kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Nina hoja ambayo hata hivyo kwa vile nimegusa kundi la watu "wasiokosea" kwa kuwa tu wanajua mambo kwa undani zaidi,nipo tayari kupokea matusi na povu kama lote.
Hoja ya kwanza ni hii;Ninawasikia wasomi wakitoa takwimu kuwa kundi la vijana au niseme watoto kati ya miaka 15 - 25 wanaongoza kwa kasi ya maambukizi ya ukimwi.
Hatua za kudhibiti hili pamoja na nyingine,ni kuwakemea watu wazima hasa wa kiume wanaosemekana kuwaambukiza watoto hawa.
Je mmewahi kujiuliza kuwa tangu dawa za kufubaza virusi vya ukimwi zianze kunywewa Tanzania imeshafikia miaka 18?
Hawa watoto waliozaliwa na ukimwi,na wanatumia dawa hizi,hamjui kuwa sasa wapo hadi vyuo vikuu na hawajulikani kama wanaugonjwa huu?
Je, mnajisahaulisha kuwa watoto hawa vyuoni wanafanya ngono kama chakula wao kwa wao?kwa nini wasiambukizane?
Kwanini hakuna elimu kubwa kuwaonya watoto hawa wa kiume na kike waache ngono zembe kwa kuwa wenzao waliozaliwa na ugonjwa huu wanasoma nao bila wao kujua?
Hapo mnakwama wapi wasomi nyie mnashindwa kuwa amsha watoto hawa wasiendelee kuumia?
Naomba niishie hapa,nikiwa wazi kwenu kwamba ninasikitishwa sana na kuona mnashindwa kupigana vita halisi,badala yake mnaimba wimbo uliozoeleka wa fataki( mtu mzima mnene kama Peter Msechu) na mnasahau kuwa hawa "vimodo" ni hatari sana kwa kuwa mnawaaminisha watu kuwa wao hawawezi kuwa fataki.