Hivi hawa wanawake wa kilokole(wafia dini) wana matatizo gani?

nilikuwa nikiona wanashambuliwa nikawa nahamaki saa nyingine napatwa na hasira kusikia wanasemwa vibaya kwani hata mimi ni mpendwa ila nimekuja kugundua kwa wale ninaowajua kuna kaujinga fulani wanao vichwani. Mimi nasema wasemwe tuu hizi tabia ni kweli zipo unakuta wanaolewa na makanisa na kazi za makanisa pamoja na huduma mbalimbali za makanisa badala ya waume wao. Ndoa ya Benny Hinn ilivunjika kwa sababu ya yeye kutokuwa na time na mkewe akaja kukiri mwenyewe 'I WAS MARRIED BY MINISTRY AND I FORGET THAT I HAD MARRIED A WIFE' kabla ya maombi ya wapendwa kuiombea ndoa yake kurudiana, mwangalie na Pastor Chriss Oyakhilome ndoa ilivunjika kifupi hawa dada zetu tabia ni kama hizihizi sasa lazima wafahamu ya kwamba kwa jinsi Mungu anavyotupenda hawezi kusimamia ndoa yenu ivunjike kwa sababu ya ujinga wako kujifanya upo bize sana na kanisa unaacha kuwahudumia watoto, na mumeo kumbuka Mungu ndie aliekupa huyo mume na atakuonesha namna ya kuishi nae usifate mapokeo ya madhehebu yenu. halafu saa nyingine unakuta dhehebu linaongozwa na mchungaji ambaye Un-educated and not civilized anakulazimisha kufanya mambo ya ajabu yanyohatarisha ndoa still unafuata tuu bila kujudge hii ni hatari ndio maana madhehebu mengine Mchungaji lazima awe ana kiwango fulani cha elimu japo sii lazima ila hii huwa inasaidia sana kupunguza ujinga ujinga unaofanyika makanisani saa nyikngine huwa nikiona napatwa na hasira sana wanavyofanya mambo ya ajabu na kufanya jina la Mungu linatukanwa kumbe ni kwa sababu ya ujinga ujinga tuu. hatusemi usifunge kuomba, hatusemi usiende kwenye semina hatusemi usimfate mchungaji unaempenda ila iwe kwa kiasi na ubalance kati ya kanisa na familia ili haya mambo yweze kwenda kwa amani bila ugomvi. Leo hii kila mtu hamtaki mwanamke mlokole kwa sababu hizi wakati nyie ndio mliokuwa wife material. Badilikeni sio wote ila haya yanayosemwa yapo kabisa. Mkipata wanayofanya wanaume walokole yasiyokuwa ya maana nayo yaleteni hapa wabadilike mambo mengine hayahitaji Biblia hata sisi tupo humo ndani na tunaona kabisa hii amefanya ni kwa sababu ya ujinga, hii yuko sawa wala hakuna shida ila wale dada zetu nasema kwa sauti kuu badilikeni.
 
Inanibidi niseme nisiposema basi hawa mabinti watazidi kujifaragua na kuhalibu sifa za wanawake wengine wenye maadili na hekima njema....
Ni hawa mabinti wa Kirokole...
Utasikia naenda kwenye mkesha,naenda kwa mwakasego,naenda kwa katunzi..naenda semina ya vijana,
Lakini sasa!!!!!!Daaaaah
Acha leo tuwachane live.....
NI nyie nyie.....
1.mnao ongoza kwenda makanisani na kwenye majukwaa ya semina za kikanisa WAKATI kwenye ndoa zenu hamjitolei sawasawa

2.Mnaongoza kujipendekeza kwa kuheshimu wachungaji na wazee wakanisa Wakati waume zenu hata tone la heshima hamna

3.mnaongoza kwa matendo mabaya kuliko hata wapagani wasiomjua mungu...ni waongo,wanafiki,wasengenyaji,wasiosamehe,wenye chuki mioyoni mwenu...

4.
mwisho ni kuwa ndo nyie nyie mnaongoza kwa kuvunja ndoa kila siku..tena ndoa zenyewe zilighalamika kwa kila khari...daaaaah!!!Hivi hawa watu wana matatizo gani???

ngoja nisimalizie.....

Wadau malizieni.......

mm ya kwangu ilivunjika bila huruma baada ya mke kuanza kusali makanisa hayo anafululiza mwezi mzima eti yupo mkesha!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mkuu punguza jazba maana umetumia hasira kurusha ujumbe. Inaonesha wazi shemeji yetu ameokoka so kuna kitu amemisbehave ndo umekuja huku kuwahukumu usiowajua THATS NOT FAIR!
Hakuna mtu asiye na madhaifu na kama hujui kuokolewa kunaanza ndipo tabia za mtu huanza kubadilika taratibu kwa kadri anavyopata mafundisho ya Kristo yaliyo sahihi,narudia YALIYO SAHIHI. neno ndilo humbadilisha mtu ila wokovu hupewa bure kwa kumuamini Yesu na kazi yake ya msalaba.

Siwatetei wadada waliomwamini Kristo aka kuokolewa kwani acjilia mbali wokovu suala la amekuzwaje liko palepale. So utamkuta Dada aliyeokoka mwongeaji sana, mkimya sana mkali sana mwenye hasira sana,mwenye upendo sana mkarimu nk nk.

Ni kama kusema mafisadi walioko bongo haimaanishi watumishi wa umma wote mafisadi au labda zile kashfa za mapadre wa Katoliki kulawiti watoto huko USA je tuconclude hata wazee wetu hawa wa hapa Tz wanafanya hivyo?? Hapana.

La msingi anayekosea na kufanya unafiki aambiwe yeye i asaidike kuliko kutomwambia ukaja kurusha huku.

Mwisho nakupa pole ya dhati maana hapana shaka kuna mtu amekukwaza bro

Hapana mkuu...nimefululuzia kuona ndoa tano za wanawake wakirokole sasa zinavunjika na ukiangalia tatzzo ni hawa wachingaji wanaosimama makanisani nakuwafundisha wanawake mafundisho ya kishetani...
 
mm ya kwangu ilivunjika bila huruma baada ya mke kuanza kusali makanisa hayo anafululiza mwezi mzima eti yupo mkesha!

Post sent using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu...mungu yuko pamoja nawe...
Siku zote mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenywe
 
Aysee ngoja nichangie kidogo hapa.

Yan unaweza sema wanafundishwa kuwa ukiwa na yesu huhitaji kingine kabsa maana kiburi kingi wanataka kuonyesha dunia kuwa wao ni zaid ya yeyote.

Kisa.

Yupo mama mmoja jina nahifadhi alikuwa mlokole kutoka kenya, amefikaje tz alikuja na mume wake ambae kwangu mimi ni ndugu yetu.

Sasa huyu mama ametukuta akina sisi tuna imani yetu basi akatuona tuko nyuma saaaaana kuhusu wokovu.

Mada yangu iko hapa.... Akawa anaona familia flani flani pale mtaani zinapishana kauli na zingine kuvunjika basi akawa anapiga propaganda kuwa hio nikwasababj watu wa pale kijijini kwetu hawana wokovu wajui kuomba wala hawakeshi kama yeye kwenye mikesha ya maombezi maana kristo amesema kesheni mkiomba.

Tena akajksifu mbele za wazazi wetu kuwa yeye ni shujaa wa ndoa maana anayesu ndani yake na mume hampi shida yoyote.

Navyoandika hapa mda huu kesi yao ya ndoa ni ngumu kuliko zote zilizowahi kutokea pale kijijini kwetu mpaka inaimarisha ndoa zingine kuwa isije ikafikia huko walipofikia wao.

Yani ni ngumu kweli kweli wameachana na habari ya kurudi kenya imenoga lakini vikwazo vingi kama mlima kitonga kutoka kwa mume anaemhendo.

Kanisa walilokuwa wanasali siku hizi hata hawajui limepakwa rangi gani.

Hata wakisikia kesho limehamia kwao hawataelewa sawa sawa maana hawana habari nalo.
 
nilikuwa nikiona wanashambuliwa nikawa nahamaki saa nyingine napatwa na hasira kusikia wanasemwa vibaya kwani hata mimi ni mpendwa ila nimekuja kugundua kwa wale ninaowajua kuna kaujinga fulani wanao vichwani. Mimi nasema wasemwe tuu hizi tabia ni kweli zipo unakuta wanaolewa na makanisa na kazi za makanisa pamoja na huduma mbalimbali za makanisa badala ya waume wao. Ndoa ya Benny Hinn ilivunjika kwa sababu ya yeye kutokuwa na time na mkewe akaja kukiri mwenyewe 'I WAS MARRIED BY MINISTRY AND I FORGET THAT I HAD MARRIED A WIFE' kabla ya maombi ya wapendwa kuiombea ndoa yake kurudiana, mwangalie na Pastor Chriss Oyakhilome ndoa ilivunjika kifupi hawa dada zetu tabia ni kama hizihizi sasa lazima wafahamu ya kwamba kwa jinsi Mungu anavyotupenda hawezi kusimamia ndoa yenu ivunjike kwa sababu ya ujinga wako kujifanya upo bize sana na kanisa unaacha kuwahudumia watoto, na mumeo kumbuka Mungu ndie aliekupa huyo mume na atakuonesha namna ya kuishi nae usifate mapokeo ya madhehebu yenu. halafu saa nyingine unakuta dhehebu linaongozwa na mchungaji ambaye Un-educated and not civilized anakulazimisha kufanya mambo ya ajabu yanyohatarisha ndoa still unafuata tuu bila kujudge hii ni hatari ndio maana madhehebu mengine Mchungaji lazima awe ana kiwango fulani cha elimu japo sii lazima ila hii huwa inasaidia sana kupunguza ujinga ujinga unaofanyika makanisani saa nyikngine huwa nikiona napatwa na hasira sana wanavyofanya mambo ya ajabu na kufanya jina la Mungu linatukanwa kumbe ni kwa sababu ya ujinga ujinga tuu. hatusemi usifunge kuomba, hatusemi usiende kwenye semina hatusemi usimfate mchungaji unaempenda ila iwe kwa kiasi na ubalance kati ya kanisa na familia ili haya mambo yweze kwenda kwa amani bila ugomvi. Leo hii kila mtu hamtaki mwanamke mlokole kwa sababu hizi wakati nyie ndio mliokuwa wife material. Badilikeni sio wote ila haya yanayosemwa yapo kabisa. Mkipata wanayofanya wanaume walokole yasiyokuwa ya maana nayo yaleteni hapa wabadilike mambo mengine hayahitaji Biblia hata sisi tupo humo ndani na tunaona kabisa hii amefanya ni kwa sababu ya ujinga, hii yuko sawa wala hakuna shida ila wale dada zetu nasema kwa sauti kuu badilikeni.
Point sana mkuu...
Wachungaji ufinyu wa akili na mapokeo ya kidini yawafanya wanakengeusha ndoa za watu...mchungaji akifikia hana neno wala hawezi kukemea wanafunzi wake hilo ni bogazi la.mchungaji...ni bora kuwa mpagani tu...
Hiz dini zingine ni matatizo matupu
 
Hapana mkuu...nimefululuzia kuona ndoa tano za wanawake wakirokole sasa zinavunjika na ukiangalia tatzzo ni hawa wachingaji wanaosimama makanisani nakuwafundisha wanawake mafundisho ya kishetani...
Soma vzr ujumbe wangu bro nimesisitiza mafundisho sahihi. Unajua dunia ya leo kwenye imani kuna mafundisho fake kibao si ktk ukristo au uislam.
Leo hii unakiri umefululiza kuona ndoa za hao waliookewa zikifa. Well siwatetei ila kama wanakishwa matango mwitu sishangai. Ni sawa tu na watu kama Boko haram au Isis ukiongea na muislam anayeijua dini yao atakwambia wale waongo hawaupiganii uislam japo wao wanajibainisha kbs kuupigania uislaam mfano ni hao bokoz.

So brother tatizo si wokovu bali mtu husika

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Point sana mkuu...
Wachungaji ufinyu wa akili na mapokeo ya kidini yawafanya wanakengeusha ndoa za watu...mchungaji akifikia hana neno wala hawezi kukemea wanafunzi wake hilo ni bogazi la.mchungaji...ni bora kuwa mpagani tu...
Hiz dini zingine ni matatizo matupu
hapana mkuu habari ya kuwa mpagani hapana Mungu ni mzuri kuliko unavyoweza kufikiri ila namna watu wanavyojiita wenyewe na kufanya matakwa ya wanadamu na sii ya Mungu. unaweza kukumbuka Yesu alikuwa anawaambia mnafanya matakwa ya wanadamu hamfanyi yangu. Mungu anatupenda sana kabla ya kufanya ukimuuliza atakuonesha namna ya kuishi na mkeo hata na mmeo pia. Shida inakuja pale unapopokea pokeo la mtu au la dhehebu. Roho Mtakatifu ni rafiki mzuri mno unaeweza kuwa nae shida tuu ni yale mapokeo ya watu na sii ya Mungu. Mungu yupo mkuu na anaishi mwamini upagani hapana maana when we depart from here there is another world and also there is a promise to live here after. Cha msingi tusome neno na tunsikilize zaidi Mungu anasemaje kuhusu ndoa zetu tuachane na mapokeo
 
Tatizo la Ndugu zangu Hawa wanaamini alichounganisha mungu binadamu hawez kutengua so wanaishi ilimradi,wanasahau wajibu wao kwenye ndoa zao ,wakati Chriss mauki kila Leo anafundisha,pia upendo,heshima na ibada ya kweli vinaanzia nyumbani kwa familia alokupa mungu,mchungaji ana yakwakwe khaaa!!

Post sent using JamiiForums mobile app
 
mm ya kwangu ilivunjika bila huruma baada ya mke kuanza kusali makanisa hayo anafululiza mwezi mzima eti yupo mkesha!

Post sent using JamiiForums mobile app
Sidhani kama kuna kanisa wanalokesha kila Siku. Kingine, uliongea nae? Na kama ndio alisemaje? Kwanini msingekwenda kumuona huyo mchungaji, mkamueleza?
 
Yaani hawajaelewa maana ya kuokoka,naona walifuata kutafuta kuolewa,maana mambo yao ya chinichini,kusengenya wengine ndio haswaaa wa kwanza,watachomwa vbaya hao

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Walokole hawako hivo, wasichafue majina ya watu, labda mtoa mada pia ujue sio kila anayesema ameokoka ndivo ilivo, la! Wengine hutumia jina flani kwa manufaa binafsi.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom