Hivi haya majina ya vitu vipya kwa Kiswahili nani huwa anatunga?

Stress Challenger

JF-Expert Member
Feb 24, 2022
1,778
4,282
Wawe wanashirikisha wadau bana.

Na hata kama hawashirikishi wengine watunge basi majina ama maneno mazuri. Sasa kama hili kishkwambi Yani unaltamka huku umekunja uso. Angalau wangeita tu tableti.

Mengine yanayokera jokofu wangeacha tu friji. Smart phone Eti simu janja. Eti password nywila unabaki kushangaa WTF?! Angalau wangeita tu paswedi.

Nahisi ni wakenya Hawa kwasababu juice eti kinywaji tamu unabaki kukasirika tu afadhali bongo tumekomaa na juisi. Shirikisheni wadau mnapotunga nakuita vitu kwa majina ya ajabu ajabu.

Sijui drones wanaziitaje?
 
Kiswahili lugha adhimu kabisa.

Mapendekezo yako ni kwamba kiswahili "kisingekuwepo kabisa", maana kila neno la kiingereza umependekeza kiswahili chake kiwe ni "kiingereza kiswahili". Nadhani sio sawia.

Umependekeza hivi:
1. Tablet ingeitwa tableti.
2. Fridge ingeitwa friji

Kwa mtazamo huo kiswahili kama lugha itakua vipi endapo itajibanza kwenye kiingereza kwenye kila kitu mkuu ?

Neno KISHKWAMBI ni neno mujarab kabisa lisilo na tashwishwi yoyote. Na hiyo ndio ladha halisi ya lugha ya kiswahili.

Karibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom