Hivi hawa wasanii wa kike kwanini hawawezagi kujitungia nyimbo?

screpa

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
10,792
15,693
Nimefatilia sana hawa wasanii wa kike waliopata kuwa na majina makubwa tangu zamani kama Ray C, Mwasiti, Linah, Rachel, Vumilia, Qeen Darlin, Pipi, Shilole, Snura, Vanessa Mdee, Ruby, Maua Sama, Nandy, Giggy, Mimi Mars, Amberlulu, n.k kwenye mahojiano kwa nyakati yofauti wakisema kutungiwa nyimbo zao na watu kama Barnaba, Amini, Ditto, Mario, etc tena sio kutungiwa tu wakati mwingine wanapewa hadi melody 'wanapita mulemule', je pengine hii ndio sababu huwa hawadumu sokoni? Tatizo nini hasa, mfano juzi nimemsikia Nandy anasema huo wimbo wake mpya alikuwa ameufanya Aslay akapewa, kwangu mimi huyu sio mwanamuziki bali ni mwimbaji. Kuandikiwa nyimbo sio tatizo, hata kule mbele wasanii wakubwa sometimes wanaandikiwa, but kutegemea 100% kuandikiwa wakati mwingine kupewa na melody kuna shida hapa. Nadhani udhaifu wa wasanii wengi wa kike ndio kunafanya kukosekane wa kukaribia legacy ya Lady Jaydee, wengi ni wasanii wa kutengenezwa na sio vipaji, na hii ndio ilichangia hata Rubby kuyumba sana alipotoka kwa kina Ruge, alizoea kupikiwa kilakitu yeye anaingiza vocal tu.
 
Misingi hawana. Nafahamu muziki/sanaa ni kipaji lakini kipaji huhitaji kunolewa na kutunzwa kwa mazingira wezeshi.
 
Muda ndio tatizo kama nandy muda wa kuandika anapata saa ngapi muda wote yupo kupigana madole na bill nass
 
Muda ndio tatizo kama nandy muda wa kuandika anapata saa ngapi muda wote yupo kupigana madole na bill nass
Mbona kina Diamond daily kuchezea viuno vya kina Mobetto pale Madale Guest House lakini anatunga ile mbaya? Usimsingizie mzee wa ndole 'Juma Nyosso'
 
Inategemeana kila mtu ana uwezo mahali pake anapopawezea vizuri...wengine kutunga hawajui ila wanajua kuimba vizuri.
 
umeshajijibu mwenyewe kuwa hao ni waimbaji.uandishi ni kipaji.unaweza kuwa na sauti usijue kuandika ,wapo wanaojua kuandika sauti hawana,rihana na beyonce na wasanii wengi wa r&b na pop.nao ni vivyo hivyo wanatungiwa wao wanaimba tu.
 
Back
Top Bottom