho ambayo ndio chimbuko la hiyo salamu au kusema tumsifu Yesu Kristu wakati huamini kile wanachokiamini wale wanaotumia hiyo salamu.
Tatzo la mtoa mada ni uelewa tu. Hivi salamu inapotolewa hua inaangalia Nini. Kwan unaposalimia mtu kwa kiingereza wewe tayari ni mwingereza. Nahisi huyu ana chuki binasfi na marehemu. Salamu za watu zinakukwaza na Nini.

Hivi Mimi na mwarabu tunapokutana tutatumia maneno gan kusalmiana ikiwa anajua kiarabu tu. Na wewe unajua kiarabu japo sio mwislamu. Utatumia salamu gan hapo? Hiyo ni lugha tu Wala isikupe shida

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom