Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,273
Niko hapa navinjari kwenye michepuko ya JF, nimeshituka nakujikuta niko kwenye blog ya kaka Michuzi. Mvinyo wa mwaka 2001 toka Chile nilioubembeleza kwa masaa kadhaa sasa unaishia, nimeshusha robotatu ya chupa tayari, uliobakia uko kwenye bilauri, ninampango wa kuubwia kwa mpigo kabla ya kudondoka kitandani. Chicha limepanda naanza kuhisi kipandauso kitaniandama asubuhi au kutwa nzima kesho.
Mpango wa kujiganga alfajiri kesho kwa bilauri mbili za maji kama ilivyo jadi umewadia. Kama lazima vile, najikokota kuchota maji na kuyaweka kwenye chupa ya plastiki, huu ni mtungi wangu wa cocacola nilioutunza kwa sababu kama hizi, nembo za cocacola zote zimeshafutika kwa kusurutishwa kila mara. Nauleta chumbani na kuutundika kwenye meza pembeni ya kitanda. Narudi kwenye tarakilishi yangu, na ghafla nikivinjari kwa Michuzi naona picha ya Waziri Mkuu, Mh. Pinda, nasita kuondoa macho, naikodolea macho picha mithili ya jamaa chakari aliyerudi usiku wa manane kutoka vilabuni na kujikuta asubuhi bado ana tenga kadhaa mfukoni.
Naendelea kuiangalia picha huku macho yakigubikika kila baada ya sekunde mbili tatu. Najaribu kuidadisi huku nikipambana na usingizi wangu maana mapema leo hii mchana nilikumbana na picha ya Mh. Zitto kwenye blog mojawapo ya Mtanzania mwenzetu, kama unampango wa kuniuliza kama nilikuwa tungi pia, jibu ni hapana, sikuwa bwii hata kidogo. Basi nami kuona taswira za waheshimiwa hawa zina ulinganifu wa aina fulani hivi, napekesha kwenye blog ya kaka Michu ili kupata picha nyingi zaidi. Nafanya zoezi hilo kwa karibia robo saa....... Badala yake, pamoja na umri wao kupishana, naishia kuibuka na swali moja tu, je, hawa waheshimiwa ni ndugu?!! Naomba unisaidie kama unaweza, natumaini kesho nikiamka bila kipandauso nitapata kuongeza zaidi uelewa wa viongozi wangu. Nakutakia mapumziko mema ya mwisho wa juma. Alamski!