Hivi haya Magorofa ya kisasa yenye kuta za vioo ni Salama? Kwanini imekuwa mtindo?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
783
3,207
Siamini kabisa haya majengo marefu yenye kuta za vioo

Unakuta jengo halina hata tofali, najiuliza hivi ule ukuta wa kioo unaweza ukaegamia kwa amani?

Ikitokea tetemeko vipi?

Sababu kubwa za kutumia vioo karika ujenzi wa magorofa makubwa ni jini?

View attachment 1859304
 
Siamini kabisa haya majengo marefu yenye kuta za vioo,

Una elimu gani? Maana kukuelewesha hapa zitatumika terminologies ambazo kuzielewa elimu inatakiwa iwe kubwa kidogo.
 
Siamini kabisa haya majengo marefu yenye kuta za vioo,
Unakuta jengo halina hata tofali, najiuliza hivi ule ukuta wa kioo unaweza ukaegamia kwa amani?

Ikitokea tetemeko vipi?

Sababu kubwa za kutumia vioo karika ujenzi wa magorofa makubwa ni jini?
Acha kutia aibu basi mkuu Kuna ukuta wa kioo wapi ndugu nije kushangaa🤪🤪🤪🤪🤪
 
Unapoona Vitu hatalishi kama hivyo vimekubalika katika maeneo hatalishi basi ujue pale ukomo wako ulipoishia ndio wenzako wakaanzia kwenda juu...

Kuta za vioo Ni Salama kwa kiwango ambacho huwezi zania,

Kile kioo unachokiona pale kina upana wa mm12, vinakua viwili ndani 6mm iliyokua subject to Tension katikati 1mm kwa ajili ya hewa halafu nje 6mm nyingine iliyokua subject to compression(Ulisoma Effects of forces 4m2?)

Kitaalam wanaita Tempered glass,
Ni kioo cha kawaida kinachopitishwa kwenye joto la 600°c-1400°c baada ya hapo kinapitishwa kwenye very high pressure cooling air system kinapozwa haraka sana ndani ya sekunde kadhaa..

Kitendo hiki kinafanya upande wa nje kusinyaa(ref kutanuka na kusinyaa kwa mada) hii inaleta compression halafu upande wa pili unajivuta kutoka nje na kutengeneza tension, kazi inakua imeisha na hapa ndipo sifa ya ugumu wa hivyo vioo unapopatikana, na vinakua na ugumu ×5 ya kioo cha kawaida..

Sasa Vingine vinakua laminated, yaani pale kati baada ya kuacha space ya hewa wanaweka plastic ambayo nayo ni transparent kama kioo halafu process kama hio inafanyika, hiki cha namna hii sasa ndio usiombee.

Kutokana na hizo mechanical process hapo unafanya pia hicho kioo hata kikipasuka, badala ya kutoa vipande vikubwa kubwa vinavyoweza kumkata mtu, inatoa chenga chenga ndogo(ushawahiona kioo cha gari kimepasuka?)

Hawatumii kioo kwenye ujenzi eti ili kufanya jengo livutie.. kuna advantage nyingi sanaaa...

1. Kupata mwanga wa Asili hii hupelekea kupunguza gharama za umeme kuwasha taa mda wote kwa ajili ya mwanga
2. Kupunguza uzito hatimaye gharama ndogo za msingi..
3. Haviungui,(Tumeona kilichompata mwenzetu kule kimara)
4. Kioo hakiathiliwi na hali ya hewa(nahisi unaelewa ukuta wa nyumba uliopigwa rangi ukipigwa sana na jua)
5. Ni water na dustproop( kii hakipitishi maji na hakipokei vumbi kirahisi na ikiw hivyo kinafutika kirahisi).
6. Ujenzi wa haraka..

Nimejitahidi kutumia terminology nyepesi kadiri niwezavyo japo ni ngumu kuelewesha baadhi ya mambo kwa kiswahili.

NOTE: usalama wa kitu chochote una ukomo wake, katika matumizi ya kawaida na emergency, ukizidisha yatakukuta kama ya 👇
Screenshot_2021_0719_102746.png

Na ukienda ukajaribu menginenyo mimi simo.
 
Ziko salama sana mkuu, tena kuweka hizo tofali ndo kunaongeza mzigo katika jengo, elimu elimu elimu
 
Siamini kabisa haya majengo marefu yenye kuta za vioo,
Unakuta jengo halina hata tofali, najiuliza hivi ule ukuta wa kioo unaweza ukaegamia kwa amani?

Ikitokea tetemeko vipi?

Sababu kubwa za kutumia vioo karika ujenzi wa magorofa makubwa ni jini?
View attachment 1859304
Mkuu 'skelton' ya ujenzi mkubwa ni beam.

Beam kama ipo ya kiwango, kuta hata zingelikuwa za mbao ama box ghorofa linasimama imara tu.

Jambo jingine, katika kuboresha mjadala huu, tembelea hizo ghorofa unazosema na uingie ndani, uone kama hivyo vioo kama ni mhimili wa hilo jengo.

Utakuta vyumba na kila kitu humo ndani ni vya block kama kawaida, isipokuwa mzunguko wa nje kwenye vibaraza ambapo mijengo ya zamani walijenga kama sehemu za kupungia hewa ndiyo iliyozibwa kwa vioo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashangaa mtu anamcheka mtoa mada au kumshangaa halafu hamsaidii chochote..

Mkuu Unapoona Vitu hatalishi kama hivyo vimekubalika katika maeneo hatalishi basi ujue pale ukomo wako ulipoishia ndio wenzako wakaanzia kwenda juu...

Kuta za vioo Ni Salama kwa kiwango ambacho huwezi zania,

Kile kioo unachokiona pale kina upana wa mm12, vinakua viwili ndani 6mm iliyokua subject to Tension katikati 1mm kwa ajili ya hewa halafu nje 6mm nyingine iliyokua subject to compression(Ulisoma Effects of forces 4m2?)

Kitaalam wanaita Tempered glass,
Ni kioo cha kawaida kinachopitishwa kwenye joto la 600°c-1400°c baada ya hapo kinapitishwa kwenye very high pressure cooling air system kinapozwa haraka sana ndani ya sekunde kadhaa..

Kitendo hiki kinafanya upande wa nje kusinyaa(ref kutanuka na kusinyaa kwa mada) hii inaleta compression halafu upande wa pili unajivuta kutoka nje na kutengeneza tension, kazi inakua imeisha na hapa ndipo sifa ya ugumu wa hivyo vioo unapopatikana, na vinakua na ugumu ×5 ya kioo cha kawaida..

Sasa Vingine vinakua laminated, yaani pale kati baada ya kuacha space ya hewa wanaweka plastic ambayo nayo ni transparent kama kioo halafu process kama hio inafanyika, hiki cha namna hii sasa ndio usiombee.

Kutokana na hizo mechanical process hapo unafanya pia hicho kioo hata kikipasuka, badala ya kutoa vipande vikubwa kubwa vinavyoweza kumkata mtu, inatoa chenga chenga ndogo(ushawahiona kioo cha gari kimepasuka?)

Hawatumii kioo kwenye ujenzi eti ili kufanya jengo livutie.. kuna advantage nyingi sanaaa...

1. Kupata mwanga wa Asili hii hupelekea kupunguza gharama za umeme kuwasha taa mda wote kwa ajili ya mwanga
2. Kupunguza uzito hatimaye gharama ndogo za msingi..
3. Haviungui,(Tumeona kilichompata mwenzetu kule kimara)
4. Kioo hakiathiliwi na hali ya hewa(nahisi unaelewa ukuta wa nyumba uliopigwa rangi ukipigwa sana na jua)
5. Ni water na dustproop( kii hakipitishi maji na hakipokei vumbi kirahisi na ikiw hivyo kinafutika kirahisi).
6. Ujenzi wa haraka..

Nimejitahidi kutumia terminology nyepesi kadiri niwezavyo japo ni ngumu kuelewesha baadhi ya mambo kwa kiswahili.

NOTE: usalama wa kitu chochote una ukomo wake, katika matumizi ya kawada na emergency, ukizidisha yatakukuta kama ya View attachment 1859335
Na ukienda ukajaribu menginenyo mimi simo.
Asante Sanaa
 
Mimi tatizo ninaloliona ni moto.

Moto ukiwaka juu kwa zimamoto yetu iliyoshindwa kuzima moto soko la Kariakoo hapo itakuwaje?
 
Back
Top Bottom