Hivi hawa wabunge wanaotoka bungeni wakati vikao vinaendelea wanakuwa wapi muda huo?

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi na hata kidato cha kwanza hadi cha nne, nilisoma na wanafunzi ambao kwa kutotambua umuhimu wa kuhudhuria msomo darasani na hata shughuli za nje baada ya masomo walikuwa na mfumo wao wa maisha tofauti kabisa na utaratibu wa shule.

Wengine walikuwa wakikusanyika vichakani wakivuta bangi, sigara, kula kuberi na hatimaye kujikuta miili yao inakuwa na matamanio ya kujamiiana.Wengine kwasababu tu hawapendi kusoma walibaki mabwenini wakiwa wamelala, wao suala la kufuata ratiba ya shule ilikuwa ni majaribu kabisa, wakati wengine tulihaha kukimbia huku na kule kunywa uji, kuoga baada ya usafi ili kuwahi mstarini na hatimaye kuanza masomo kwa wakati, wao ndiyo kwanza uliwaona wanatoka vitandani tena kama wamelazimishwa vile.

Takribani wiki tatu sasa wabunge wa upinzani wakishasaini mahudhurio ili kujihakikishia posho ya siku hiyo, huondoka na kutokomea kusikojulikana. Wabunge hawa wengi wao wana familia kwa maana ya mbali na kuwa na watoto, pia wana wake/waume zao. Wenzi wao hawa wengi wako mikoani. Wengine hawajaolewa wala kuoa lakini ni watu wazima lazima wana wenzi au wachumba.

Kuwa Mh. mbunge haina maana mahitaji ya kimwili yanakoma na wala tabia ya mtu haiwezi kukoma kwasababu tu ya kuitwa mheshimiwa. Tena unapokuwa hauna kazi matamanio ya mwili yanakuwa ya kiwango cha juu(siyo mtazamo wangu, ni utafiti wa kibaiolojia).

Hawa waheshimiwa wabunge wanakuwa wapi muda wote huo ambao wamekuwa wakitoka bungeni saa 3:00 asubuhi hadi kesho yake tena saa 3:00 asubuhi, masaa 24 bila kazi?

Mytake: Napendekeza sheria ya kuwataka wabunge wasiohudhuria vikao vya bunge bila sababu kutolipwa posho iwatake pia kuondoka katika mji wa Dodoma ili wakaungane na familia zao na hivyo kuwaondolea vishawishi ambavyo vinaweza kupelekea wakasaliti ndoa zao kwasababu tu ya miili yao kukaa kujishughulisha.

Hii pia itauacha salama mji wa Dodoma na wakazi wake hususani tatizo la watoto wa mitaani, migogoro katika ndoa za wenyeji n.k.
 
....si unajua UDOM ipo na hivi boom halitoshi. ...ulabu a.k.a kupombeka, maana mjengoni pana bana sana.
 
Pia nahisi ndoa nyingi za wabunge wanaogomea vikao vya bunge zitavunjika kwa sababu ya hao wabunge kuwa na muda mwingi idle hapo i dodomya, na sasa wengi watakuwa wanaendekeza kale ka mchezo ka baby
 
Shingongo kawa mzembe sana,ile timu yake ya fichua maovu ilitakiwa iweke kambi hapo Dom.

Angeuza sana magazeti
 
Huwa wanakuwa library ya bunge wakisoma siunajua hawa ni tofauti na wa CCM......
 
Huwa wanakuwa library ya bunge wakisoma siunajua hawa ni tofauti na wa ccm......
Library ipi? Mbona hatuoni habari yoyote ikielezea hwepo wao huko? Wenye vijisichana vya shule na wake zao hapo Dodoma wachukue tahadhari.
 
Library ipi? Mbona hatuoni habari yoyote ikielezea hwepo wao huko? Wenye vijisichana vya shule na wake zao hapo Dodoma wachukue tahadhari.
Unadhani kujua kwao mambo kunatokana na nini kama sio kujisomea, kujadiliana na kufanya tafiti?
Lini uliwahi kumsikia Mbunge wa upinzani anasema Gadaffi ni rais wa Kuwait?
Hao wa kwenu wenye kiwango cha juu cha ujinga ndio wanaokuja na hoja za sanamu ya Diamond na vichekesho vingine.
Mie nilidhani baada ya kuliondoa lile batch la kina Asumpta Mshama kutakuwa na nafuu kumbe mumeongeza malumbesa mengine?
 
Back
Top Bottom