Hivi hawa wachoma mahindi wa Mbezi Beach, ni mbwembwe tu au kuna siri gani kibiashara?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,381
26,721
Hebu tulione hili wakuu, hawa jamaa kipande cha Mbezi kuanzia TangiBovu hadi Africana.

Wanapochoma mahindi huweka pia mashina yake, yaani ni kama wameyang’oa shambani na miti yake.

Kisha hufanya kama kivuli kwenye kilinge, hata kama sio kivuli japo mawili matatu kuashiria kuna mahindi mabichi.

Hii sijawahi kuiona sehemu nyingine yoyote, sijui kama ni ujivuni tu kama ilivyo kwa wakazi wa maeneo hayo, au kuna sababu kibiashara..?

Na kila siku utakuta majani yake mabichi kabisa [hayakauki], hebu mwenye kujua tafadhali atuambie, vinginevyo naona wanachafua barabara zetu tu.

Note:
Usiniulize kama mahindi yao hayahitaji ndimu wala chumvi au yale yale tu, muhimu usisahau kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ndipo ufakamie mahindi yako.

View attachment 1406005View attachment 1406006
 
Duh hivi kumbe kuna watu hawajawahi kuona ‘miti’ ya mahindi.? Basi picha nikipita mitaa hiyo tena, muweni na subira.
 
Hebu tulione hili wakuu, hawa jamaa kipande cha Mbezi kuanzia TangiBovu hadi Africana.

Wanapochoma mahindi huweka pia mashina yake, yaani ni kama wameyang’oa shambani na miti yake.

Kisha hufanya kama kivuli kwenye kilinge, hata kama sio kivuli japo mawili matatu kuashiria kuna mahindi mabichi.

Hii sijawahi kuiona sehemu nyingine yoyote, sijui kama ni ujivuni tu kama ilivyo kwa wakazi wa maeneo hayo, au kuna sababu kibiashara..?

Na kila siku utakuta majani yake mabichi kabisa [hayakauki], hebu mwenye kujua tafadhali atuambie, vinginevyo naona wanachafua barabara zetu tu.

Note:
Usiniulize kama mahindi yao hayahitaji ndimu wala chumvi au yale yale tu, muhimu usis!ahau kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka ndipo ufakamie mahindi yako.
A picture speaks louder than a thousand words! WEKA PICHA YA HAYO MAHINDI TUPATE POINT ZA KUCHANGIA VIZURI ZAIDI.
 
Wale wa kuhitaji picha ya mahindi.
IMG_5839.JPG
 
Mi nafikir n mbinu mpya ya biashara ili kuaminisha wateja kwamba mahind n ya Leo Leo tofauti na mengn utakuta yameka siku 3.
Hii Ni sawa na ukifika mfani izazi barabar ya Iringa- Dodom utakuta wanauza nyama ya mbuzi pemben wamening'iniza kipand Cha mkia au mguu ambao haujanyonyolewa.

Bila hivo watu wasinge nunua wakihic nyama ya dog!
Picha haziko vizuri ila ni afadhali kuliko bila bila.
View attachment 1406009

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom