Hivi hawa wanaomsifia Magufuli huwa wanalala kweli?

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,511
2,000
Kama heading inavyojieleza, hivi hawa wanaomsifia magufuli huwa wanalala saa ngapi?

Kwa kipindi hiki ambacho huku niliko jiji ninaloishi liko chini ya zuio la kutoka nje ya nyumba, mitandao imekuwa sehemu yangu kubwa ya kutembelea mda wote kwa vile sina ratiba nyingine tofauti, kwa huko nyumbani Tz nimeshangazwa na vitu kadhaa kwenye mitandao.

Kuna baadhi ya account huko facebook, tweeter, Insta, JamiiForums na site zingine Kuna majina na ID kazi yao ni kumsifu magufuli tu haijalishi ni kuhusu nini tena bila hoja za msingi hawa watu hawako kwa ajili ya chama Wala serikali wao ni magufuli tu.

Cha kushangaza zaidi wako active mda wote yaani 24/7hrs na karibu kila taarifa au thread wao ndio wa kwanza kucomment, kipindi mimi nakuwa nimechoka na upweke wa kujifungia ndani kila nikiingia online naziona hizohizo ID kwenye kila post iwe mchana, adhuhuri, alasiri,usiku wa manane hata asubuhi. Hawa watu wanafanya majukumu yao saa ngapi na wanalala mda gani? na ni Kama wanaambiana yaani wanashambulia kwa pamoja, au ni mtu mmoja anamiliki ID zaidi ya 10? Ina maana hawa jamaa hawalali?

Mimi ninashangaa kwa sababu sijawahi kufikiria Kuna watu wa namna hii yaani uwe online 24hrs kila siku kwa ajili ya mtu tena kwa kuandika matusi kwa kila post? Labda Kama Kuna malipo wanapata, Anyway nimeshangaa tu wakuu

Mimi bado naendelea na Lock-down

Chukua tahadhari, Corona Ipo na ni hatari.
 

Nas Jr

JF-Expert Member
May 15, 2018
4,494
2,000
Mimi nishangaa kwa sababu sijawahi kufikiria Kuna watu wa namna hii yaani uwe online 24hrs kila siku kwa ajili ya mtu tena kwa kuandika matusi kwa kila post? Labda Kama Kuna malipo wanapata, Anyway nimeshangaa tu wakuu

Ni vijana wa Lumumba, na wapata ujira wa Elfu Saba kama posho ya kazi yao ya kusifu iliyotukuka...

Now you know
 

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
7,897
2,000
Sisi ni Jeshi kubwa, ni wanamapinduzi, kazi yetu ni kuelewesha, kuzima upotoshaji na kujenga hoja za Tanzania ya miaka 100 baadaye.
 

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,629
2,000
Timu gwajima ni ukabila tu hakuna kingine..........gwajima na makonda ndio waratibu wa kundi hili la kikabila......wanalipwa pesa ndefu sn sn
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom