Hivi hawa watangazaji wa vyombo vya habari mnawaelewa? Wamekaa kimasiharasihara tu

Yaani mtanganzaji anasoma vichwa vya habari vya magazeti vya asubuhi mwenzake anamuingilia na kuanza kuongea ujinga palepale studia. Kwa mfano leo watanganzaji wa kiss fm wa kipindi cha morning kiss wanasoma habari kwenye gazeti "Walimu 2000 wapandishwa madaraja kinondoni" halafu mwingine anachomekea "daraja la koko ama la wapi" hapo weledi wa habari upo wapi? kwanini vijana wamepotoka hivi?
Napenda sana kusikiliza radio,naweza kaa siku nzima nasikiliza redio ila hasa vipindi vya michezo,hasa efm ..sport headquaters na clouds sports extra..hapa namkubali edgar kibwana
 
Tulieni nyie wazee hizi zama nyingine, mambo hubadilika don't take everything seriously
 
Yaani mtanganzaji anasoma vichwa vya habari vya magazeti vya asubuhi mwenzake anamuingilia na kuanza kuongea ujinga palepale studia. Kwa mfano leo watanganzaji wa kiss fm wa kipindi cha morning kiss wanasoma habari kwenye gazeti "Walimu 2000 wapandishwa madaraja kinondoni" halafu mwingine anachomekea "daraja la koko ama la wapi" hapo weledi wa habari upo wapi? kwanini vijana wamepotoka hivi?
Ccm is the source of all evils. Discuss.
 
Mtangazaji Mbwiga wa Mbwiguke na Zomboko huku ni kunajisi tasnia. Mtangazaji Eddo Kumwembe ama Mauldi Baraka wa Kitenge pia unashangaa kusikia Shafii Dauda nae mtangazaji.
Tofautisha Kati ya mtangazaji (presenter) na mchambuzi,wengine hapo umewataja siyo watangazaji,wameingia studio kama wachambuzi (analysers). Wengine wameingizwa ili kunogesha vipindi,mfano Mbwiga au yule jamaa anaeigiza sauti ya kihindi.
 
Sawa basi nitajie sifa za kuwa mtangazaji achilia mbali sharti la serikali ya kuwa mwandishi wa habari ama mtangazaji awe na elimu kiwango cha chini ni diploma ya utangazaji na uandishi ni nani na hata kwenye uchambuzi ukiachilia maradhi yetu ya kubebana na kujidai hatujali kitu hakuna.
 
Clouds tv and radio hazina hadhi ya kuwa vyombo vya habari nafikiri waliwahi kufungiwa kwa kukosa maadili .

Radio nyingi sasa hivi zipo kufundisha watoto maadili mabaya na kucheza bongo fleva hakuna cha ziada
Wao wanajiita vituo vya burudani mkuu
 
Fani imeingiliwa.....ilimradi unaweza kuongea ongea mtandaoni tayari unabebwa kwenda kutangaza.
Kama kina baba levo, anaongeaga pumba hadi anakera.
Inasikitisha so! Sasa Majizo anamuweka Stive Nyerere studio sijui anataka nini
 
FM Radio zilikuwa Radoo One na RFA enzo zile sio sasa.

Hizi zingine hakuna kitu, kwanza watangazaji ni weupe vibaya mno kichwani mno, na vipindi vyao asilimia kubwa ni kama hawatacheza Miziki, basi ni mijadala ya fumanizi, majungu, maada ya Ndoa, maada ya Ma house Girl, hizo ndo Maada wanazimudu,

Hawa huwezi wasikia wakichambua Biashara kati ya Tanzania na Kenya,

Hawa wape maada za mafumanizi wanataririka mbaya
Nadhani naweza kuwa upande wako. Nikipata muda huwa nawasha radio one/free kwa ajili ya BBC/DW labda zaidi ya hapo sana ni vipindi vya kma michezo. Kuhusu habari nimeamua kutumia social media. Burudani ndio inasababisha nisipendelee kuangalia local contents ni sauti feki za watangazaji 😓
 
Back
Top Bottom