Hivi hawa wana undugu wa mbali?!...

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Niko hapa navinjari kwenye michepuko ya JF, nimeshituka nakujikuta niko kwenye blog ya kaka Michuzi. Mvinyo wa mwaka 2001 toka Chile nilioubembeleza kwa masaa kadhaa sasa unaishia, nimeshusha robotatu ya chupa tayari, uliobakia uko kwenye bilauri, ninampango wa kuubwia kwa mpigo kabla ya kudondoka kitandani. Chicha limepanda naanza kuhisi kipandauso kitaniandama asubuhi au kutwa nzima kesho.

kabwe.jpg

Mpango wa kujiganga alfajiri kesho kwa bilauri mbili za maji kama ilivyo jadi umewadia. Kama lazima vile, najikokota kuchota maji na kuyaweka kwenye chupa ya plastiki, huu ni mtungi wangu wa cocacola nilioutunza kwa sababu kama hizi, nembo za cocacola zote zimeshafutika kwa kusurutishwa kila mara. Nauleta chumbani na kuutundika kwenye meza pembeni ya kitanda. Narudi kwenye tarakilishi yangu, na ghafla nikivinjari kwa Michuzi naona picha ya Waziri Mkuu, Mh. Pinda, nasita kuondoa macho, naikodolea macho picha mithili ya jamaa chakari aliyerudi usiku wa manane kutoka vilabuni na kujikuta asubuhi bado ana tenga kadhaa mfukoni.

pinda.jpg

Naendelea kuiangalia picha huku macho yakigubikika kila baada ya sekunde mbili tatu. Najaribu kuidadisi huku nikipambana na usingizi wangu maana mapema leo hii mchana nilikumbana na picha ya Mh. Zitto kwenye blog mojawapo ya Mtanzania mwenzetu, kama unampango wa kuniuliza kama nilikuwa tungi pia, jibu ni hapana, sikuwa bwii hata kidogo. Basi nami kuona taswira za waheshimiwa hawa zina ulinganifu wa aina fulani hivi, napekesha kwenye blog ya kaka Michu ili kupata picha nyingi zaidi. Nafanya zoezi hilo kwa karibia robo saa....... Badala yake, pamoja na umri wao kupishana, naishia kuibuka na swali moja tu, je, hawa waheshimiwa ni ndugu?!! Naomba unisaidie kama unaweza, natumaini kesho nikiamka bila kipandauso nitapata kuongeza zaidi uelewa wa viongozi wangu. Nakutakia mapumziko mema ya mwisho wa juma. Alamski!

kabwe2.jpg

Wewe nilishakwambiaga hayo manywaji ya pwani uyaachage, na usitudanganyage eti maWaini ya Chile. Yaani asavali ungesema hata Dodoma waini tungekuamini.
Mwanawane kwani siyo wewe hapo uko na Brazameni mnachanganya mambo?? Hebu rekebisha hako ka fotola.
mnazi.jpg
 
mmhhhhhhh haya .

ila usishangae akawa ni mwanawe
 
Wewe nilishakwambiaga hayo manywaji ya pwani uyaachage, na usitudanganyage eti maWaini ya Chile. Yaani asavali ungesema hata Dodoma waini tungekuamini.
Mwanawane kwani siyo wewe hapo uko na Brazameni mnachanganya mambo?? Hebu rekebisha hako ka fotola.
mnazi.jpg

Ha ha ha ha, Ng'wanone huo mvinyo nilibahatika kuletewa na rafiki yangu aliye ughaibuni alipokuja likizo, nimeutunza muda mrefu ili uchachafike... si unajua tena, kadiri unavyokaa ndiyo unaongezeka thamani.. lol

picha hii hapa, brazameni nilimwambia tuupeleka huu mnazi kule Mikoroshoni akasema hamna haja sana, utanyweka huku huku Kawe!!

Aisee!

Hiyo togwa ya mnazi au tembo imenitia kiu ya kweli.
Huku ughaibuni tunakunywa ulabu unaokosa hewa ndani ya chupa, ni kipole hata sijui waligema lini.(Bia).
Picha nyingine msilete hapa zina mshawasha, kwa sababu watu tunaweza kata tiketi za ghafla kurudi kwetu kwa kiu ya Tembo.

Duu!
 
haya mapombe ya kienyeji yanatukumbusha mbali sana,ULANZI,kwa sana jkt mafinga,lazima ikuharibu joints,basi on your way back kambini,pale kwenye ka mto lazima utumbukie.wenye kumbukumbu tukumbushane,eti ile pombe ya kienyeji ambayo kabla ujanywa inabidi ufunge suruali chini kwenye miguu,maana punde ukiinywa lazima uharishe,nikumbusheni hii pombe jina please
 
Inaitwa Pingu,siku hizi inapatikana sana Moro,ila msimu wa Ulanzi tayari umekaribia sana, masikini marehemu jkt ulitupa mengi.
 
Back
Top Bottom