Hivi hawa wasichana huwa wanavutiwa na nini?

Jawai

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
526
394
Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka 25, nimemaliza chuo na ninafanya kazi na huwa sipendi kujikweza kwa watu, Nimetafuta sana mchumba ili kama tutaendana tufanye maisha pamoja lakini cha ajabu kila nikitupa ndoana sifanikiwi, kiasi ambacho huwa najiuliza hivi hawa wasichana huwa wanavutiwa na nini? Niombeni ushauri wanajf.
 
-labda sound zako ziko out ov date bana uez jua...

-vipi kuna kifaa kinaitwa mswaki sijajua kama una ushirikiano nacho mzuiri...

-umesomea shule za boyz miaka 6??
 
Wataka ushauri au mke? kama ni mke umempata. Kama ni ushauri labda unalenga matawi sio yako.
 
Inawezekana maana mi napenda sana wenye elimu ya kawaida kama vile hawe na elimu ya kidato cha nne au sita tu.
 
waschana/wachumba wanapenda unachokipenda wewe ingawa sio wote!!..kama umeshindwa kutambua wewe unapendelea nini basi itakuwa kazi kumpata mmoja wapo....
 
Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka 25, nimemaliza chuo na ninafanya kazi na huwa sipendi kujikweza kwa watu, Nimetafuta sana mchumba ili kama tutaendana tufanye maisha pamoja lakini cha ajabu kila nikitupa ndoana sifanikiwi, kiasi ambacho huwa najiuliza hivi hawa wasichana huwa wanavutiwa na nini? Niombeni ushauri wanajf.
Huwa wanavutiwa zaidi mshiko na uhakika wa maisha mazuri baada ya ndoa. Wewe unaweza ku-provide hayo?
 
Jsaudi; Mshiko cyo sana, ila uhakika wa maisha mazuri ninao japo ni kwa rehma za mungu kutokana na elimu yangu.
 
waschana/wachumba wanapenda unachokipenda wewe ingawa sio wote!!..kama umeshindwa kutambua wewe unapendelea nini basi itakuwa kazi kumpata mmoja wapo....

Sijakuelewa unamaanisha nini Prof, ushauri wako hupo general sana toa japo mfano kidogo.
 
Acha uBrotherman Dogo, Kuwa muwazi kwa demu unaempenda, mueleze ombi lako with confidence, acha longo longo unaonekana mtampotezea muda tuu. "Ukienda kuazima jamvi usitie story"!
 
Tatizo lako unatembea na four figure, muda wote unaongea hisabati, ukibadilisha mada unaongelea katiba, mabinti hawataki mambo magumu bwana.
Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka 25, nimemaliza chuo na ninafanya kazi na huwa sipendi kujikweza kwa watu, Nimetafuta sana mchumba ili kama tutaendana tufanye maisha pamoja lakini cha ajabu kila nikitupa ndoana sifanikiwi, kiasi ambacho huwa najiuliza hivi hawa wasichana huwa wanavutiwa na nini? Niombeni ushauri wanajf.
 
Acha uBrotherman Dogo, Kuwa muwazi kwa demu unaempenda, mueleze ombi lako with confidence, acha longo longo unaonekana mtampotezea muda tuu. "Ukienda kuazima jamvi usitie story"!

Sawa nimekusoma.
 
Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka 25, nimemaliza chuo na ninafanya kazi na huwa sipendi kujikweza kwa watu, Nimetafuta sana mchumba ili kama tutaendana tufanye maisha pamoja lakini cha ajabu kila nikitupa ndoana sifanikiwi, kiasi ambacho huwa najiuliza hivi hawa wasichana huwa wanavutiwa na nini? Niombeni ushauri wanajf.

hapo nilipo-bold ndio penye utata...kwa umri wako wachumba sahihi wanakuona bwana mdogo sana na utawapotezea muda atleast ungekuwa na age kama 30yrs hivi...ningekushauri kwa age yako uanze kutafuta mademu/girlfriends wa kucheza nao na possibly ma-girlfriend wako wanapatikana form 3-chuo mwaka wa kwanza. ukitafuta wa mwaka wa 4. lazma atakusumbua tuu. pole sana.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom