Hivi hawa wasomi kwanini wanashindwa kujua vitu vidogo vidogo tu?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,642
2,000
Nina hoja ambayo hata hivyo kwa vile nimegusa kundi la watu "wasiokosea" kwa kuwa tu wanajua mambo kwa undani zaidi,nipo tayari kupokea matusi na povu kama lote.

Hoja ya kwanza ni hii;Ninawasikia wasomi wakitoa takwimu kuwa kundi la vijana au niseme watoto kati ya miaka 15 - 25 wanaongoza kwa kasi ya maambukizi ya ukimwi.

Hatua za kudhibiti hili pamoja na nyingine,ni kuwakemea watu wazima hasa wa kiume wanaosemekana kuwaambukiza watoto hawa.
Je mmewahi kujiuliza kuwa tangu dawa za kufubaza virusi vya ukimwi zianze kunywewa Tanzania imeshafikia miaka 18?

Hawa watoto waliozaliwa na ukimwi,na wanatumia dawa hizi,hamjui kuwa sasa wapo hadi vyuo vikuu na hawajulikani kama wanaugonjwa huu?

Je, mnajisahaulisha kuwa watoto hawa vyuoni wanafanya ngono kama chakula wao kwa wao?kwa nini wasiambukizane?

Kwanini hakuna elimu kubwa kuwaonya watoto hawa wa kiume na kike waache ngono zembe kwa kuwa wenzao waliozaliwa na ugonjwa huu wanasoma nao bila wao kujua?

Hapo mnakwama wapi wasomi nyie mnashindwa kuwa amsha watoto hawa wasiendelee kuumia?

Naomba niishie hapa,nikiwa wazi kwenu kwamba ninasikitishwa sana na kuona mnashindwa kupigana vita halisi,badala yake mnaimba wimbo uliozoeleka wa fataki( mtu mzima mnene kama Peter Msechu) na mnasahau kuwa hawa "vimodo" ni hatari sana kwa kuwa mnawaaminisha watu kuwa wao hawawezi kuwa fataki.
 

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,642
2,000
Huwa naumia sana kuona watu wamesomeshwa kwa gharama kubwa halafu uwezo wao wa kutatua changamoto unakuwa mdogo na wote wanaigana kufikiri.

Nikupe mfano mdogo tu mwingine,leo kuna wasomi waliobobea sana katika sayansi na tafiti kuhusiana na chanjo,wana hoji usalama wa chanjo za Covid 19, wakati huo huo wasomi wengine wanapigia kampeni chanjo,halafu anakuja msomi wa hapa kwetu anatukana watu kuwa wanapotosha kutokana na uelewa mdogo,je kwa nini asitusaidie kutwambia kama wasomi wenzake wanaopinga chanjo labda wana roho mbaya tu ndio maana wanatupotosha hivi?
Wasomi wanasayansi wenyewe wakibishana kwa nini watu wasibaki na Mungu?
Mleta uzi punguza hasira.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
8,710
2,000
Watu wanakemea ukimwi tu lskini mazingira ya kupata ukimwi yanaachwa na yanapaambwa,hauwezi kuisha.

Maadili yanapotea,wanamuziki wanaharibu jamii na kuhamasisha ufuska,wenye dhamana hawaaemi kitu wanaacha wanakuja kupambana na ukimwi.

Sebeni hii haitoisha,wewe kazi yako kutoa maji kwenye pipa lakini boma linoleta maji kwenye pipa unaliacha tu liingize maji,matokeo yake utaendelea kufanya kazi hiyo na maji hayatoisha kamwe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom