Hivi hawa Viongozi wa Vini kwanini wanamdhihaki Mungu kwenye mikutano ya Kisiasa?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
708
1,000
Ninaomba ufafanuzi kidogo kuhusu hawa Viongozi wa Dini ambao huongoza dua na maombi kwenye mikutano ya kisiasa.

Ninachojua mimi ni kwamba, hawa ni viongozi wanaoongoza waumini wenye itikadi tofauti ndani ya madhehebu yao, chaajabu ni kwamba ukisikiliza Sala na maombi yao unakuta badala ya kua maombi ya kuelekezwa kwa Mungu atimize mapenzi yake, maombi hayo yanakua sehemu ya kampeni kwa mgombea husika na chama chake.

Je, huku sio kumdhihaki Mungu? Je, huku sio kuwakwaza waumini wasiomtaka mgombea unaemuombea? Lakini pia ni kwanini tumwingize Mungu kwenye mambo ya siasa ambayo yamejaa uchafu wa kila namna?

Mi nadhani ili kuondoa hii sintofahamu, kuwe na wasoma dua ambao wanatambuliwa, na kupitishwa na tume ya uchaguzi na hao watu watasoma dua na sala kwa vyama vyote na sio kila chama kutafuta wa kwake.

Alafu kwenye hiyo dua au sala, isionyeshe kwamba msomaji anamtaka nani, Ila anamuomba Mungu awajalie wananchi kumpata kiongozi mzuri ambae ni Mungu pekee anaemjua.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom