BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 327
- 414
HIVI HAWA WAKO SAWA HAWA?. HAWA NDO TUWAPE MADARAKA?
Utawasikia kwenye mikutano au mitandaoni kwamba Watanzania hawana hela, hali yao mbaya mara nyie mafukara na maneno mengi sana ya kejeli na dharau kwa Watanzania lakini wakimaliza mikutano yao utasikia wanaanza kutembeza mabakuri kuchangisha hela kwa hao hao waliowasema kwamba hawana hela na mafukara. Hivi uzwazwa gani huu wanatuona Watanzania? Yani wanatudharau kiasi hiki halafu muda huo huo wanatutaka hela zetu. Mbona wanatuona Watanzania kama watoto wadogo na wanachezesha sana akili zetu. Hawa ndo tuwape kura hawa?
Ooooh!!! mara Tanzania hakuna uhuru wa habari, vyombo vya habari vinapendelea mara vyombo vya habari vinalalia upande mmoja halafu hao hao wanawafukuza TBC waliokuja kuwasapoti na kuwaonyesha kwamba Tanzania uhuru wa habari upo na hakuna anayependelewa. Hawa ndo washike madaraka hawa?
Halafu angalia wanavyowatukana, kuwadhalilisha na kuwavua utu wao watumishi wa umma wa nchi hii wanaofanya kazi kubwa kwa maslahi ya Watanzania wote kwa kuwaita eti wameokotwa majalalani. Yani hawa mawaziri wanaotatua kero za watu kila siku leo wamajajalani? Wakuu wa mikoa kwa wilaya, wakurugenzi, maafisa tarafa, kata, vijiji na watumishi wa umma wameokotwa jalalani? Dharau gani hii halafu ndo tuwape kura hawa?
Huu ni udhalilishaji na matusi makubwa kwa Watanzania wote wa nchi hii tena udhalilishaji unaotoka kwa watu wanaotaka tuwape madaraka. Tukaokomeshe siku ya Jumatano. Yani tumshukuru Mungu tu na tukawaadhibu kwa hasira kwenye sanduku la kura Oktoba 28. Hawawezi kutudharau kiasi hiki.
0657475347.